02 March 2011

Rais Kikwete kutoa mada Ufaransa leo

Na Edmund Mihale

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kutoa mada kuhusu  umuhimu wa shughuli za uziduaji na uwazi katika mapato ya madini katika mkutano wa Kimataifa wa
Tasnia ya Uziduaji, (EITI), ambayo ina malengo ya kuongeza uwazi na uwajibikaji katika mapato yatokanayo na uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia.

Mkutano huo wa siku mbili unaanza leo,jijini Paris, Ufaransa, Tanzania iliomba na kupewa uanachama wa muda wa EITI   2009  na itapata uanachama kamili baada ya kukamilisha na kutimiza vigezo vya kuwa mwanachama kamili na kuweka  misingi  ya utoaji taarifa hizo muhimu kwa umma juu ya malipo ya kodi kutoka makampuni mbalimbali  yaliyopo nchini.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi Habari ya  Ikulu Dar es Salaam  jana, ilieleza kuwa lengo kuu la kujiunga na EITI ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia kwa kutangaza hadharani malipo yanayotokana na rasilimali zake kwa manufaa ya wananchi.

"Utaratibu huu utaweka uwazi  na kuondoa usiri ambao unaweza kuwa mwanya wa kuficha mapato halisi ya kampuni husika.

"Baada ya kumaliza mkutano huo wa Paris, Ufaransa, Rais Kikwete atasafiri kwenda moja kwa moja Nouakchott, Mauritania kwa ajili ya kikao cha marais wa Afrika wanaotafuta suluhisho la tatizo la kisiasa katika Ivory Coast," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Ilieleza kuwa akiwa  Mauritania, Rais Kikwete atajiunga na marais wa Mauritania,  Afrika Kusini,  Burkina Faso, Chad, Nigeria na Equatorial Guinea pamoja na wawakilishi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Balozi Jean Ping na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN).

Katika kikao hicho, viongozi hao watafikia uamuzi wa AU kuhusu mzozo huo na kupendekeza namna gani ya kuutatua mzozo huo uliolipuka kutaokana na  raundi ya pili ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa Ivory Coast Novemba 28, mwaka jana.

Ilieleza kuwa , nchi hiyo imegawanyika katika sehemu mbili, moja ikimuunga mkono aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bw. Alassane Quattara na nyingine ikimuunga mkono rais aliyekuwa anatetea kiti chake katika uchaguzi huo,  Laurent Gbagbo.

Kila mmoja kati ya wanasiasa hao amejitangaza kuwa rais na kila mmoja ameunda na kutangaza serikali katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Wiki iliyopita, viongozi hao wa Afrika walikutana mjini Nouakchott na baadaye walikwenda  Abidjan, Ivory Coast ambako walikutana na viongozi hao wawili nchini humo katika jaribio la kutafuta suluhisho la mzozo huo.

6 comments:

  1. Hivi huyu rais wetu ni lecturer ?

    ReplyDelete
  2. Hivi waziri wa nishati na madini au katibu mkuu wa wizara ambao ndiyo haswa wataalam wasingefaa kwenda kutoa hiyo mada! Nchi ipo kwenye hali tete sana. The president should stay at home and concetrate on the current problems. (Electricity, instability of the currecy,food shortage etc

    ReplyDelete
  3. Kula good time President.

    Temana na wasiojua starehe.

    Tanzania haijafikia kiwango cha kumng'oa aliye madarakani kama Misri,Algeria,Libya.... Kama likivimba litamvimbia anayekuja baada yako wewe wakatihuo umejichimbia kama Ben. Isitoshe Watanzania wepesi wakusahau shida. Poa braza nitakushauri tena next time naona nimeitwa nje kidogo.

    ReplyDelete
  4. Hiyo mada ambayo kwake hawajui itaanzia ugenini?

    ReplyDelete
  5. Hivi watanzania kwa nini man wivu sana president wenu akisafiri kidogo tu.

    Mnataka makae naye hapa "tule mihogo wote misaada atahemea nani?"

    Au, hamjui yeye ndiye msuluhishi wa migogoro afrika hii- mnafikiri amani itapatikana je Bwana Kikwete akikaa hapa tu

    ReplyDelete
  6. tehetehetehete!! sasa, wakati yeye ni failure regarding the theme atamfundisha nani? halafu washauri wa raisi muwe munamuelimisha basi na mwenzenu, wanamuita akasuluhishe mgogoro wa wizi wa kura wakati yeye ni mwizi wa kura, wanamuita akafundishe udhibiti wa rasilimali wakati yeye ndiye mpotezaji namba moja!! au wanataka awakilishe opinions / models zinazolead into failure?

    ReplyDelete