09 May 2011

Beckham na mkewe wazidi kutesa kwa utajiri

LOS ANGELS, Marekani

MCHEZAJI nyota David Beckham na mkewe Victoria, wameripotiwa kuwa na utajiri unaofikia pauni milioni 165.Nyota huyo wa soka na mkewe, ambaye ni mwanamuziki wa
zamani wa kundi la Spice Girl wanadaiwa kufikisha kitita hicho, baada ya mwaka jana kuingiza fungu la dola milioni 20 wakishuru mafanikio ya kazi ya uanamitindo inayofanywa na Victoria, ambayo imewavutia wateja wake wengi.

Mwimbaji huyo wa zamani wa muziki wa pop ambaye hivi sasa ana ujauzito wa mtoto wa nne, hivi sasa ameongeza ubunifu wa mikoba ya akina mama hali ambayo indaiwa kuwa huenda faida ikaongezeka muda wowote.

Katika shughuli hizo za uanamitindo, Victoria amesaini mkataba wa mamilioni ya pauni na kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari ya Range Rover.

Lakini hata hivyo mwana dada huyo, anadaiwa hajamzidi mumewe ambaye ameshajikusanyia fedha nyingi kupitia soka.

Miaka miwili iliyopita Beckham (36), kabla ya kukatwa kodi alikuwa akilipwa pauni milioni 56 na Klabu yake ya Los Angeles Galaxy, wakati hivi karibuni alitangaza kuingia mkataba wa mamilioni ya pauni na Kampuni ya Samsung wakati atakapokuwa balozi wake kwenye michuano ya Olimpiki itakayofanyika mwakani jijini London.

No comments:

Post a Comment