LONDON, England
MWANAMKE ambaye anadaiwa kuwa mke wa nje wa mchezaji Wayne Rooney, Jenny Thompson amekimbizwa hospitali akiwa mahututi kwa kile kinachodaiwa
ni kuwa amezidisha kiwango cha dawa aina ya Valium.
Taarifa zilieleza jana kuwa Jenny (22), alikuwa katika hali mbaya wakati wafanyakazi wa kikosi cha dharura walipowasili nyumbani kwake mjini Bolton juzi saa 12:30 jioni.
Mwanadada huyo ambaye anadai kukinga kitita cha pauni 1,200 kwa siku ambazo alikuwa akilala na nyota huyo wa Manchester United, anadaiwa kubwia chupa nzima ya dawa hizo na kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya Royal Bolton, ambako aliutumia usiku mzima wa kuamkia jana akiwa hoi.
Vyanzo vya habari vilieleza: "Asubuhi alikuwa akinywa kwenye baa na baadaye hakuna aliyefahamu mahali alipo na hakupokea simu yoyote."
"Marafiki zake walipigwa na butwaa baada ya mmoja wao kwenda nyumbani kwake na kufungua mlango, kisha akamkuta akiwa amelala sakafuni. Alikuwa akionekana kama mtu ambaye alikuwa amekunywa chupa nzima ya dawa za kupunguza maumivu," viliongeza vyanzo hivyo vya habari.
No comments:
Post a Comment