02 March 2011

Mbowe: Tutaandamana hadi kieleweke

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amemjibu Rais Jakaya Kikwete akisema chama chake kitaendelea
kuwahamasisha wananchi kufanya maandamano ya amani mpaka pale serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) itakaposikia kilio chao.

Alisema CHADEMA haitaogopa vitisho vilivyotolewa juzi na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taifa wa CCM kwa vile serikali yake imeshindwa kuweka sera sahihi zitakazowaondolea Watanzania ugumu wa maisha.

Bw. Mbowe alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga na vitongoji vyake mara baada ya maandamano makubwa yaliyoanzia eneo la daraja la Mhumbu hadi katika viwanja vya Joshoni kata ya Kambarage, manispaa ya Shinyanga.

Rais Kikwete hivi sasa amepata presha kubwa kutokana na maandamano haya ya amani pamoja na mikutano ya hadhara inayoendeshwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, anasema CHADEMA tunachochea vurugu na kuwahamasisha wananchi waikatae serikali na wamuondoe rais madarakani.

Sisi tunasema tutaendelea na maandamano haya mpaka pale kitakapoeleweka, ni maandamano ya amani, kama yeye Kikwete anaona yanamkera basi atukamate atuweke ndani, na tunasema watu wa usalama wa taifa mpo hapa, mpelekeeni salaamu hizi, hatuogopi kitu, tutaandamana, tutaandamana na kuandamana mpaka kieleweke.

Kikwete anapaswa aelewe kwamba sisi siyo wendawazimu,  tunaandamana kwa kuwa hatutaki ailipe DOWANS kama vile kamati kuu yake ya CCM ilivyokuwa imeamua, serikali yake iwaondolee Watanzania ugumu wa maisha, sasa anapozuia maandamano na mikutano anatarajia Watanzania tutazungumzia wapi.
 
Ni budi ajifunze utaratibu mwingine wa nguvu ya umma wa kuzungumzia matatizo yao, maana njia zile za kidemokrasia zimeshindikana kutokana na maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura kuchakachuliwa na watu wa CCM.
 
 Hii ni njia mpya njia muafaka ya kuiamsha serikali ya CCM ijue ina wajibu kwa Watanzania, leo Kikwete anazungumzia matatizo ya sukari, anafikiri matatizo ya Watanzania ni sukari peke yake, maisha ya wananchi yamepanda kwa ujumla kwa sababu serikali yake haina sera mbadala.
 
Tunamweleza rais kuwa huu ni mwanzo tu, hana haja ya kupata presha, hatuwezi kuiheshimu serikali ambayo inashindwa kuondoa kero za wananchi na kuwaheshimu wananchi wake, haitaki kuwasikiliza,"
 
"Ameshindwa kuwawajibisha watendaji wake pale wanapofanya makosa ya makusudi.

Hakuna waziri anayethubutu kujiuzulu kutokana na uzembe unaofanyika katika wizara zao, tatizo la umeme mmeliona, mabomu ya Mbagala mwaka juzi na sasa Gongolamboto hakuna anayewajibika, sasa tufanye nini kama siyo kuandamana? alihoji Bw. Mbowe.

25 comments:

  1. mboe tatizo sio ww nimakengeza ndio yanayosababisha wewe umelaniwa na mungu ndiomaana ukawa na makengeza wewe ni shetani atakae kufuata ni shetani mwenzio

    ReplyDelete
  2. Napenda kutoa tahadhari kwetu sote watanzania tuwe makini na tunachoshabikia ni kweli tuna matatizo mengi sana hilo halina kupinga ni kweli kabisa,lakini na tuangalie njia tunazozitumia zina athari gani na zipi,maana kirusi kilichoenea huko ughaibuni kwa wenzetu ni Kuongoza kwa njia za ufalme,udikteta,na pia kuamua bila kupitia bunge na pia ni kuwa hawana demokrasi ss tunafanya uchaguzi kila miaka 5,na ikiwa tunataka kutumia njia hii Chadema wakafaulu basi ujuwe kesho itatumika njia kama hiyohiyo kuipinga hiyo Serikali ya CDM nchi itakuwa haikaliki kwa furaha kwani si rahisi CDM wakaingia madarakani wakaanza kubadili maisha mara moja itachukuwa muda pia hapo vurugu hazitaisha tuwe MAKINI, tusifikiri ni lele mama tuangalie wenzetu sasa baadhi yao wengi wamekuwa wakimbizi ghafla.

