20 June 2011

Simba yapigwa mwereka Congo

*Yafurushwa michuano CAF

Na Mwandishi Wetu, Kinshasa

WAWAKILISHI wa Tanzania katika michuano ya Shirikisho, Simba jana iliduwazwa Jijini Kinshasa baada ya kufungwa mabao 2-0 na DC Motema Pembe ya
jijini hapa.

Simba katika mechi hiyo ilikuwa ilitakiwa kupata angalau sare ya aina yoyote, ili iweze kutinga hatua ya makundi katika michuano hiyo kutokana na ilikuwa na akiba ya bao moja ililopta Dar es Salaam wiki moja iliyopita, lakini umakini wa mabeki umeiponza timu kutolewa.

Wawakilishi hao wa Tanzania waliipata nafasi hiyo, kingekewa baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuiengua TP Mazembe katika michuano ya Klabu Bingwa pia Congo DRC kutokana na kumchezesha mchezaji asiyestahili.

Hata hivyo Simba baada ya kuchukua nafasi hiyo, ilitolewa na Wydad Casablanca ya Morocco kwa mabao 3-0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja huru Cairo, Misri.

Baada ya Simba kutolewa katika michuano ya Klabu Bingwa ikapata nafasi ya kucheza michuano hiyo ya CAF, ambayo jana ilizimwa kwa kwa kufungwa na Motema Pembe. 

Kutokana na matokeo hayo, DC Motema Pembe imepata nafasi ya kucheza hatua ya makundi baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 2-1.

Katika mechi hiyo Simba iliingia uwanjani na kucheza kwa tahadhari kubwa, lakini hata hivyo haikuweza kuwasaidia kwani Motema Pembe ilipata bao la kwanza dakika ya 38 kupitia kwa Bokota Labama.

Bao hilo lilipatikana baada ya kutokea kizazaa langoni mwa Simba kutokana na mpira wa krosi ambao kipa, Juma Kaseja alijaribu kuokoa lakini mwamuzi akaelekeza mpira kuwekwa kati kwani mpira ulishavuka mstari wa goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo DC Motema Pembe ilipata bao la pili kupitia kwa Tresor Salakyaku baada ya mabeki wa Simba kufanya uzembe katika harakati za kuokoa..

1 comment:

  1. Tumeshazoa kushindana Simba na Yanga basi.Lakina katika mashindano ya kimataifa ni sifuri.Tangu mwanzo maandalizi ya simba hayakuwa mazuri.Unatajia kucheza na DC Motema pembe alafu unakwenda kujipima nguvu na timu ya mchanganyiko ya mkoa wa Tanga.Hivi kweli hayo ni matayarisho?Hata kabla ya mechi na TP Mazembe,Twalibu alisha waambia ya kuwa mnatakiwa kupata michezo ya majaribio na timu kubwa lakini ni kama mawazo yaliingia katika upande mmoja wa sikio na kutokea upande wa pili.Mkapoteza huo mchezo.Mkapata bahati tena ya kurishwa katika mashindano tena dhidi ya Waydad casablanca ya morroco mkarudia matayarisho yaleyale na kutolewa.Hii nafasi ya mwisho mliopata mmerudia yaleyale.Nyie kazi yenu ni kucheza mpira kwenye magazeti na maneno mengi mdomoni.Mpira hauchezwi kwa mdomo,vitendo ndio vinavyo takiwa.

    ReplyDelete