01 June 2011

Madiwani wa UDP wasusia kikao

Na Zuhura Semkucha, Bariadi

MADIWANI wa Chama UDP Wilaya ya Bariadi mkoani Shinyanga wamesusia kikao cha Baraza la Madiwani kwa madai kuwa kucheleweshewa makablasha ambayo
yana taarifa za kamati mbalimbali ambayo yalitakiwa kuwafikia kabla ya siku saba kabla ya kufanyika kikao.

Tukio la madiwani hao kukisusia kikao hicho lilifanyika muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa Halmashauri, Bw. Bahati Magamula kufungua kikao hicho na kuruhusu kuendelea na ajenda mbalimbali za kikao huku akitoa maelezo ya kuchelewa kwa kablasha moja lenye taarifa kuwafikia madiwani wote kutokana na sababu za msingi.

Tuki hilo lilitokea saa 8.30 mchana lakini  madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliendelea na kikao kama kawaida.

Wakizungumza na waandishi  wa habari nje ya ukumbi mara baada ya kutoka katika ukumbi huo madiwani hao walisema kuwa  kikao hicho kinaendeshwa kibabe bila kufuata kanuni za kikao. 

Walisema wangeamua kuendelea na  kikao wangekuwa wanawadanganya wananchi kwa kujadili taarifa ambazo hawajazipitia kabla ya kuingia kwenye kikao.

Walisema kuwa katika baraza hilo waliweka maadhimio kuwa mtu atakaye sababisha kukwamisha kikao cha baraza la madiwani kishindwe kufanyika kwa  upande zote mbili  madiwani na watumishi wa halimashauri utagharamia gharama zote za kikao.

Hata hivyo baadhi ya madiwani hao akiwemo diwani wa Kata ya Luguru Bw. Mlyandingu Cheyo alisema kuwa waliatakiwa kupea makabalasha hayo na kuayapitia ili wabaioni ni wapia wanatakiwa kutoa ushauri ama kupatiwa ufafanuzi.

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw. Bahati Magamula awali akifunguwa kikao hicho aliwaomba madiwani kupokea makablasha na kuyapitia katika kikao

No comments:

Post a Comment