Na Patrick Mabula, Kahama
ASKAFU wa Jimbo Katoliki la Kahama Mhashamu Askofu Lodovick Minde ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali na wa Vyama vya Siasa kutoisahau jamii ya watu wenye
ulemavu na watu wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwasaidia misaada mbalimbali ya kijamii ili wasijione kama wanatengwa kwa vile hawakupenda kuwa hivyo kwani hayo ni Mapenzi ya Mungu.
Askofu Minde alitoa wito huo juzi katika Sherehe ya Pasaka iliyokuwa imeandaliwa katika Parokia ya Ngaya, Kahama na na Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige kwa watu wenye ulemavu wa Jimbo la Msalala.
Akizungumza katika Sherehe hiyo iliyotanguliwa na Misa Takatifu ya Pasaka, Askofu Minde aliisema kuwa serikali na Vyama vya Siasa vinapoapanga mipango mabalimbali kutowasahau watu wenye ulemavu ambao wanauhitaji makubwa katika maisha yao .
"Kuanzia ndani ya Jamii, viongozi mbalimbali tunawajibu pia wa kuwapenda walemavu ambao nao hawakupenda kuwa na hali hizo na kuishi maisha kama hayo na wamekuwa wakitamani kuishi kama binadamu wengine wasiokuwa na ulemavu wowote lakini kwa Mapenzi ya Mungu wakajikuta wanazaliwa hivyo au alikuwa mizima lakini wanapata kilema katika maisha yetu ya kila siku,"alisema Askofu Minde.
Kwa upande wake Bw . Maige ambaye pia ni mbunge wa jimbo hilo aliwataka walemavu kuacha kuwa watukutu bali wawe na tabia nzuri na pale wanapopata misaada inayotolewa na wasamalia wema , waitumie vizuri kwa maendeleo yao katika maisha yao ya kila siku .
Bw. Maige alisema kupata na kuwa mlemavu siyo dhambi wala adhabu hiyo ni mapenzi ya Mungu basi wanatakiwa kuacha ukorofi kwa kisingizio cha ulemavu wawe waadilifu kwa kujikosoa na kuwadhibiti wale wakorofi wanao kwamisha juhudi zao za maendeleo yao kwa kujinufaisha kupitia migongo yao.
Aliahidi na kuwahakikishia ataendeleza kutoa misaada mbalimbali kwa walemavu hao kadri atakavyoweza na katika sherehe hiyo alitoa msaada wa shilingi millioni moja na laki moja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi baada ya Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Bw. Charles Kafuku kudai kuwa shirikisho hilo halina ofisi
Aidha akitowa shukrani zao Bw. Kafuku walimuomba Bw. Maige kupeleka hoja serikalini ili wakati wa ukusanyaji wa maoni ya rasmu ya mabadiliko ya katiba yanayoendelea sasa hivi hapa nchini kuwa nao washirikishwe katika uundwaji wa katiba mpya .
TANZANIA HAIWAJALI WALEMAVU.USTAWI WA JAMII HAWAFANYI KAZI KABISA ,SIKU MOJA NILIONA PICHA KWENYE MICHUZI ILE PICHA ILIKUWA YA KUTOKA TANGA,YULE KIJANA ALIKUWA ANA UTINDIO WA UBONGO MZAZI WAKE AMEMFUNGA KAMBA KAMA MBUZI ILI ASIONDOKE NYUMBANI,SASA HIYO NI KAZI YA SERIKALI KUWAUDUMIA WALEMAVU JAMANI SIO OFISI ZA SERIKALI KUWA NA WAZIRI ANATUMIA MAGARI YA THAMANI WAKATI WALEMAVU WANATESEKA .INASIKITISHA SANA ILE PICHA NILIIPRINT NINAYO NITAITUMA KWENYE VYOMBO VYA HABARI VY KIMATAIFA KUONYESHA UNYANYASAJI WA WALEMAVU TANZANIA
ReplyDelete