Na Gladness Mboma
ALIYEKUWA Mwenyekiti Mwanzilishi wa Chama cha Jamii (CCJ), Bw. Richard Kiyabo amejitokeza na kumpinga kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe juu ya waanzilishi wa Kilichokuwa Chama Cha Jamii (CCJ) huku akidai kuwa waliotajwa hawahusiki.
Bw. Kiyabo ambaye alibwaga manyanga CCJ baada ya kukosa usajili na kuhamia CHADEMA, na baadaye kurejea CCM na kushiriki katika kampeni dhidi ya Bw. Mpendazoe wakati wa kampeni kwenye Jimbo la Segerea, aliibuka jana na kumpinga Bw. Mpendazoe, akisema kuwa watu aliowataja kama waanzilishi hawakuwa wa kweli.
Bw. Mpendazoe amekaririwa juzi akiwataja Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Samueli Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, Katibu wa itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nauye, Mbunge wa Lupa, Bw. Victor Mwambalaswa na Bw. Paul Makonda kuwa walikuwa miongoni mwa waanzilishi wa CCJ.
Bw. Kiyabo alisema kuwa yeye na Bw. Renatus Muabhi ndio waliokuwa waanzilishi wa CCJ, na miongoni mwa watu waliojiunga nacho ni Bw. Mpendazoe ambaye alitaka kuwa Mwenyekiti wa Taifa, lakini hawakukubali ombi lake ambalo hakuliwasilisha kimaandishi.
"Chama kilimpitisha kuwa msemaji. Swali la kumuuliza Bw. Mpendazoe alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa ni hao aliowataja? Na je, hao walikuwa na nyadhifa zipi na kazi zipi za chama? Je, amesahau kwamba alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Bw. Sitta kwamba ajiunge na CCJ?," alihoji Bw. Kiyabo.
Bw. Kiyabo alisema kuwa vyama vya siasa hasa CHADEMA wanatakiwa kukumbuka kwamba siasa za udaku hazitawafikisha ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo wanajaribu kuonesha.
Alisema kuwa Watanzania wamekua kisiasa na ndio maana hawakuwaingiza CHADEMA ikulu kwa kura zao na kwamba kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kuchaguliwa kwenye chumba cha kupigia kura.
"Namshauri Bw. Mpendazoe na wenzake wa CHADEMA waache siasa za udaku. Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika na siyo udaku. Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha, mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera mpya ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi," alisema.
Alisema kuwa kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha, ambapo aliongeza kuwa CHADEMA wameonyesha kwamba nguvu ya umma siyo kura tena, 'bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani'.
Bw. Kyabo aliiponda CHADEMA, akisema kuwa wanajiita Chama cha Demokrasia na Maendeleo, lakini ajabu wanayoyaonesha siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa 'chama chao ni cha maandamano na vurugu'.
"Je, wanaiheshimu kweli demokrasa? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watanzania kwa kura zao, sasa kwa nini hawawaheshimu, wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka CHADEMA ishinde uchaguzi. La hasha. Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao," alisisitiza bila kutoa mifano ya kauli hizo.
Alisema kuwa huu ni wakati wa kujenga Taifa, hivyo kinachotakiwa ni kushirikiana na serikali na siyo wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha na kuwataka Watanzania kuwa makini na wanasiasa wasioutakiwa mema utaifa wao na amani ya nchi.
"Tukumbuke kwamba suala la amani ni sawa na nyanya ikitumbuliwa kuishona tena huwa ni kazi ngumu sana. Bila amani shughuli za kimaendeleo haziwezi kufanyika, hata shughuli zao wenyewe CHADEMA hawataweza kuzifanya," alisema.
Naye Katibu CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Kilumbe Nge'nda alisema kuwa wamesikitishwa na taarifa zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA kuhusu Bw. Nape kuwa aliomba kugombea kwenye chama hicho baada ya CCM kumteua mwanachama mwingine kugombea jimbo la Ubungo.
"Ukweli ni kwamba Bw. Nape alikuwa miongoni mwa wanachama 13 waliojitokeza kuomba wateuliwe na CCM kugombea ubunge katika jimbo la Ubungo lakini kipindi chote cha mchakato wa kampeni za kutafuta mgombea ndani ya CCM, alikuwa akitoa kauli kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, kwamba ataheshimu matokeo na atakuwa tayari kumsaidia mgombea yeyote atakayeteuliwa na CCM ili chama kipate ushindi," alisema.
Alisema kuwa Bw. Nape hajawahi kuomba kuteuliwa kugombea CHADEMA na ingekuwa hivyo asingepata hata nguvu ya kuanika ufisadi unaokiandama chama hicho 'cha wanaharakati kinachofanana na chama cha wanasiasa'.
Hivi karibuni, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CHADEMA, Bw. Mabere marando alisema Bw. Nape baada ya kushindwa kura za maoni ndani ya CCM aliomba kugombea kupitia CHADEMA lakini baada ya kumjadili ndani ya vikao walibaini hana sifa kumshinda Bw. John Mnyika ambaye kwa sasa ndiye mbunge wa jimbo hilo.