    ReplyDelete
  3. LEO IWEJE KIONGOZI WA CDM AKASEME WAZI KUWA HATUWEZI KUIHESHIMU SERIKALI!MAANA YAKE KUWA NA WANACHAMA WAO WAANZE PIA KUIDHARAU HV KWELI WAKO MAKINI?AU WANAFIKIRIA KUWAHAMASISHA WATU NI NJIA SAHIHI YA KUANDAMANA KILA KUKICHA HAYA YETU MACHO, ASIYE SIKIA LA MKUU ...,

    ReplyDelete
  4. Ndugu wadau, kutoa maoni ni haki ya kila mtanzania, lakini tujitahidi kutumia lugha nzuri. si vyema kumkashifu mtu kutokana na maumbile yake. Pia hata wewe unaye mkashifu mh. Mbowe pia nawe si mkamilifu katika maumbile yako.

    ReplyDelete
  5. Kuna watu wa CCM leo ndio wanatoa maoni yao,ngoja tuwape uwanja.Sema ni busara hata wao wakakubali kuwa wanachotetea CHADEMA ni sahii kwa mustakabali wa nchi hii.Acha waandamane,acha watu wajue ukweli,mind you 2015 vijana ndio watakuwa asilimia 75 ya wapiga kula wote,hata wazee baadhi wameanza kutambua umuhimu wa mabadiliko,vijana wa leo hawavutiki na wala hawavutiwiw na hoja za akina Makamba,Chiligati na watu kama hao,kwao kina makamba wanawakilisha kizazi cha watu wanaong'ang'ania madaraka na kukataa kupisha vijana kwenye ajira na kuwaona ndio wanaosababisha wao kuzunguka mitaani kila siku na vyeti.please CCM tafuteni vijana wasemaji wenye mvuto etc kama kina Nape,Bashe and the like wawe wanakisemea chama,vinginevyo you are heading to a great fall.

    ReplyDelete
  6. Watanzania wenzangu,naomba tutumie vizuri uhuru wetu wa kutoa maoni kwenye Mtandao.Nchi zingine uhuru wa namna hii haupo.Si vyema sisi tulionao tunautumia vibaya.HAIPENDEZI KABISA.Toa maoni ya ki-ungwana inatosha.

    ReplyDelete
  7. Habari za kuaminika leo DR Slaa yuko anahojiwa na polisi kahama heti kwa kufanya mkutano bila kibali,kisa heti wakati akiwa njiani kwenda kahama alisimamishwa na wananchi njia akasimama akawasalimia tayari kwa CCM eti kakosea kafanya mkutano bila kibali,naomba kuuliza kama mjinga,hivi vibali vya mikutano au kusalimia wananchi ukiwa on transit vinatakiwa kwa vyama vya upinzani tu,je CCM nao wakitaka kufanya mikutano au maandamano,au kiongozi kusimama njiani kusalimia raia anahitaji kibali cha polisi?

    ReplyDelete
  8. Huyo pmb anayesema Mbowe ni makengeza hana macho na kisha inaelekea kichwa chake kimejaa matope na sio akili. Huyo kalewa njaa inayosababishwa na sera na ufisadi mkuu wa utawala wa ccm. Matahira kama hao ndio vipenzi vya chama na serikali yake. Huna lolote, wewe ni kahaba wa kisiasa uliyetawaliwa na upumbavu. Wacha Mbowe na wanachadema wawahamasishe Watanzania.

    ReplyDelete
  9. Kakuambia nani kuna demokrasia huku Bongo. Demekrasia ya kuchakachua kura? Demokrasia ya sheria ya vigogo na sheria ya watu wa kawaida? dmokrasia ya kuwanyanganya wananchi ardhi na kuwapa wageni? demokrasia ya kulinda na kuwakumbatia maswahiba ambao wanajulikana wazi kuwa mafisadi wa kutupwa? demokrasia ya kupora hela za umma (benki kuu, n.k.) na kuzitumia kuweka watu madarakani? demokrasia ya kutumia hela za umma kwa magari, ndege, na safari nyingi na mikutano wakati wananchi wanakufa kiu na maji? Tunabunge ndio, lakini la aina gani? Juzi makinda kamfanyia nini Lema na ushahiri wake juu ya Waziri Mkuu? Demokrasia ipi wakati wabunge wanahongwa mikopo ya milioni tisini wakati wafanya kazi na walalahoi wanakufa njaa? Hiyo ndiyo demokrasia kwa staili ya Tanzania. CCM imeoza, inanuka. CCM inayokumbatia hata uchawi ni kiama cha nchi hii. Akina Slaa, Mbowe na Chadema kwa ujumla: fanyeni kazi, endeleeni na uzi huo huo kutuondolea hiki kisirani.

