01 July 2011

Shibuda awatunishia misuli CHADEMA

Na Grace Michael, Dodoma

SIKU moja baada ya uongozi wa CHADEMA na Kambi ya Upinzania kuahidi kumshughulikia Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA), Bw. John Shibuda kwa
kutofautiana wazi na msimamo na sera yao, yeye amesema kuwa yuko tayari kuhojiwa iwapo kama atatakiwa kufanya hivyo lakini akasisitiza kuwa hakupingana na sera wala ilani ya chama hicho.

Alisema kuwa alichokifanya bungeni cha kuiomba serikali kuongeza posho hiyo, ilikuwa na maana ya kumsaidia mbunge 'maslahi ya jamii wa chama jamii' ambaye lengo lake ni kuwatumikia wananchi kwa muda wowote na kwa shida yoyote.

Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu, akiwa mjini hapa, Bw. Shibuda alisema pamoja na msimamo wake kuonekana kuwakera baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa chama, hawezi kubadili msimamo au mtazamo wake kwa kuwa yuko sahihi kwa alichokifanya.

Alisema kuwa anasikitikika kuona chama kama CHADEMA ambacho ndio tegemeo kubwa kwa wananchi kutokana na namna kinavyotetea maslahi ya wananchi kuona hakiishi migongano.

“Nawasubiri waniite, nikiitwa nitakwenda kuhojiwa lakini natoa tahadhari kwamba hao ambao wamezungumza katika vyombo vya habari vya leo (jana) wasishiriki katika vikao vya kunihoji kwa kuwa tayari wamepoteza sifa ya kufanya hivyo,” alisema.

“Mbowe na Zitto ambao tayari wamenihukumu hawana sifa za kunihoji kwa sababu tayari wameshanihukumu, ila nasema baada ya kunihoji nitakwenda kwa Watanzania, nitakwenda kwa wananchi wa Maswa kuwaeleza mtazamo wangu na ukweli wa msimamo nilioutoa bungeni.

“Nitakwenda kufafanua mchango wangu 'mbunge masilahi ya jamii ambaye hafungi simu na ambaye anashiriki mambo mengi, mimi ni kiongozi kiyoyozi kwa wananchi kwa kuwa nashiriki kila jambo la wananchi na shida zao,” alisema Shibuda.

Pamoja na hayo mbunge huyo alisema hana ugomvi na mtu yeyote wakiwamo wanachama wa CHADEMA kwa sababu kukosana kwa askofu au kukosana ma shekhe siyo kukosana na msahafu au biblia.

Alisema kuwa, siku zote ukweli hauogopi mahakama wala polisi kwa sababu ukweli haubadiliki kwa ukaidi wa unyapara wa mtu yeyote bali ukweli utabaki kuwa ukweli siku zote.

Alisema kuwa anatarajia kufanya mikutano ya hadhara na kueleza ukweli wa hoja yake ili wananchi wajue ukweli wa suala hilo.

Kutokana na hali hiyo, aliwaomba wananchi na wanachama kwa ujumla kutulia katika kipindi hiki kwa kuwa yeye ni mtu anayesimamia uwazi na ukweli na kamwe hatafunika ukweli kwa maslahi ya wachache.

“Umaskini wa cheo si ufukara wa hekima, hivyo wasitugandamize kwa vyeo walivyonavyo…nimejifunza mengi na ninajua nilichokifanya,” alisema Bw. Shibuda.

17 comments:

  1. Huyu Shubyda ni pandikizi inatakiwa atolewe CHADEMA as soon as possible,sio siri bado ana fikra mgando za kiCCM hataki kwenda na mabadiliko.Wangejua CHADEMA wangemuacha na murder kesi yake wasingemsaidia hizo hoja zake angemueleza JAJI.