Bw. Kiyabo asihadae umma kwa kupotosha taarifa iliyotolewa ktk vyombo vya habari juu ya madai ya Mpendazoe. Ikumbukwe kwamba, madai ya Mpendazoe yaliyoripotiwa kkt vyombo vya habari yalidai kuwa hao aliowataja walishiriki ktk mchakato wakuanzishwa CCJ japo ktk hatua za mwisho hawakujiunga na chama hicho.
ReplyDeleteMadai ya Mpendazoe kwakiasi fulani yanaungwa mkono na taarifa ya majibu ya madai hayo toka kwa Mh.Sita iliyotolewa ktk vyombo vya habari siku chache zilizopita. Yeye alionyesha kuwa mtu ambaye ni makini si ajabu kufuatwa na vyama vingine na kushawishiwa ahamie huko. Alieleza wazi kuwa yeye ni mtaji wa Urais. Na kwamba mazungumzo ya aina hiyo ni ya kawaida ktk shughuli za kisiasa na kumshangaa Mpendazoe kuona kama kauli yake haikuwa ya maana hata kidogo. Hayo ya Nape pia yamejibiwa juu juu tu.
Binafsi nakubaliana na maelezo ya Mh. Sitta japo katika vita ya maneno ya kisiasa, mazungumzo hayo yanaweza kutafsiriwa kwa namna tofauti, namna 2 kama hiyo ya Mpendazoe na pia hiyo ya Sitta mwenyewe. Zaweza kuwepo tafsiri nyingine zaidi.
Sasa hayo maswali Kiyabo anayotaka tumuulize Mpendazoe hayana mantiki hata kidogo. Huwezi kutaka Mpendazoe athibitishe kama alipojiunga CCJ aliwakuta hao aliowataja wakati anakueleza hawakupata kujiunga na CCJ japo walishiriki ktk mchakato wa uanzishwaji wa chama hicho kama utengenezwaji wa katiba uliofanywa na Nape kwa madai yaliyotolewa na Mpendazoe. Pia swali juu ya nyadhifa zao CCJ halina maana tena kwa sababu nilizozitoa hapo awali. Na jambo la kunukuliwa na vyombo vya habari kuwa alitaka Mh.Sitta ajiunge na CCJ linazidi kuunga mkono hoja ya Mpendazoe kuwa hao aliowataja hawakuwahi kuwa wanachama wa CCJ. Kwa kigezo hicho tu, Kiyabo hakutakiwa kuhoji nambari za uanachama au nyadhifa za watu hao ambao Mpendazoe anadai kuwa walishiriki ktk mchakato wauanzishwaji wa CCJ.
Kiyabo kwakua mmoja wa viongozi waanzilishi wa CCJ hapati uhalali wa kuaminika eti kwasababu hiyo tu, hata kwa maswali anayohoji pasipo logic na maelezo yake kupingana na ya Mh.Sitta ambayo japo hayakueleza moja kwa moja ila yanaashiria mazingira yakuwaepo kwa mazungumzo ya kisiasa ambayo yeye anayaona ni ya kawaida katika maisha ya mwanasiasa aliye makini.
Watanzania tunapaswa kuwa makini na kauli za hivi karibuni zinatotolewa na wanasiasa.Tusizichukue hivi hivi, lazima wakati wote tuzichambue na kuzihoji. Vinginevyo tunaweza kuishia mahali pasipo pazuri kama tutakua tu bendera fuata upepo hata kwa mambo yaliyodhahiri kama hayo ya Bw. Kiyabo.
SIO SIRI KIYABO ANAONEKANA KAMA HAYUPO SAWA,ALIKUWA CHAMA CHA MAJAMBAZI,AKAHMIA SISIJ AKAENDA CDMA SASA SISIM.HOJA ZA HUYU BWANA NI KAMA MTU ANEONGEA NA WATU WASIO NA ELIMU NA UELEWA WA JAMBO LENYEWE.HESHIMA YA KISIASA IMESHUKA SANA NA HANA USHAWISHI WOWOTE MBELE YA WATU HATA AKINUNULIWA KUKANUSHA TUHUMA ZINAZOTOLEWA DHIDI YA MNAUYE BADO WATU HAWAZICHUKULII KWENYE UZITO KWANI AMEKUWA SIO WA KUAMINIWA.
ReplyDeleteJAMII HII YA VIONGOZI NDIO IPO KWA HAWA RAFIKI ZETU SISI MINYAWATU,
HATA AKITHIBITIKA HAWEZI JIUZURI SISI MINYAWATU HAWANA UJASIRI HUO.
Kiabo hana jipya,yeye akae afanya mambo yake,coni logig ya kutetea wa2 ambao wao kwa kauli za na majibu yao inaonyesha dhahiri kwamba wahucka katika ,mchakato huo vyombo vya hbr vimeandika nnape baada ya kuhojiwa juu ya mambo hyo anjibu yaliyopita cndwele wazi alihucka ss kiyabo anatwambia nn?
