Na Grace Michael, Dodoma
WAKATI Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe akisema amerejesha gari kwa lengo la kupigwa mnada na fedha kuelekezwa katika miradi ya
maendeleo, Uongozi wa Bunge umesema bado haujapata taarifa yoyote ya kiofisi inayoonesha kurejeshwa kwa gari hilo.
Hatua hiyo ilijulikana jana mjini hapa wakati Kaimu Katibu wa Bunge, Bw. John Joel akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na madai ya Bw. Mbowe.
“Mpaka sasa hatuna taarifa zozote za maandishi za kurejeshwa kwa gari hilo na kama taarifa hiyo itakuja tuko tayari kusikiliza maamuzi yao...Bunge lina utaratibu wa kutoa magari, nyumba na walinzi kwa viongozi bungeni kulingana na hadhi yao, hivyo kama watarejesha tuko tayari kwa kuwa sisi ni watendaji zaidi na
si wanasiasa,” alisema Bw. Joel na kuongeza kuwa Bw. Mbowe pia amepewa nyumba Dodoma na Dar es Salaam kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani.
Juzi Bw. Mbowe aliwaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, "...kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe, ameamua kurejesha gari yake aina ya “Shangingi” alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada. Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na taifa kwa ujumla".
Lengo la hatua hiyo, Bw. Mbowe alisema ni kutaka kuipunguzia serikali mzigo, kisha fedha hizo kuongezwa katika bajeti ya maendeleo ili kupunguza ukali wa maisha kwa Mtanzania wa kawaida kwa kuboresha miradi ya maendeleo yanayosuasua kwa sasa kwa maelezo kuwa 'sungura ni mdogo'.
Akizungumzia suala la Kambi Rasmi ya Upinzani kuandika barua kutaka kutenganisha fomu za mahudhurio na za kuchukua posho ili kutofautisha waliohudhuria na waliopokea posho, alisema kuwa fomu wanazojaza wabunge ni kwa ajili ya mahudhurio, ambayo lengo lake ni kujua endapo mbunge amehudhuria kikao cha bunge.
“Fedha zote zinaingizwa benki moja kwa moja, hivyo suala la kutenganisha fomu halina msingi,” alisema Bw. Joel, huku akisema mpaka sasa wabunge hao wanaendelea kupokea posho hizo kwa kuwa hawajawasilisha barua ya kukataa posho hizo.
Hata hivyo, Bw. Joel alisema kuwa, 'kama wanataka kukataa posho hizo waandike barua na kuweka saini zao ili ijulikane ni nani anakataa', kauli ambayo inatofautiana na aliyotoa Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda wakati akizungumzia suala la Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zitto Kabwe aliyeandika barua kuzuia posho zake na kuelekeza zipelekwe kwenye Taasisi Maendeleo Kigoma (KDI).
Katika majibu yake, Bi. Makinda alisema ulipaji wa posho ni kwa mujibu wa sheria na fedha hizo hupelekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya mbunge kwa kuangalia orodha ya mahudhurio.
Akizungumzia masuala hayo, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani, Bw. Tundu Lissu, alisema jana kuwa gari la Bw. Mbowe limekabidhiwa tangu juzi lakini alipohojiwa zaidi kueleza lilikabidhiwa wapi, aliwataka waandishi wa habari kumhoji Bw. Mbowe mwenyewe.
Kuhusiana na suala la posho, Bw. Lissu alisema kuwa wanatarajia kuwasilisha barua rasmi leo kwa lengo la kuzikataa.
Wakati huo huo kambi hiyo imewasilisha rasmi barua ya malalamiko kwenye Kamati ya Kanuni ya Kudumu ya Bunge kumshtaki Spika Makinda kwa kuendesha bunge kiupendeleo.
Bw. Lissu alisema kuwa barua hiyo wameikabidhi rasmi juzi kwa Katibu wa Bunge.
Malalamiko hayo yalitokana na kitendo cha Spika kumzuia Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kujibu swali lililokuwa limeulizwa likitaka ufafanuzi wa mauaji ya wananchi katika Mgodi wa Nort Mara yaliyofanyika hivi karibuni, akisema liko mahakamani.
Maoni kuhusu shangingi la Mbowe
Mwanazuoni wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Bw. Bashiru Ally mbali ya kupongeza uamuzi Bw. Mbowe, alisema hatua hiyo haipaswi kuishia hapo kwani mjadala ni mpana zaidi ya posho na mashangingi, anaripoti Tumaini Makene.
