*Wabunge wake waandika barua nao wakatwe
Na Pendo Mtibuche, Dodoma
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema kuwa tayari kimeandaa barua ambazo kitaziwasilisha kwa Waziri wa Fedha, Bw. Mustafa Mkulo kuelekeza posho za
vikao kwa wabunge wanne wa chama hicho zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo kwa Mkoa wa Kogoma.
Mkuu wa Idara ya Habari na Uenezi wa chama hicho, Bw. David Kafulila alisema hayo jana kuhusu Bajeti ya mwaka 2011, 2012 na kubainisha mambo mbalimbali juu ya ukuaji wa uchumi, deni la taifa, misaada na mikopo na suala zima la vipaumbele katika uchumi wa nchi.
Msimamo huo wa NCCR-Mageuzi unaunga mkono hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni inayoongozwa na CHADEMA ambayo tayari imeweka msimamo huo, huku Waziri Kivuli wa Fedha, Bw. Zitto Kabwe akienda mbali zaidi kwa kuwasilisha barua ofisi ya bunge kutaka posho zake za vikao zipelekwe kwenye taasisi ya Kigoma Development Initiative (KDI).
Bw. Kafulila alisema kuwa mbali na kupendekeza posho zao kuelekeza kwenye miradi ya maendeleo, pia wanapendekeza posho zote zikatwe kodi ili kuongeza mapato ya ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mbunge huyo alisema kuwa barua hiy leo itapelekwa kwa Waziri wa Fedha na nakala yake kwa Sipka wa Bunge, wakiwataka fedha zao za vikao vya bunge zipelekwe kwenye kifungu74 ambalo ni fungu la miradi ya maendeleo kwa Mkoa wa Kigoma.
"Uamuzi huu pia tumeamua kuufanya kwa kuwa moja ya sehemu kubwa ya mapato hutumika kushibisha mfumo mkubwa na udhaifu wa kiutawala pamoja na ufisadi, hata ukiangalia katika serikali kuna vyeo vingi kwa mfano hiki cha ukuu wa wilaya kina kazi gani, watu wanakula fedha na kazi hawafanyi huu ni mlundikano wa madaraka kwa watu ambao hawana hata kazi," alisema.
Alisema kuwa wao kama chama cha upinzani wataendelea kusisitiza mabadiliko ya mfumo wa utawala katika eneo moja tu la kuondoa wakuu wa wilaya na makatibu tarafa nchini na kubaki na uongozi wa halamshauri ambao unatosha kusimamia majukumu yote ya ndani ya wilaya na kuokoa fedha ambazo zinatosha kununulia mitambo mipya yenye uwezo wa kuzalisha umeme zaidi ya megawati 200.
INAONYESHA WATU KUTAFUTA UMAARUFU WA BILA SABABU,LEO KAONA WENZAKE WAMEINGIA WAPYA BUNGENI ANAWALETEA GOZIGOZI SIKU ZOTE ALIKUWA WAPI? HIYO KAMA NI HAKI YAKE YEYE BINAFSI NI WAJIBU WAKE AIPELEKE KTK JIMBO LAKE KIGOMA SIO BUNGE,NA AKIONA HANA MUDA HUO NI NAMNA YA KUIELEKEZA BENKI YAKE KUWA PESA HIZO ZIKIINGIA TUU WAZIHAMISHIE KDI HAKUNA SABABU YA KULETA MJADALA USIO NA TIJA AU KAMA ANAONA HAZIHITAJI BASI ATOE SADAKA.NA SERIKALI INGEFUTA VITI MAALUMU NI UNYONYAJI PESA ZINAPOTEA BURE KAMA NIA NI KUWAPA WINGI WANAWAKE BASI KTK MAJIMBO KUWE NA MKAKATI WA KILA CHAMA KUSIMAMISHA WAGOMBEA NUSU KWA NUSU NA WANAWAKE IONDOLEWE KABISA HII VITI MAALUMU
ReplyDeletekazi kwelikweli, hapa ndio tutfahamu ni nani mwakilishi thabiti wa wananchi?
