LISBON, Ureno
POLISI wenye silaha walitinga kwenye jengo linalomilikiwa na mwanasoka nyota, Cristiano Ronaldo kwa kile kilichoelezwa kuwa kufuatilia uhalifu.Walikwenda
katika eneo hilo, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa uchunguzi kuhusu utekaji wa magari na mashine za kutolea fedha.
Jirani alisema: "Polisi walitoka na mtu huku akiwa amefungwa pingu na akiwa na begi jeusi, ambapo alikuwa amechukua vitu kwenye gereji.
"Vijana wote waliokuwa wakiishi pale, kila wakati walikuwa wakiendesha tofauti, wakiwa na magari yenye nguvu."
Nyota wa Real Madrid, Ronaldo mwenye miaka 26, alikuwa amenunua nyumba hiyo ya ghorofa mbili katika eneo la Alcochete, karibu na mji mkuu wa Ureno, Lisbon mwaka 2008 wakati alipokuwa akichezea Manchester United.
Novemba mwaka jana Ronaldo, alipatwa na mashaka baada ya uvamizi kufanyika karibu na nyumba yake yenye thamani ya pauni milioni 4.3 mjini Madrid, ambapo jirani yake alikamatwa kwa kutuhumiwa kuwa na dawa za kulevya zenye thamani ya pauni milioni 175.
No comments:
Post a Comment