    ReplyDelete
  2. Umaskini wa cheo si ufukara wa hekima, hivyo wasitugandamize kwa vyeo walivyonavyo…nimejifunza mengi na ninajua nilichokifanya,”
    Huna lolote bw shibuda, we ni msaliti na utakufa msaliti. Baba wa taifa aliwahi kusema, ' mtu akishaonja nyama ya mtu hawezi kuacha tena'' na wewe umeshaonja dhana ya usaliti ukakiasi chama na wanachama walikupa thamana, na chama ulichoachiwa na babu zako, ukasaliti, ukauwa na ukala nyama ya ccm, hata huku chadema tunajua utafanya hivyo, kwani muda uliotumia CCM ni mara dufu ya wa chadema lakini ulivyo na damu ya usaliti huko kooote ulikotelewa na ccm ulipuuza ukiasi ukakimbia..... Leo hata ukirudi kwetu wananchi tutakukanya kama ulivyoikana CCM. Kama wewe ni CDM lazima sera na itikadi na katiba vyote vilandane na chama. Hutakaa ufanye chochote cha manufaa kwa nchi yako kwani dhambi ya usaliti imekuaa hata macho yako mwenyewe yanaonyesha.... Si ajabu ukamsaliti hata mkeo na familia yako ukakimbilia ughaibuni... Shame upon yourselve!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Mr. Shibuda naona unatumia neno hekima bila kulielewa maana yake. Mtu mwenye hekima hasemi mambo kwa kujitangaza kwamba yeye ni mbunge maslahi jamii, hii inapimwa na watu wenye hekima na akili. Lakini si ajabu kwani watu wengi wenye ufahamu mdogo hawafahamu pia kwamba wako hivyo na hudhani kuwa watu wote wako kama wao. Unasimamia kwenye uhuru wa kuongea: hata hapa tena umetumia neno usilolifahamu. Ebu fahamu kwamba baada ya kukubali kuwa mwanachama na tena mbunge wa CHADEMA; uhuru wako unapimwa na jinsi unavyolandana na yale yaliyomo katika CHADEMA, zaidi ya hapo unaleta fujo. Kwa maneno mengine wewe ndiye uliyejihukumu na kupoteza sifa za kuwa Mwanachadema na mwana upinzani. Usingoje sasa mpaka wenzako akina Zito au Lissu wakuvue gamba. Umechemsha mzee!

    ReplyDelete
  4. Huyu Shibuda asitudanganye, kama anatumia fedha hizi kwa ajili ya wananchi? Kama kweli anataka zitumike hivyo basi apendekeze posho hiyo ipelekkwe kwenye mfuko wa jimbo wa maendeleo halafu ikaguliwe na CGA! Vinginevyo asichukua haki yetu na kudai kutukirimia!

    ReplyDelete
  5. Huyo shibuda si mwanamapinduzi halisi roho ya usaliti imemtawala,bora atupwe nje ya Chadema 2baki na watu wenye roho ya kizalendo.Hiyo posho aitakayo si kwa manufaa ya wananchi wake wake wa Maswa, so watu take care hamna mbunge hapo.

    ReplyDelete
  6. Okotaokota hizi CHADEMA wawe makini wakati mwingine.Shibuda CCM damu kilichompeleke CHADEMA ni kutaka ubunge tu.

    ReplyDelete
  7. shibuda ulishakula nyama ya mtu ya ufisadi ccm, rushwa na kupenda vipochopocho. huwezi kuacha; nyama hizo za watu zitakuua pamoja na huyo hawala yako mwandishi mlevi.

    mumesukani huku halafu mnaandikia upuuzi wenu wa kitandani. eti mliongea kwa simu wapi, wapi na wapi si museme ukweli mlipokuwa? walevi na malaya wakubwa

    ReplyDelete
  8. Nyie mbwa wa Slaa hamna akili ni juzi tu Shibuda alipotukana ccm mlimsifia na kumuita shujaa leo mnamtukana,hata huyo Zitto wenu anyesema Shibuda afukuzwe anakula matapishi yake hakumbuki mara ngapi amenusurika kufukuzwa? ati leo naye anasema mwenzie afukuzwe. Hawa ni madikteta na Watanzania mtakiona cha moto,ole wenu. Ni ajabu kila jambo au wazo linalopingana na wachaga au slaa tayari moto unawaka,picha kamili hiyo Watanzania,viongozi wa chadema wanafanya hila za kidikteta ili waogopewe ole wenu mtakiona cha moto saa mtakapojaribu kuwapinga hawa wachaga

    ReplyDelete
  9. Jamani hawa viongozi wa chadema mbona kila siku kazi zao ni kulumbana. Sijasikia hata siku moja mbunge wa chadema akaongelea maendeleo aliyoyapeleka jimboni kwake. Inasikitisha kuona badala ya kuwaleatea maendeleo wananchi kazi ni kujitafutia umaarufu.

    ReplyDelete
  10. Well Done Shibuda. Mbunge anatakiwa afanye maamuzi magumu. Swala la posho limebuniwa na viongozi wetu ili wapande chati kwa wananchi. wanachokisema sicho wanachokitaka. Ni wanafiki tu.

