Na Mwandishi Maalumu
Rais Jakaya Kikwete ni miongoni mwa viongozi saba duniani ambao watakuwa wageni maalumu kwenye Mkutano wa 100 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) ulioanza
Juni Mosi mwaka huu mjini Geneva, Uswisi.
Rais Kikwete ambaye aliondoka nchini jana kwa ziara ya siku tatu, amepangiwa kuhutubia mkutano huo mchana wa leo, akiwa mgeni wa mwisho kuhutubia mkutano huo unaomalizika keshokutwa.
Viongozi wengine walioalikwa kuhutubia mkutano huo ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Susilo Yudhoyono na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.
Viongozi wengine watakaohutubia mkutano huo unaojumuisha washiriki kutoka nchi zote 183 wanachama wa ILO ni Waziri Mkuu wa Russia, Vladimir Putin; Rais wa Jamhuri ya Uswisi, Micheline Calmy-Rey; Rais wa Finland, Tarja Halonen na Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Palestine, Salam Fayyad.
Mkutano huo wa 100 tangu kuanzishwa kwa ILO mwaka 1919, unaodhuhuriwa na watu 7,000 unashirikisha viongozi wa nchi na serikali wa zamani, mawaziri wa nchi mbalimbali, taasisi za kimataifa, na taasisi za kiraia.
Mada za jumla zinazozungumzwa katika mkutano huo ni pamoja na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira duniani, zahama ya kimataifa ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana, jinsi ya kuongeza kiwango cha kulinda watu zaidi duniani kupitia mifuko ya hifadhi za kijamii, na haki za wafanyakazi na watumishi kazini na hasa zile za watumishi wa ndani.
Mada mahsusi zitakazozunguzwa kwenye mkutano huo ni Ajira na Haki za Kijamii katika Dunia ya Utandawazi; Nafasi ya Ajira ya Heshima katika Utandawazi wa Haki Zaidi, Kijani Zaidi na Endelevu Zaidi; Mafunzo Kutokana na Zahama ya Karibuni Katika Kujenga Jamii Eendelevu na Zenye Kushirikiana; na Umuhimu wa Nyakati Mpya za Haki za Kijamii.
Katika barua yake ya mwaliko, Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Dkt. Juan Somavia alimpongeza Rais Kikwete kwa mpango mzuri wa ajira katika Tanzania ujulikanao kama Tanzania Decent Work Country Programme na pia akakumbusha uhusiano wake na shughuli za ILO na jitihada zake za kutafuta na kuboresha ajira duniani hasa kwa vijana.
“Ulitupa heshima wakati ulipohutubia Mkutano wa 11 wa Mwaka wa Afrika Aprili mwaka 2007. Tunakushuru kwa uamuzi wako huo. Pia tunakupongeza kwa kazi uliyoifanya ukiwa mjumbe wa Tume ya Afrika – Danish Africa Commission - kuhusu namna ya kutafuta na kuongeza ajira kwa vijana,” alisema Dkt. Juan Somavia.
Sokoine's cousin:
ReplyDeleteMrisho ukisharudi safari yako ya Switzerland (ILO summit), uwe serious na hizo ppf, lapf, nssf, pspf zako hapa petu bongo!! Sio unakuja kuchecheka nao wakurugenzi wake (i.e.ppf, lapf, nssf, pspf) kisa they are just close to u but be serious plz for the mutual benefit, make the ILO summit ur focus, huh Mrisho?
Hivi huyu mtu si mbovu jamani? na hizi safari nyingi nyingi si kaambiwa apunguze? juzi tu alikuwa SA, leo Uswisi, kesho sijui wapi Mungu anajua! Kwani si ampe makamu wake au waziri mkuu au rais wa znz kwani lazima yeye aende? Mbona Urusi anakwenda waziri mkuu na mawaziri wakuu wengine wengi tu watahudhuria huo mkutano! Punguza sifa mzee, utapunguza siku za uhai wako bure afya yenyewe mgogoro!
ReplyDeleteHuyu si ndio amegombana na TUCTA? Si ndio alitishia kuwafanya kitu mbaya wafanyakazi wakigoma? huyu si ndio ameacha mifuko ya hifadhi za jamii ikifisadiwa na mapatna? huyu si ndio ametoa mshahara mdogo wa kwa watumishi wa nyumbani? Huyu si ndio ameruhusu ufisadi unaopunguza ajira kwa vijana? Hawa ILO vipi? Si huu mkutano wawakilishi wa TUCTA watakuwapo? Watajisikiaje kuhutubiwa na mgomvi wao? Jamani watu waandamane pale Geneva nje ya ukumbi kupinga heshima hii feki! Hizi heshima za aina hii ndio zinmvimbisha kichwa mkwere! Hapo nyumbani nendeni pale ofisi za ILO (karibu na mawenzi hotel ya zamani) mueleze kisikitishwa kwenu na kietendo cha ILO kumtunuku mtu anayetenda kinyume na ILO standards. Hivi ndivyo wakereketwa kote duniani wanavyofikisha ujumbe. Fursa kama hizi msiache zikapotea bure! Hapa Geneva vyombo vya habari hawezi kuvikimbia kama wenyewe mkianzisha !
ReplyDeleteAcheni fitna nyie wachangiaji hapo juu. Kikwete amealikwa kuhutubia. Mchango wake unaonekana kimataifa. Hakuamua yeye mwenyewe kwenda Uswiss, ameitwa, kati ya wote wanaouzulia kikwete ni mmoja wa wachache watakaohutubia mkutano. Hakuomba ameombwa kufanya hivyo. Ni chadema tu wasioona mchango wa Kikwete katika dunia yetu. Someni makala vizuri kabla hamjachangia. Moja ya kazi za rais yeye ni jicho la nchi katika jumuiya ya kimataifa, kwa hiyo lazima asafiri. Watanzania hawakuchagua makamu wa rais au waziri mkuu kuwa rais. Kwanini atume makamu wa rais wakati yeye yupo? Wanachadema komaeni. Hata mgombea urais wenu akichaguliwa atafanya vile vile, ni moja ya majukumu ya rais kutembelea jumuiya za kimataifa. Nyie mnaangalia gharama za rais anaposafiri, lakini hamuangalii hizi safari zinaliletea nini taifa.
ReplyDelete