Na Benjamin Masese
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU) Bw. Christopher Kazio ameidai kwamba Shirika ka Reli la Tanzania na Zanzibar (TAZARA) limepata
hasara ya sh. bilioni 12 kati Machi na Mei mwaka huu kutokana kusitishwa kwa safari za treni kwa siku 30.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Bw. Kazio kwa mara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kushika nafasi hiyo Mei 16 mwaka huu alisema kuwa TAZARA haitaonesha mafanikio yoyote ikiwa matatizo yanayoikabili hayatapata ufumbuzi wa haraka.
Bw. Kazio alisema kuwa kati ya Machi na Mei mwaka huu treni zilishindwa kuondoka vituoni kutokana na kukosa mafuta kitendo ambacho alidai kinafanywa kwa makusudi na Menejimenti iliyopo madarakani sasa huku ikitoa taarifa kwa umma zinazopotosha ukweli na uhalisia wa jambo lenyewe.
Alisema hivi karibuni manejimenti hiyo ilitoa taarifa kwa umma kwamba kila mwezi inapata hasara ya sh. milioni sita na kudai kwamba chanzo cha hasara hiyo ni kutokana na wafanyakazi kushindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa.
"Kinachofanywa na Menejimenti ya TAZARA ni kuhujuma ili shirika life, treni inashindwa kuondoka vituoni ikiwa sababu ni kukosa mafuta ambapo mkurugenzi ndiye anayesababisha yote hayo istoshe wafanyakazi.
"Wanapotoa kilio chao na mapendekezo kwa serikali hayasikilizwi,sisi tumefikia mahali kuona kuna dalili ya baadhi ya viongozi ndani wizara ya uchukuzi kuwa na hisa Tazara,"alisema.
Aliongeza kwamba hali ya TAZARA ni mbaya kiuzalishaji na imekuwa na madeni sehemu nyingi hivyo ameiomba Serikali ya Tanzania kufanya majadiliano na Zambia ili kuachana na ushirikiano huo ambapo kila nchi ijiendesha.
Alisema serikali ya China imekuwa ikitoa misaada mingi kwa TAZARA lakini hakuna kinachobadilika zaidi ya kuendelea kudhoofika na kuongeza kwamba ikiwa kila nchi itajiendesha mapato ya shirika hilo yataongezeka na hata pato la taifa.
Bw. Kazio alisema Menejimenti ya TAZARA imekikuka agizo la Waziri wa Uchukuzi, Bw. Omari Nundu alilolitoa hivi karibuni la kutaka kukutana na TRAWU na kumaliza migogoro yao.
Alisema mbali ya Trawu kupeleka barua ya kuomba kukutana na menejimenti hadi sasa hawajapata jibu lolote huku akidai ni dalili za kudharau serikali ya Tanzania.
Akizungumzia madai ya TRL ya kifuta jasho, mafao na mkataba wa hali bora kwa wafanyakazi alisema kuwa wembe ni ule ule kama ilivyokujwa kwa Marehemu Rwegasira huku akidai kwamba atazidisha makali ya kudai haki zao kusikilizwa na kutekelezwa.
Jamani huyu mwandishi wa habari hii ni mwongo sana ila nadhani mhariri unatakiwa kuwapeleka waandishi wako shule ili wakitia habari zile za ukweli. Tangu nizaliwe sijawahi kusikia shirika la Reli la Tanzania na Zanzibar, jamani huyu mwandishi inaonesha hajawahi kufika zanzibar aone hakuna reli ila angesema Zambia hapo kweli
ReplyDelete