Alisema hoja hiyo ni matokeo ya taifa kukumbatia mfumo wa ubepari uchwara, ambao umezalisha viongozi wasiowajibika kujali maisha ya wananchi wao, na kuwa hiyo ni dalili za dhahama kubwa ya mgawanyo usiokuwa sawa wa rasilimali za taifa.
"Hoja za posho, magari ya anasa ni hoja nzito na zenye maana kwa jamii, na hicho alichokifanya ni sahihi lakini mimi nadhani tuko kwenye crisis...taifa liko kwenye dhahama kubwa, lakini mara nyingi tumekuwa tukitumia muda mwingi kujadili dalili za tatizo badala ya chanzo kilichozalisha matatizo tuliyonayo.
"Tuna tatizo kubwa la uzalishaji na mgawanyo wa rasilimali au mapato yetu, tumelea mfumo wa ajabu sana ambao umesababisha ufa mkubwa sana kati ya mfumo wa uzalishaji na mfumo wa ugawanyaji rasilimali zetu. Hii ni kwa sababu tumekumbatia ubepari uchwara.
"Mfumo ambao umezalisha viongozi wasiojali akina mama wanaokufa wakijifungua, mfumo ambao umezalisha wanasiasa na viongozi limbukeni, ngoja nikupatie mfano. Makamu Mkuu wa chuo cha SAUT (Mtakatifu Augustine, Mwanza) nimekutana naye akiendesha gari mwenyewe gari lake la kawaida tu, lakini makamu wakuu wa vyuo vyetu vya umma wana magari yao ya kazini aina ya mashangingi na gari ya nyumbani, wanatumia magari ya anasa wakati vyuo vyetu hivi hivi havina chaki, wala ofisi, ninavyokwambia hapa mimi nina muda mrefu sina ofisi maalumu ya kueleweka."
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, alisema kuwa uamuzi wa Bw. Mbowe ni wa kupongezwa, akisema wakati sasa umewadia kwa suala la matumizi makubwa ya serikali kuwa moja ya chanzo cha hamasa ya mabadiliko nchini.
Alisema katika kuzunguka kwake duniani, amewahi kwenda Uingereza na Marekani ambako alikuta watumishi wa umma, wakiwemo wanasiasa, wakitumia usafiri wa kawaida, huku wakiwaheshimu wananchi wao, kwani wanajua wakifanya matumizi ya anasa 'watalipuka' kuhoji wametoa wapi mamlaka hayo ya 'kutanua' kwa kutumia rasilimali za nchi.
"Nmekwenda mimi 10 Down Streets pale Uingereza, wanatumia magari wanayotengeneza wenyewe, vifuu vile...Austin, ambavyo hata parking ni economical pia, nikamuuliza mmoja wa waandishi wa habari pale kwa nini wanatumia haya, akasema wanajua siku wakinunua mashangingi kutakuwa na upingaji mkubwa nchi nzima.
Mchungaji Mtikila alisema kuwa mabilioni ya fedha hayo yakayookolewa kwa kuminya matumizi makubwa ya watumishi wa umma, yapelekwe kwenye miradi ya maendeleo au katika kusaidia huduma za jamii kama vile kukopesha dawa hospitalini ili 'Watanzania waweze kuahirisha vifo vinavyoepukika na kuongeza siku za kuishi."
Haina mantiki yoyote, kurudisha au kutorudisha ni kijikosha tu, Mbona amelitumia kwanza? Hapo anataka kuituhadaa wananchi wakati yeye ni mkwepa kodi mkubwa, tangu wakati huo mpaka leo, amekimbilia siasa ameacha biashara ili kuipindisha sheria kwa mgongo wa Siasa. anataka kupata huruma ya kisiasa kupitia Jambo kama hilo, tusidanganyike watanzania hao Chadema wanayo agenda yao ya Siri, nia ni kutaka kuvuruga Amani na Utulivu wetu. Ni Bora Kufa Masikini kuliko kuichezea Amani yetu na Utulivu wetu.Mtikila alikwisha kisiasa siku nyingi amebaki kutapeli waumini wake.Hatudanganyiki na Propaganda zenu wajinga wakubwa Mbowe na Wenzako wote.
ReplyDeleteHivi hili swala la kukwepa kodi mbona linarudiwa sana? kwani anayekwepa kodi ni Mbowe Tu. na hawa wahindi? hapa tusidanganyane, ukweli unabaki palepale, wafanyabiashara kukwepa kodi ni uzembe wa Kikwete na serikali yake na si tatizo la mbowe.
