LONDON, England
NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard ameelezea malengo ya timu hiyo msimu ujao akisema ni lazima wafuzu michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.Mchezaji huyo
alisema juzi kuwa uwezekano huo upo baada ya kurejea kocha, Kenny Dalglish na matumizi makubwa yatakayofanyika wakati wa usajili wa msimu huu.
Hata hivyo mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 30 anaamini kuwa kurejea katika michuano hiyo ya UEFA, kunahitaji malengo ya awali.
"Hakuna kitu kingine ambacho ningekipenda kama kuwaongoza vijana hawa msimu ujao kutwaa ubingwa, lakini siwezi kuweka matumaini zaidi kwa kusema kuwa kitu hiki kitatokea," alisema Gerrard kupitia tovuti ya klabu hiyo.
"Nitakuwa mpumbavu kuweka matumaini makubwa wakati hakuna kitu ambacho kimeshajitokeza. Kila mwanzo wa msimu matumaini ya Liverpool huwa yanakuwa makubwa, lakini kwa kuwa Kenny amerejea na usajili mdogo alioufanya nina uhakika tutakuwa juu," aliongeza.
Alisema kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ndiyo itakuwa lengo lao kubwa na akasema anadhani kila klabu inatamaini kufanya hivyo, kutokana na kuwa fedha zinazopatikana katika michuano hiyo ndizo zinazoleta ushindani mkubwa, lakini akasema pia ushindani huo unasababishwa na kuwa michuano hiyo ni mikubwa kwa kila mchezaji.
"Kila mmoja anapenda kuhusishwa katika michuano hiyo, tumekuwa na usiku wa raha kwa miaka kadhaa Anfield katika mashindano hayo, sote tungependa kuona usiku huo unarejea tena," alisema Gerrard.
kweli kaka,mcmu ujao ni wetu tuuuu,viva liverpool the only best european club from England
ReplyDelete