20 May 2011

Serikali yachelewesha vitabu vya bajeti

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeshindwa kuwapa wabunge vitabu vya bajeti ya 2011/2012 siku 21 kabla ya Mkutano wa Bunge kuanza kama inavyotakiwa na Kanuni za Kudumu za
Bunge.

Kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la mwaka 2007), wabunge wanapaswa kupata nakala ya bajeti ya makadirio ya serikali siku 21 kabla ya Mkutano wa Bunge kuanza.

Pamoja na Kanuni hiyo, hadi leo jana zikiwa kimebaki siku 19 kikao cha bajeti kuanza, wabunge walikuwa hawajapata nyaraka hizo muhimu. Mkutano wa Bunge wa bajeti unanataratajiwa kuanza Juni 7, 2011.

Kwa mujibu wa Shirika lisilo la kiserikali linalojihusiaha utafiti kuhusu masuala ya bunge, Sikika, imekuwa ni kawaida kwa wabunge kupokea vitabu vya bajeti kwa kuchelewa, na wakati mwingine hupokea wakati Mkutano wa bajeti umekwishaa. Kuchapishwa kwa bajeti ya taifa kwa wabunge na umma kwa ujumla, ni hatua muhimu katika kuongeza uwazi, ubora na ufanisi katika bajeti.

Limetoa mfano wa mwaka jana, wabunge walichelewa sana kupata vitabu vya bajeti huku lihoji kama kweli wabunge waliijua bajeti waliyokuwa wakiipitisha wakati wa kikao.

"Kwa kawaida vitabu vya Bajeti vinawasilisha takwimu nyingi hivyo wabunge wanaweza ama kwa kujua au kutokujua kukubaliana na bajeti kwa ajili ya shughuli isiyo muhimu kwa wakati huo.

"Mfano mzuri wa kupitisha bajeti bila kujua ni kuidhinisha kwake kiasi cha sh. bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba mbili za makazi ya magavana wa Benki Kuu ya Tanzania mwaka jana, matumizi hayo yalivuta hisia za umma hata kupelekea Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kufanya uchunguzi hivyo kuiongezea serikali matumizi ya ziada," ilisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Sikika, Bw. Irenei Kiria.

Iliongeza: "Wakati Bunge likifanya uchunguzi wa sh bilioni 2.5 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za makazi, sh. bilioni 3.7 (kifungu cha 42, kifungu kidogo cha 2001 katika vitabu vya bajeti vya mwaka 2008/09 na 2009/10) kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi ya Spika huko Dodoma hazijahojiwa. Hii ni aibu na inaonesha madhara ya kukosekana kwa muda wa kutosha wa usambazaji wa taarifa za bajeti na hivyo kusababisha wabunge kutofanya uchambuzi wa kina hata kusababisha bajeti kutokuwa na ufanisi na tija.

Juhudi za kumpata Waziri wa Fedha, Bw. Mustafa Mkulo na Katibu wa Bunge ziligonga mwamba jana baada ya simu yake kuita muda mrefu bila kupokewa.

2 comments:

  1. Wanaharakati wasilianeni pia na ofisi ya rais na waziri kivuli wa wizara ya fedha. watanzania tunataka Tanzania inayowajibika!

    ReplyDelete
  2. YOTE HII NI MATUNDA YA UONGOZI MBOVU.

    ReplyDelete