ReplyDeleteKama watu wameachwa wakifanya biashara kihuni hilo tatizo la serikali si tatizo la upinzani. Na sisitiza TATIZO LA KUKWEPA KODI SI LA MBOWE NI UBOVU WA SERIKALI YA YETU.
Swala la kurudisha gari mimi pia siungi mkono, ila nadhani upinzani unatakiwa kukaza buti kuhakikisha sheria zinazoruhusu magari ya kifahali zinabadilishwa na siyo kurudisha gari alilopewa kisheria.
swala la amani ya Tanzania mimi sikuungi mkono hata kidogo, hakuna amani Tanzania. watu hawafi kwa risasi ila kwa njaa, kukosa elimu na maradhi hiyo ni amani? Amani unayoitetea ni ya kwako wewe unayenufaika na ufisadi wa Tanzania. Kama kunaamani kwa nini misafara ya viaongozi inaulinzi mkali sana? kwa nini viongozi huvaa bullet proof? HAKUNA AMANI TANZANIA NA MAENDELEO HAYAPATIKANI KWA KUDANGANYANA KUWA ATI UKIDAI HAKI UNAVURUGA AMANI. HUU NI UPUUZI.
sisi wananchi tunachotaka ni kuona watu wanasimamia haki za watu, haijulishi kama huyu mtu anataka kujikosha au anataka kujimbeleza au anataka kujenga jina lake.
ReplyDeleteMimi nampongeza mbowe kwa kuamua karudisha gari hilo ambalo taifa ni kama mzigo.
mimi naona wabunge wengepewa ata bajaji na watumishi wengine wa selikari.
Naanza na mchangiaji wa kwanza, swala la amani ndani ya umasikini ni uongo na kutofikiria vizuri! Ktk umanisikini amani yaweza kuwepo in a short run but baadae mabo yatakwenda kombo. Kuna ukomo wa watu kuvumilia umasikini ambao wanajua si kwa uzembe wao bali sababu ya viongozi wao. Hivyo dawa ya amani ya kudumu ni kuendeleza nchi yetu na watu wake, namaanisha siyo maendeleo ya kwenye takwimu eti GDP iko vizuri kwenye karatasi ila watu wengi wao wanasota. Ukitaka ujue umasikini ni tishio kwa amani angalia wengi wa washiriki maandamano ya ufisadi au against polices' misconducts hapa Tanzania ni wale masikini na watu wa kawaida, hutamuona mwenye suit or so hata km ni mpinzani labda awe kiongozi. Na karibu nchi yote zilizoondolewa madarakani hivi karibuni kwa maandamano waandamanaji wengi ni wale watu wa kawaida wakiwa coordinated na viongozi wachache, matajiri na wenye nafuu ya maisha hata km ni mwanachama wa upinzani hawaendi barabarani maana hawana njaa. Kwahiyo nashawishika kusema kwamba serikali serikali isipuuze kilio cha masikini maana ndo wengi hawana cha kupoteza ndo maana nchi yoyote masikini ndo mtaji wa wapinzani na wanawasikiliza kweli, na nchi ikiwa na maskini wengi km TZ na bado isitatue matatizo yao ikizani ni siasa tu za wapinzani na ikafikiri ni maneno tu ndo yanaleta amani bila watu kushiba wasubiri yatakayotokea, km si leo basi miaka yaja.
ReplyDeleteKuhusu mbowe kurudisha gari me nasema haijarishe analengo gani ila naamini kitendo hiki kinatuma msg kwetu sote na serikali kwa ujumla kuwa matumizi ya mashagingi kwa maelfu na maelfu yaanze kupunguzwa km si lazima sana kuanzia sasa na siyo kuongea kwenye vyombo vya habari na mikutanoni tutapunguza matumizi leo au kesho au.....! Kweli ni aibu eti mashagingi kila mtu kisingizio barabara wakati wengine ofisi posta na kariakoo hafu wanaishi masaki, oysterbay n.k, basi mkitumia magari ya kawaida nahisi hata ujenzi na ukarabati wa barabara utaongezeka ili mabosi wetu wasisikie mashimo.
Anyway, nahisi mchangiaji wa kwanza aidha anasema kishabiki zaidi kiasi hata cha kuilazimisha nafisi yake ipoteshe ukweli kuwa amani na umasikini havikai zizi moja kwa muda mrefu.