ReplyDeleteIssue iwe kufuta posho zote,hazina tija watanzania badilikeni,kimaadili,kimsimamo,kiakili,kimtazamo,ccm mnalo mlizoea kuzichanga mpaka wakati wa kampeni mnanunulia kura.SASA ITAKUAJE
ReplyDeleteuzalendo utawashinda.watu walikuwa wanagombea ubunge ili wangake posho za vikao;anajua akimaliza posho zote vikao vya mwaka mzima,anaongeza vitega uchumi vyake.sasa posho zifutwe,nani atagomebea tena ubunge,na mashangingi yakitolewa tena basi,watapatikana wabunge ambao hawana tamaa ya mali,mabepari yote yatatoweka katika ubunge.na ndiyo mwisho wa ufisadi nchi hii.watu wanaloga ubunge kwa ajili ya posho,magari makubwa, na pensheni baada ya ubunge na si vinginevyo,ndo maana wengine wakifika vikaoni wanalala usingizi alimradi mwisho wa siku kitu kiingie mfukoni.wapinzani komaeni,hao ccm wanatamaa sana,wezi na ufisadi juu.
ReplyDeletehapo nimekupata mkuu
ReplyDeleteHapa naona hawa wanatunchanganya kabisa,sasa je kweli jambo hili ingeanza mapema mbona tungefaidika huku chini? ila hizi ni siasa tuwe makini!
ReplyDeleteswala si kuanza mapema , kila jambo lina wakati wake. Dr Slaa wakati fulani alilisema jambo hili, du walimkomalia kwelikwweli na kumwambia eti ametoa siri ya bunge, sasa yale yale yanarudi tena, huu ni wakati wa Mungu kutukumbuka TZ, Mungu hataleta malaika anatumia watu , hivyo ni kuwaunga mkono , mwisho wa siku kitaeleweka.
ReplyDeleteUkombozi hauji mpaka mapambano. Huu ni mfano wa mapambano. Kati ya wenye uchu wa fedha na wale wenye uchu na maendeleo ya nchi yao. Ila ukweli utajionyesha. Ni vizuri harakati hizi zikaungwa mkono na vyama vyote vya upinzani. Walioingia ubunge ili wachume watajulikana. Maana wao watanganania posho kana kwamba mshahara wa milioni saba kwa mwezi hautoshi!
ReplyDeleteHivi harakati kama hizi si zitaokoa matumizi mabaya ya fedha? Na mapato yakielekezwa kwa vipaumbele kama umeme, elimu, mawasiliano mbona unafuu utakuwepo hata kama utachukua muda mrefu! Tatizo la nchi yetu si hela, ni vipaumbele! Hela inakusanywa lakini inaliwa na wajanja kwa sababu njia za ulaji zilishaandaliwa na system.
nchi itajengwa na wenye njaa na itawiliwa na wachache wajanja.sasa mshahara wa ml.7; bado posho, na vikao vya bodi mbalmbal,magari ya kifahari,haviwatoshi jama,bado posho za ajabu,mtuhurumie tupate japo panadol hospital za bure,mama zetu wajifungue kwa huduma ya bure; waalimu wapate japo nauli za likizo elimu ipande.waalimu wakipata ajira mpya japo walipwe fedha za kujikimu wazingira hatarish wanayokwenda kuyakabil.wabunge haya yote wamefumba macho,wanataka kukinga tu.uchungu hawana,hata wale wabunge wamama,wajitolee wenzao wajifungue ktk mazingira mazuri,naona wamekaa kimya tu,kwa kweli fedha,fedheha.nataka nimsikie japo mama kilango kwa hili.wabunge mkubali nyakati za mabadiliko ni hizi.slaa udumu!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteNaona wabunge hawa wa Chadema na NCCR-Mageuzi wameisaidi serikali katika kupata chanzo cha mapato.Ni kitu cha kushangazi kwa Spika na Waziri wa fedha kuwalazimisha posho wabunge wetu ambao wameonyesha uzalendo.Ni matumaini yetu kuwa fedha zinahitajika sehemu nyingi.Mfano shule zetu za sekondari hazina vifaa vya maabara,nk .Hivi kweli mtu anakuletea fedha ya maendeleo wewe unakataa kwa sababu za kiitikadi ! Hapa tunaona Wabunge walio kimasilahi na Kikazi .Hongera Chadema na NCCR - Mageuzi kwa hili.
