13 June 2011

DC arushiwa zigo mauaji Serengeti

Na Benjamin Masese

WANANCHI wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamemlalamikia Mkuu wa wilaya hiyo, Luteni Kanali Edward Ole Lenga kwamba amechangia kuchochea mauaji ya
kikatili kati ya Wakurya na Wangoreme yalitokea kijiji cha Mosongo na kusababisha watu sita kuuawa akiwemo mwanafunzi wa Sekondari ya Maria Nyerere na viongozi wa kijiji.

Vile vile walisema kuwa watu 835 kutoka kaya 150 wamekimbia makazi yao tangu kutokea mauaji hayo Machi 6, 2009 na kuweka makazi yao katika kijiji hicho bila ridhaa ya wazawa huku wakikingiwa kifua na Bw. Ole Lenga kutokana na kuozwa mke wa Kikurya.

Madai hayo yalitolewa katika mkutano wa viongozi wanne kutoka kijiji cha Mosongo uliofanyika Dar es Salaam juzi ukiongozwa na Bw. Wilson Nyamchabha na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi walio uhamishoni.

Bw. Nyamchabha alisema kuwa katika mauaji hayo watu wengine walijeruhiwa kwa kutobolewa macho, kung'olewa meno na kukatwa mikono na mguu pamoja na uporaji wa mali na mifugo na kusababisha wanafunzi zaidi ya 163 waliokuwa wakisoma katika shule mbalimbali za msingi na sekondari kuacha masomo yao  na kuwafuata wazazi wao uhamishoni.

Alisema tangu kutokea kwa mauaji hayo, Mkuu wa Wilaya na viongizi wengine husika wa wilaya hiyo wamekuwa kimya licha ya kufahamu taarifa zote.

Waliouawa katika mapigano hayo wametajwa kuwa ni Mwikwabe Wambura, Bw. Genturu Maro, Thomas John aliyekuwa mwanafunzi wa sekondari ya Maria Nyerere, Bw. Noel Mathayo aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mosongo, Bw. Munsi Mahimbo na Bw. Jacob Wambura.

"Mkuu wa wilaya Ole Lenga amechangia sana watu kupoteza maisha yao kwani yeye ameonekana waziwazi kuwa mtetezi na wakala wa wahamiaji haramu huku akitukandamiza na kutuweka rumande bila ya mashtaka na kutoruhusu dhamana kwa sababu ameozwa mke na ukoo huo, pia amepewa hongo kwa kuchangiwa ng'ombe na pesa.

Akijibu tuhuma hizo kwa njia ya simu, DC Ole Lenga alisema kuwa tuhuma zinazoelekezwa kwake zinamuongezea uchungu na mawazo ya kufiwa na wake zake wawili mfululizo na kusababisha kuishi bila mwanamke hadi sasa.

Alikiri kuwepo mauaji hayo yalitokea Machi 6,2009 huku akikanusha vikali tuhuma dhidi yake, za kuozwa mke wa Kikurya na kusema wanamkumbusha machungu kwani hivi sasa anaishi bila mwanamke.

Kanali alisema kuwa kitendo cha kumsingizia ameozwa na ukoo huo na kupewa hongo ya ng'ombe na pesa ili kuwalinda Wakurya ni uzushi na haipaswi kurudiwa kutamkwa tena, na atawachukulia hatua kali wanaosema hivyo ili walete udhibitisho.

"Nimechukizwa kweli, ndio maana sitaki marafiki hapa Mkoa wa Mara, mimi hapa nimeongoza miaka mitatu lakini sina kundi la rafiki kwa sababu najua historia ya watu wa Mara," aliasema.

2 comments:

  1. Huyu DC ni mjinga hana maana kwani yeye anaongoza wananchi wa wapi? kwanza huyu ni miongoni mwa Ma-DC wa Lowasa na kikwete wanaoteuliwa kwa ushoga, na watanzania wenzangu mnaweza mkaona hata aina ya majibu anayotoa, hana sifa hata za kuwa balozi wa kijiji lakini ati ni DC kwa sababu Lowasa alimwombea kwa Kikwete! Hii nchi inapotea kwa kuwa na viongozi wa hovyo kama huyu DC na Rais wake aliye mteua na hata kusoma hakusoma anaweza au kuchunga ng'ombe tu wala siyo watu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maana we unajua kuongoza eeeh, au ni fitina tyu unajua hata maisha yake mpuuz ww usiekua na adabu ,jiangalie we elimu yako ndo imeishia hapo mpuuz mmoja

      Delete