Na Anneth Kagenda
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, kimesema wamepata madhara makubwa kutokana na baadhi yao kuropoka na kutoa siri za chama hicho
hadharani kuliko vyama vya upinzani.
Kimesema vyama vya upinzani vimekuwa na siri, na havipendi kusema mambo yao hadharani kama wanavyofanya wana CCM.
Hayo yalisemwa juzi na na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. John Guninita, wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Tawi la Mwembe Simba katika Kata ya Charambe na Mianzini Manispaa ya Temeke.
Alisema umefika wakati wanachama wa CCM kufuata katiba ya chama chao ikiwa ni pamoja na kuelekezana ndani ya vikao badala ya kuzungumza masuala ya ndani barabarani, jambo linaloweza kusababisha kubomoka kwa chama hicho.
"Sisi ndio tuna matatizo ambayo yanaweza kusababisha kubomoka kwa chama chetu, ni nani amewasikia wapinzani wakiropoka barabarani?
Lakini sisi tunashindwa kuelezana kwenye vikao badala yake tunaropoka! Acheni kufanya hivyo tumieni vikao kuelezana kila mtu alipokosea," alisema Bw. Guninita.
Aliwataka wanachama hao kuacha tabia ya rushwa na kusema kuwa hivi sasa wamejipanga vyema kuhakikisha wanakosoa tabia hiyo ndani ya CCM.
Alisema chama hicho hakitasubiri mtu akamatwe na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) badala yake atakayeonekana anafanya hivyo atachukuliwa hatua kali.
"Rushwa iko mara mbili, kwenye serikali pamoja na kwenye chama, lakini hasa ni serikali na Taasisi zake kuanzia kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa hadi juu.
Miradi inakuja ya mfano ya sh. milioni tano, lakini mtu anaandika milioni 15/-, mambo haya hatutayavumilia hata kidogo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa, tuna katiba inayotuongoza," alisema.
Alisema katika uchaguzi wa mwaka kesho wa chama hicho kila mtu atachaguliwa kwa sifa yake na si kwa kutoa rushwa na kusisitiza kuwa kigezo kikubwa kitakuwa ni uwezo wa mtu na uaminifu.
Kwa kweli manaropoka,nimemuona Mbunge wa Nkenge Asumpta ,kwa kweli kazi kweli kweli.Anaropoka 2 bungeni,akianza kuongea watu wanazima simu.
ReplyDeleteCCM kweli mwenyekiti umesema kweli.Hakuna anayeichukia.Bali Tabia na Matendo ya baadhi yenu ndiyo inaudhi watu.Kutamba tamba hadharani, kubeza mnayoambiwa na wadau wengine,kujiona kuwa mpo siku zote na mtaendelea kuwepo ndio kinachowafanya mchukiwe.kwa mfano issue ya kujivua Gamba.Mmesema weee! sasa watu wanasubiri waone.Kama mngeitana mkavua hayo magamba yenu kwenye vikao watu wangeshangaa na yanayotokea na heshima inakuwepo.Lakini kuzunguka nchi yote mkijinadi kuwa mtawaadabisha wanaotuhumiwa,mtajikuta mwisho wa siku watu wanayazoea hayo mazungumzo!Hongera mwenyekiti kwa kugundua!
ReplyDeleteNdugu Guninita wewe kweli ni mzalendo. Sikutegemea kiongozi wa CCM kutamka ukweli kama huo naona kama ni ndoto tu. Ninamshauri Nape Nnauye naye alione hili jamani kwani kwa uropokaji yeye ni namba moja. Chama chetu tunakipenda ila viongozi wake wanakisababisha chama kichukiwe kutokana na kauli zao. Wapinzani ni waungwana sana mambo yao wanajadili kimya kimya. Ameondoka Yusufu Makamba msema hovyo yule lakini tumepewa Nape Nnauye mmakonde msema hovyo kuliko wote waliopita. Tena huyu Nape anatumia majukwaa kulipiza kisasi kwa kina Mh. Lowassa. CCM sio mahali pa watu kutendeana maovu jamani. Acheni chama chetu kama kilivyo kuropoka ropoka hovyo kunazidi kuleta mpasuko kwenye chama.
ReplyDeleteTatizo ambalo lipo CCM ni unafiki na maswala ya kuburuzana. Sasa hayo yamekwenda mpaka yamefika mahali watu wameyachoka kutokana na kwamba, mengi ya maamuzi hayatokani na sera zinazotangazwa kwa wananchi, ila ndani kwa ndani ni sera za kuchakachua maamuzi yaliyowafikia wananchi. Sasa kwa wale wenye hofu ya Mungu, japo wanashangilia kama wamekubali, lakini wanajisikia kudaiwa mioyoni, na ndiyo unasikia mtu anayatoa kupunguza msongo wa mawazo. Dawa ni CCM kubadilika na kuingia zaidi katika sera za kuokoa Taifa hili lisiangamie. Kujivua gamba au kulivaa sisi hakutusaidii. Kushindana na Upinzani kama mko vijiweni hakuna tija kwetu! Tunachotaka ni kuuinua uchumi wa Taifa hili, ili uendane na kiwango cha maliasili iliyopo, ili maisha ya watu wa taifa hili yapate kuboreka! Siasa hazijengi, wala kuongea sana hakutuondolei njaa inayotishia kuenea nchini, wala janga la umeme. Jipangeni zaidi kwa kusudi na dhamana mliyopewa ya kulikomboa taifa na huu umasikini usio na uhalali wowote kwa TZ.
ReplyDeleteIyo sisiemu ingekuwa na maguninita wengi na ikaweza kuyaondoa mafisadi na mijiongozi mijiizi na mila rushwa na miongo na mizembe na mipenda posho.... ingeweza ikabakia na mnuko lakini ikatakata kidogo. Ze sisiem stinks
ReplyDeleteJohn Guninita Amewahi kuwa CDM na anafahamu kilicho mtoa kule ila CCM Mtulizane Na muwambie hao wabunge wenu waache kuzomea, wananchi tunaona maana tutawauliza kazi walizo fanya wakiwa bungeni.
ReplyDeleteGuninita unazidi kuonyesha jinsi ulivyoiva kisiasa. Umesema maneno ya kweli kabisa. Sisi wanachama wa CCM tunasononeka sana tunaopoona viongozi wetu wakiropoka kana kwamba wamebuya unga! Tabia hii chafu ilijengeka miongoni mwa viongozi wetu kupitia Katibu Mkuu aliyepita, maana hizo ndizo zilikuwa zake.
ReplyDeleteNimekuwa nikilifuatilia sana Bunge letu, kwa kweli wabunge wa chama changu wanayoyafanya yanasikitisha sana. Ataamka mtu kwa kufuata mkumbo tu atasema mimi naunga hoja kwa asilimia 100. Akishasema vivyo tena anaanza kutoridhika na baadhi ya maeneo anayochangia! Hivi kitu kuwa safi kwa asilimia mia 100 makosa yatatoka wapi. Hii yote sababu ya kuropoka.
Mwingine atasimama na kuanza kujigamba kuwa ooo mimi nimetembea sana, nina umaarufu lakini sijapata hiki wala kile kama Babu wa Samunge! Ooo mimi ndiye niliyeanza mbona sisifiwi, yote hayo ni uropokaji tu na wivu usiokuwa na maana. Jaribuni kuona wenzenu wa upande wa pili wanavyo jenga hoja. Msitufanye tuamini kuwa mbunge 1 wa kutoka upinzania ni sawa na wabunge 20 kutoka kwenye chama chetu.
Mujigaru Chitanda