    Kama ulivvyosema kukosana na askofu au kukosana na shekhe siyo kukosana na msahafu au biblia

    ReplyDelete
  11. Hao viongozi wa chadema wanapata hela nyingi za misaa kutoka nje. Badala ya kuziingiza katika chama kwa maslahi yetu wote wana chadema wanazila wao. hivo hawana shida ya hela. upo ushahidi.

    Tunapenda wasema kweli katika chadema na sio wambeya. Tunataka chadema kiwe chama cha watanzania wote. kisiwe cha kabila au kanda fulani. Huyo Zitto mwenyewe anaonekana ni tishio kwa wakubwa wawili. Hawampendi

    ReplyDelete
  12. Meno hayagongani yanagusana tu..............CHADEMA nini mustakabari wetu mbona migongano kila siku.. Hivi mlipompokea Shibuda hamkujua kuwa ukiona mbwa yuko juu ya paa ujue kapandishwa? Cha kufanya ni kupoza tu maana mkimtimua mnazidi kutuchanganya wanachama. Chungu cha ugali kikichemka na kumwaga maji tia unga.....Mh Mbowe tumia busara yako kudhibiti huyo kiumbe atakuchanganya Mwenyekiti wangu. Si unajua mzazi akizaa taahira hawezi kumtupa na ndio maana yake kuwa Mungu ameshakupa mzigo ubebeni mpaka mwisho. Poleni

    ReplyDelete
  13. Acheni munaosifia ujinga. Huyo Shibuda alishaanza kuonyesha Jeuri Mapema. Chadema ndio chama dume kisichoogopa mwenye pesa wala mavi ya kenge. Shibuda anadhani yupo CCm penye kitishia nyau?? Rejea uchaguzi wa vijana utaona usafi wa Chadema. Mbowe, Zito,Slaa. Timueni hiyo takataka.

    ReplyDelete
  14. Shibuda anapoikosoa na kuishambulia ccm chadema mnasema sawa bwana shibuda! hukustahili kupoteza muda wote ulioutumikia chama cha mafisadi na sio mara moja shibuda amekuwa ni mbunge mwenye fikra zake binafsi hata alipokuwa ccm na hatuja wahi kuwasikia ccm wakitamka watamfukuza kwa kauli zake hizo leo amefungua mdomo wake mara moja tu kinyume na utashi wa chadema mnamwita msaliti,wasaliti ni chadema kwa nini viongozi wa ngazi za juu wa chama wanapita wakipanuwa midomo yao kwenye vyombo vya habari kabla ya kuwasiliana naye? vipi kama muheshimiwa samuel sitta angekuwa chadema na jinsi anavyokishambulia chama chake cha cmm iposiku ushasikia waziri mkuu au katibu wa ccm akitamka sitta atafukuzwa chadema mtake msitake haina haja ya kwenda mbali kiutawala mnatakiwa mjifunze kutoka ccm baadhi ya ajenda zenu ni nzuri kiutawala bado kabisa kila kukicha migogoro ndani ya chadema mnatumia nguvu kuliko busara hiyo sio demokrasi kwani demokrasi ni mfumo unaohitaji uvumilivu wa hali ya juu na kukubali kushindwa kihoja au kimatekeo.

    ReplyDelete
  15. Mnaosema Shibuda kasaliti CDM mnakosea. Kawasaliti watanzania wanaopigana na ukoloni wa CCM. Hili swala ni zaidi ya sera za CDM. Hapa ni zaidi ya kusaliti CDM ni kuwasaliti watanzania wanaoumizwa na mfumo wa ulaji wa ccm. Laiti Shibuda angepingana na sera za CDM kama kuwepo kwa majimbo na kuleta mfumo mbadala tungemsikia lakini katika hili hana wa kumlaumu kwani katusaliti wananchi na kuunga mkono ufujaji wa fedha kwa serkali.

    ReplyDelete
  16. Shibuda ni Mnafiki numba moja, tuanze kuwaondoa kimyakimya watu kama hawa, wataliponza taifa kwa unafiki wao wa kupenda madaraka.Wanaleta mifarakano kwa jamii

    ReplyDelete
  17. demokrasia gani mliyonayo?Zito alitaka kugombea uenyekiti Mbowe na mkwe wake mavi debe,hao wasio wachaga wanatumiwa tu Lissu na Zito siku yenu inakuja,kama mnabisha jaribuni kugombea uenyekiti muone.napenda kuwaambia nyie WACHAGA, kazi inayowafaa ni wizi tu,nchi hamuipati

    ReplyDelete