Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Yanga na Gor Mahiya ya Kenya Kampuni ya Smart Sports, imetangaza viingilio ambapo jukwaa kuu
kitakuwa sh. 10,000, mzunguko sh. 1,000 na watoto sh. 1,000.
Akizungumza kwa simu jana akiwa Jijini Arusha, George wa Kuganda alisema mechi hiyo itachezwa keshokutwa kama ilivyopangwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Alisema maandalizi ya mechi hiyo, ambayo imedhaminiwa na Kampuni ya Aspire Media ya Jijini Arusha tayari yamekamilika kkinachosubiriwa sasa ni mtanange huo ambao Yanga watauchukulia sehemu ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame.
"Kila kitu kinakwenda vizuri na timu hizo na timu zote zinatarajia kuingia jijini hapa Jumanne kwa ajili ya kipute hicho," alisema Wakuganda.
Akiizungumzia mechi hiyo, Timbe alisema itakuwa kipimo kizuri kwake kuwajua wachezaji wake wapya waliosajiliwa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Alisema baada ya mechi hiyo, ataweza kupata kikosi cha kwanza ambacho atakitumia katika michezo mbalimbali inayowakabili.
We Wakuganda naona hata akili zako zimeganda Kiingilio ni shillingi elfu kumi na mzunguko ni elfu moja ambayo inalipwa na watu wazima alafu bado unataka na watoto pia walipe elfu moja kama watu wazima hivi nyie hamna watoto?
ReplyDeleteNyie ndio mao sababisha watoto kuanza udokozi majumbani mwao.