01 June 2011

TANESCO yanunua mitambo ya megawati 160

Na Peter Mwenda

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza ujenzi wa  mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 100 utakaotumia gesi katika Kituo cha Ubungo na
mwingine utakalozalisha megawati 60 na kutumia mafuta mazito katika mtaa wa Nyakato mkoani  Mwanza.

Mhandisi Mkuu wa Miradi ya Uzalishaji Umeme TANESCO, Bw. Simon Jilima aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam  jana kuwa mitambo hiyo itaanza kuzalisha umeme kuanzia Mei mwakani baada ya kukamilika kufungwa.

Alisema ujenzi wa mitambo hiyo mitatu itapunguza upungufu wa mahitaji ya umeme katika gridi ya Taifa ambayo kwa sasa ni megawati 260 kwa nchi nzima.

"Mitambo hiyo nimekwenda kuihakikisha mwenyewe kuwa inafanya kazi baada ya kufungwa nchini Sweden na kuwashwa ambako ilifanya kazi kwa ufasaha," alisema Bw. Jilima.

Alisema ujenzi wa mitambo hiyo unatokana na fedha za mkopo kutoka Benki ya HSBC ya Norway ambayo ni imetoa asilimia 85 ya fedha hizo na asilimia 15 ni fedha zimetolewa na Serikali ya Tanzania.

"Hii ni mitambo mikubwa ambayo inafika kontena zaidi ya 100 hivyo kutokana na ufinyu wa eneo letu hapa Ubungo ni mizigo mingi ambayo imegharimu fedha nyingi, thamani ya mitambo yote ni dola za Marekani 124,895,988 pamoja na kodi," alisema Bw. Jilima.

Naye Meneja Mawasiliano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud alisema kutokana na ongezeko la mahitaji ya umeme katika gridi ya Taifa, lililosababisha upungufu wa umeme, TANESCO limekuwa likifanya jitihada mbalimbali za kupambana na tatizo hilo.

9 comments:

  1. Bi. Badra Masoud,hakuna cha maana Tanesco kinachofanya kwani kodi ya wananchi italipia gharama hizo ambazo hazina faida.
    Kati ya wezi walioturudisha nyuma kitaifa,shirika lako la umeme linashika nafasi ya tatu,ndio lililotufikisha hapa pabovu tulipo. Siyo wewe pekee walikula zaidi wakati wa mzee mwinyi. Kinachoendelea sasa ni 'uncontrollable'. Kama mmeshindwa tulipokuwa miliyoni 30 kutupa huduma nzuri, je sasa arobaini na ushee unafanya nini! acheni mjerumani arudi!

    ReplyDelete
  2. tunajua hakuna lilojema kwa watanzania sijui watu wanachokitaka vichwani mwao badhi ni nn sio wote

    ReplyDelete
  3. Napenda kujua kati yenu hapo benchi la tanesco nani aliyekuwepo enzi za Waziri Mkuu mwenye "good personality" very smart guy, the late Moringe Sokoine???? Kulikuwa hakuna mgao wa umeme kamwe na viwanda vilikuwepo vingi tu! Sasa nataka kujua, nidhamu yenu ipo wapi??? Mpaka tumwite Sokoine aje kuwafundisha nidhamu, huh???

    ReplyDelete
  4. Kwanza eneo lenyewe la tanesco pale ubungo silo lenyewe hata kidogo! linge hamishwa lipelekwe mbali na kijiji chetu cha dar!!

    kwa taaarifa yenu kama hamjui akili yenu yote ipo kwenye workshop, study tours za kijinga na mikutano ya kutiana ujinga tu, taifa lenye nidhamu duniani kulikoni yote hadi mwaka 2030 watafunga nuke plants zote za nuclear na kuingia kwenye "renewable energy" kwa ajili ya umeme! nyie kazi ujinga wa siasa!!

    ReplyDelete
  5. wenzenu wajerumani wanapiga siasa lakini mambo ya muhimu yanakwenda shwari tu!! Ma-engieer wa tz ujanja wao wote........kutengeza mimashine ya kukamulia juice ya miwa na matofali wakati hizo mashine utazipata kwa bei nzuri tu ukienda kule gerezani-kariakoo!!
    tz tutakuwa wajinga miaka yote kwa kujiibia wenyewe humu humu nchini mwetu hadi Sokoine arudi tena lakini bila Sokoine ni ujinga mpaka mwishooo!!!

    ReplyDelete
  6. kati ya idara/taasisi za serikali ambazo hazina KAZI YOYOTE ILE zaidi ya kula pesa ya sisi wananchi ni bunge la kijinga ambalo halijawahi kutokea tz kamwe na PCCB (taasisi inayoongoza kwa RUSHWA NCHINI TZ!!!!!!!!! ZINGEVUNJWA HIZO tubakiwe na wizara tu chache kama ilivyokuwa wakati wa Sokoine na Nyerere!!! kulikuwa hakuna upumbavu kama huu ulivyo sasa hivi!!!

    ReplyDelete
  7. Msione sisi wananchi tumenyamaza mkidhani tunafurahia upumbavu wenu serikalini!!! nchi ina miaka 50 (hamsini) but ndo kwanza upumbavu unazidii! mnataka tufanye nini, nyie watoto?????

    ReplyDelete
  8. mchangiaji wa 1:46 umesema vyema. nchi yetu changa, viongozi kibao wengine hawana kazi matokeo yake ni kutafuta mianya ya kuiba. Lakini yote haya ni kutafutiana ulaji, leo mm nimekabidhiwa madaraka au ofisi kujikomba kwa wake nina unda taasisi na kuajiri mashemeji na wake wasio na tija yoyote. tusipobadilika tumekwishaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  9. Nawahakikisha TANESCO haiwezi kumaliza tatizo la umeme nchi hii. Uwezo wao wa ubunifu is virtually zero. Tanesco is a pool of fools

    ReplyDelete