15 June 2011

Dovutwa arukia mikopo, matibabu ya wabunge

Na Rabia Bakari

CHAMA cha UPDP kimewabeza baadhi ya wabunge wanaokataa posho za vikao bungeni kwa madai ya kutetea maslahi ya umma na kuwataka warudishe
kwanza sh. milioni 90 walizokopeshwa wakati wakiingia bungeni baada ya uchaguzi mkuu.

Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bw. Fahmi Dovutwa, alisema kitendo cha wabunge kukubali kupokea sh. milioni 90 (za mkopo wa gari) kabla ya kufanya kazi kama walivyofanya baada ya kuapishwa ni ubadhilifu wa mali za umma pia.

"Wasitetee maslahi ya wananchi katika eneo moja tu, bali wanatakiwa kuanza kujisafisha kwanza kwa kila kitu ikiwemo kurudisha sh. milioni 90 walizopokea, wajiondoe pia katika bima ya afya ya mamilioni ya fedha za umma wanayotibiwa katika hospitali za gharama ili nao watibiwe katika hospitali za serikali kama wananchi wa kawaida.

"Kuwa na bima ya afya kama ya wabunge maana yake ni kupata matibabu katika hospitali binafsi zenye ubora wa hali ya juu huku hospitali za umma zikiwa hazina hata dawa, warudi chini kwa kila kitu na si kutudanganya kwa kukataa posho, kitendo ambacho wanajua fika hakiwezi kufanyika," alisema.

Kiongozi huyo wa UPDP aliwashauri wabunge kujisafisha kwanza kabla ya kuzungumzia uadilifu na kuwataka kama kweli ni wasafi kukataa posho basi wakatae na 'huduma za upendeleo wanazopata' na kwenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hoja hiyo iliwasilishwa bungeni kwa maslahi ya kisiasa na si kwa wanannchi.

"Niliwahi kuwataka wabunge wa upinzani wanaopiga kelele bungeni kuhusu maslahi ya umma waanze kukataa posho na kurudisha fedha ambazo wamepewa kwa upendeleo, wana mishahara lakini wameng'ang'ania kwenye posho tu, kukataa posho peke yake si uadilifu, bali watuoneshe na zile milioni 90 walizopewa.

"Kukaa kimya bila kutoa ufafanuzi wa fedha nyingine walizopewa tena kabla hata hawajaanza kufanya kazi kwa wananchi, ni unafiki mkubwa ambao hatutaweza kuuvumilia," aliongeza Bw. Dovutwa bila kugusia kama fedha hizo zinarejeshwa kama mkopo au la.

Aliwataka kuondoa kiini macho cha kusimamia maslahi ya wananchi katika eneo moja ambalo ni dogo bali waguse kila sekta kwa ufafanuzi ambao utaeleweka na jamii.

Hivi karibuni baadhi ya wabunge wa CHADEMA wamependekeza serikali kuzuia ulipaji wa posho za vikao kwa watumishi wa umma wakiwamo wabunge, suala ambalo litawezesha kuokoa zaidi ya sh. bilioni 900.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Zito Kabwe, akiungwa mkono na wabunge wa NCCR-Mageuzi, amekwenda mbali zaidi kwa kumwandikia Spika Anne Makinda, akimtaka aelekeze fedha hizo katika Taasisi ya Maendeleo ya Mkoa wake ili zisaidie kuboresha huduma za jamii.

Hata hivyo, Spika Makinda amesisitiza kuwa fedha hizo zitaendelea kulipwa kwenye akaunti za wabunge hao, na pale waliposema hawatasaini karatasi za mahudhuria zinazotumika kama kigezo cha kulipa posho hizo, alijibu kuwa wasipofanya hivyo kwa mikutano mitatu watafukuzwa kwa kukiuka kanuni za bunge.

Tayari Bw. Zitto ameweka wazi kuwa yuko tayari kutimuliwa ubunge iwapo atalazimishwa kupokea fedha hizo kwa kuwa ni sawa na kuwapunja wananchi hkia yao.

5 comments:

  1. Gazeti ,mnapoteza nafasi ya maana kumzungumzia mtu ambaye ni unpopular,kwa kweli huyu Tovutwa hafai kuandikwa kwenye magazeti anamaliza nafasi tu,ni kibaraka wa CCM na twasikia anatafuta UDC kwa nguvu zote,simpendi huyu mtu,ninaposikia jina lake uwa nachefuka

    ReplyDelete
  2. huyu dovutwa ni choko mbwa koko tu....kwangu mimi dovutwa maana yake ni mtu wa ajabu ajabu....

    ReplyDelete
  3. Jamani Muelimisheni huyu Dovutwa. Kwanza anatakiwa apigwe mawe kwani alichezea gharama za kuweka jina lake kwenye karatasi za kura halafu akajitoa. Hajui kuwa alichezea kodi zetu? Hajui hata kutofautisha "MKOPO" na "POSHO" Shame upon Dovutwa Fahmi. Asipewe hata kazi ya kufundisha Mgambo.

    ReplyDelete
  4. Wewe DO VUTWA nani asiye kujua ni Kibaraka wa CCM Maana

    ReplyDelete
  5. hao tunawaita manungayembe ya kisiasa. hayauziki. hakuna haja ya kuyaeka kwenye gazeti. eti Dovutwa! Nyooooo

    ReplyDelete