ReplyDeleteNaomba watanzania wote tuunge mkono hoja ya kutoa hizi posho. Inashangaza sana kwa mba watu wanalipwa posho huku wakifanya kazi ambayo wanalipwa. Kwa undani mshahara upangwa kulingana na masaa na siku unazokuwa kazini. mara nyingi tunatumia masaa 8, siku thesalasini. Kazi inayofanywa ndani ya muda huu inapashwa isilipwe, labda mfanyakazi akifanya zaidi ya masaa anayopaswa kuwa kazini. Nchi masikini kama yetu, inaumizwa sana na hizi posho, ukilinganisa kwamba mfumo wa utawala ni kubwa na ina wafanyakazi wengi sana kupita mahitaji yenyewe
ReplyDeleteHONGERA CHADEMA NA NCCR-MAGEUZI. KWA PAMOJA MTASHINDA,
ReplyDeleteWabunge wa ccm wamezidi tamaa ya fedha na ndio maana hawaungi mkono hoja zenye tija za wapinzani. Wengi wameingia bungeni kujineemesha na sio kutetea maslahi ya nchi.Serikali ya CCM badilikeni. Kumbukeni uvumilivu hufikia mwisho Angalieni Waarabu walivyoamka. Wamevumilia tawala za kidhalimu kwa miaka mingi na yanayotokea hawakuyategemea.
ReplyDeletesiku chama cha matapeli kimeondoka madarakani basi bongo itakuwa nchi ya kiukweli.si ipendi kama mavi ya mtu mwingine
ReplyDeleteHizo posho zitumieni kuongeza mishahara ya wakaguzi wakuu wa shule wa kanda. Hawa viongozi wanaongoza kanda ambazo zina wilaya kati ya 8 na 16, shule kati ya 300 na 500, wafanyakazi walio chini yao zaidi ya 100,
ReplyDeleteKatika eneo la Mkaguzi Mkuu mmoja wa Kanda kuna wabunge wasiopungua 15 hawana hata nyumba ya kuishi, wanapanga mitaani huku watu kama MA DEO na MA REO wakitesa kwenye nyumba za serikali na mishahara mizuri. Isitoshe hawa ni subordinates wa Wakaguzi wakuu wa shule lakini wanapata mishahara mikubwa kuliko wao.
Nchi hii ina laana. Mtu anayeongoza mikoa miwili na hata mikoa mitatu anapewa mshahara sawa na mwalimu? Hebu acheni dharau !
Haya kina Zitto wamesharudisha hizo posho, wapewe wakaguzi wa shule ili wasimamie vizuri ubora wa elimu. Tena wajengewe nyumba nzuri zenye hadhi ili waache kupanga uswahilini.
Ni aibu Mkaguzi Mkuu wa Shule kuzidiwa kiwango cha mshahara na mtu ambaye anamkagua ! Ujasiri wa kazi utatoka wapi?
Mkulo changamkia hizo fedha uongeze mishahara ya wakaguzi. Hizo fedha haziwezi kuelekezwa Kigoma kwani ni kodi ya watz.
yani wapunguze hiyo posho hii ni zarau kwa walimu ambayo ni mshahara
ReplyDeleteMbona ni uelewa tu kama mbuge anataka posho ikafanye kazi ya maendeleo ni jambo jema saana,cha muhimu spika awatake wabunge wengine wafanye hivyo.Hapa sio suala la umaarufu bali ni uzalendo huu anapaswa kuigwa.MZEE MAPUNDA
ReplyDeletehizo posho zielekezwe katika sekta ya afya,japo vijijini wapate panado ya bure, wazazi wazae salama, elimu iboreshwe kuanzia kwa waalimu, elimu iboreshwe kwanza, achana na umeme.umeme utakuwepo baada ya elimu,walimu wakiangaliwa vizuri, na laboratory zitajengwa hao waalimu watafundisha, lakini kwa mpango huu wa kutanua dodoma kwa mabilioni, hakuna elimu,waalimu hawataenda kazin,mtakaa mnajadil dodoma majibu hakuna, kwa nini wanaona uchungu kuwakumbuka waalimu.wajilipe tu na sisi waalimu tunasepa zetu,mgomo wetu na baridi na mbaya kuliko maelezo,mwakani wanafeli zaidi hadi kieleweke.nyie pateni,siye tukose.
ReplyDelete