ReplyDeleteccm wameshindwa kupunguza gharama za maisha chadema wanaandamaama kuonyesha ni jinsi gn,ccm icvyojari na swala la democrca ni nani ambaye hajaona matatizo ktk uchaguzi?
Kiyabo anadai democracia wkt matokeo yalichakachuliwa walikoshinda chadema hd wa2 waliandamana ndy yakatangazwa,hvyo Kiyabo bila maandamano hii ccm ya waongeaji na cyo watendaji wakiongozwa JK wao haiwezi kutoa haki wala kufuata hyo democracia na ni kweli watanzania ss ni waelewa lkn cyo kwa mambo km yako hayo ya kinafki........
nyie wote mlio toa mawazo hapo juu mnajipya tuwape nchi mmoja wenu kama ataiweza?ugumu wa maisha haupo kwenu tu msifikirie eti nchi yenu kuwa na madini ndio mtakuwa matajiri nani kawaambia madini yanaleta utajiri wa nchi?mtaendelea kuwa masikini tu asiekuwa nacho atafute hakuna wa kuwabeba mzee msuya alisema hayo miaka ya thamanini hakuna wa kukushika mkono na kuelekeza uende kinywani kwako
ReplyDeleteInashangaza sana wapenzi wa chadema kuamini kila lisemwalo na chama chao, iwe kashfa , matusi ,uzushi na mbaya zaidi asitokee mtu kupinga au kutoa mawazo tofauti nao.Hivi mtu kuhama au kuwa na nia kuhama chama ni dhambi? Mwalimu nyerere alisema"ccm si baba wala mama yake" na alitishia kurudisha kadi iwapo msimamo wake ungepingwa, nae tumuite msaliti? hivi kiongozi gani wa upinzani hakupitia ccm au tanu? acheni watu watoe maoni yao kama ninyi mfanyavyo na si kuponda kila kitu.Hivi sitta, nape au mwakyembe kuratibu uanzishwaji wa CCJ iwe ndio sera ya chadema kupata ukombozi wa watanzania wanaoshindia mlo mmoja! chambueni hali ya uchumi wetu na si kuchambua watu binafsi. kwani viongozi wa chadema ni malaika?
ReplyDeleteHivi mradi neno likitamkwa na kiongozi au mdandiaji kama mpendadezo na vyombo vikiandika basi ni kweli?Mbona mnashangaza upenzi huu wa siasa umekuwa kama wa mpira?
ReplyDeletempendadezo kadai kuwa Nape,Sitta,na mwakyembe walishiriki kuanzisha CCJ. aliyekuwa mwanzilishi na Mwenyekiti amabae ndie aliyemkaribisha mpendadezo kwa kishindo anamkana bado mnashikilia kuwa huyo kyabo ni mamluki hivi shule mnazo soma nyinyi zinafundisha somo la ukaidi au maksudi?Tuwe makini sio kukubaliana na utumbo ili mradi eti kiongozi kasema!!!
Nyie mnafikiri kiyabo atasema nn kama sio hayo?yeye ni kada wa CCM LAZIMA AWATETEE...mwambieni atutajie basi ao vigogo sita wa ccm aliokuwa anatamba watahamia CCJ wakati alipokuwa mwenyekiti..
ReplyDeleteALIPOKUWA CCJ KIYABO ALIKUWA ANATAMBA KWAMBA KUNA VIGOGO sita KUTOKA CCM WATAJIUNGA...SASA KAMA SIO HAO ALIOWATAJA MPENDAZOE AWATAJE WAKE ILI TUMUAMIN...anazania tumesahau?bora angekaa kimya anazid kujidharaulisha
ReplyDeletekyabo atutajie hao vigogo waliokuwa waanzilishi wa ccj, ikiwa dovutwa alikuja kumtetea ridhiwani kuwa siyo billionea itakuwa huyu kiyabo, ufisadi hautakwisha tanzania mpaka viongozi wote wazee wangatuke
ReplyDeleteKYABO ANAONGEA UTAFIKIRI HAFIKIRII, HIVI KILICHOWA KINAMSUMBUA KUHAMAHAMA VYAMA NI KUTOJIAMINI. ILA NAKUMBUKA HATA DARASANI ALIKUWA MWEHU TU HANA LOLOTE, ACHA WENYE THINKING CAPACITY WAONGEE. WE SUBIRI MSAADA WA URAIS UPEWE VITI MALAAM KKA
ReplyDeleteKIYABO HATA AKIKAA NA WENZANKE ATAWASINGIZIA UONGO..MUONGO HUYO JAMAA NI BALAA!!
ReplyDeleteHATUJASAHAU WALE VIGOGO SITA ULIOSEMA WATAHAMIA CCJ WATAJE BASI TUKUAMINI.