    ReplyDelete
  10. Huyo 9:02 usitake sifa kwa kumtusi kiongozi wetu shupavu,hakuna uliloomba kwa muumba kukuumba mzima wa viungo lakini kakupa ulemavu wa ubongo!!Akili yako naona haina akili kabisa!!!utaendelea kuwa kimada wa ccm na hakuna unachoambulia wewe na ndugu zako!!!Ujue shetani alikuwa malaika mkuu wa mungu!!Lakini wewe ni ibilisi na ccm ni zimwi!!Pambaf zako

    ReplyDelete
  11. Daima hakuna kisichobadilika, mabadiliko huwa hayawezi kuzuiwa na wimbo wowote wa kipumbavu. Kama Libya ambako huduma za kijamaa ni bora kuliko za kwetu na zinatolewa bure bado wananchi wanataka mabadiliko sembuse Tanganyika?Wakati ndio huu.Nguvu ya umma juuuuuu!

    ReplyDelete
  12. Aliyemwambia mwenzake ana makengeza amekosa la kuchangia,je umejichunguza kwanza kama wewe huna maana inawezekana wewe ndo mtu nusu kabisa zaidi ya unayemsema.Kama huna maoni ya kujenga nenda kauze karanga kwenu.
    KWA SASA HOJA SI MACHAFUKO HYA NCHI BALI NI UTAWALA MBOVU WA CCM UNAOSABABISHA YOTE HAYA.HATA WANAOTETEA WANAJUA KABISA WANAUMIA SO TUAMBIANE UKWELI KISOMI

    ReplyDelete
  13. WANAO TETEA WOTE NAJUA NI WANA CCM, ILA SISI TUNASEMA: KUANDAMANA LZM MPK KIELEWEKE. TUNATAKA BEI YA SUKARI, MAFUTA NA GHARAMA YA MAISHA ISHUKE KWANI SISI WANANCHI TUNAUMIA SANA KWA MLIPUKO WA BEI ULIOKO KWA SASA.

    ReplyDelete
  14. tunaipongeza CDM kwa uamuzi uliuchukua, kwani wanasema ukweli mtupu, inatakiwa CCM iige na ibadilishe mfumo wake wa kupandisha bei vitu ovyo kama wanahama.

    hao wanaowatetea wana CCM naona ndio mafisadi wakubwa wanaokula na kumeza nchi yetu kwa kupandisha vitu bei.

    ReplyDelete
  15. TUNATAKA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA waliyotuahidi CCM kwa ari mpya, nguvu mpya na Kasi mpya. Hii ndiyo aliyoahidi.

    Sasa kama anasema hata nyerere alishindwa, kwa nini alisema yeye ana nguvu mpya, nguvu mpya na kasi mpya? Alitudanganya?

    Maana asingesema kuwa mambo yatakuwa mapya, watu wasingempa kura 2005. Hii ya juzi anajua mwenyewe kama tulimpa au hatukumpa.

    Leo analalamika CDM wanamfanyia fujo, lakini mbona kwa siku 100 ambazo chadema walikuwa hawajaanza kuandamana, hatatuambia dira inayotupa matumaini?
    Tuendelee tu kuvumilia mpaka 2015?
    Haiwezekani! Hata kama uchaguzi utafanyika 2015 tena lakini tunataka awajibike, tena haraka, asilale kusubiri 2015.
    CDM kazaneni. Akiona hawezi ang'atuke kama sio kujiuzulu.

    ReplyDelete
  16. Kwa ukwel na uwazi serikal imeshindwa kutuonyesha vijana wap kesho yetu imelala,watu tumemaliza kidato cha sita hamna hata sehem ya kujishikiza,ukimaliza Chuo huajiriwi bila uzoefu,huo uzoefu utatoa wap wakat wazee wameng'ang'ania madaraka?tunajicfia tuna amani wakat wapo watanzania kibao wacojua ucku watakula nn!wanamiliki magar ya bei mbaya wakat wengyne twakosa hata huduma za afya kwa umackin uliokithir hku kwe2,watoto wanaacha shule kutokana na kukosekana kwa ada.tunakupenda raisi wetu ila twahitaj mabadiliko zaid ya unavyofikiria...

    ReplyDelete
  17. mchangiaj wa kwanza anaaibisha kwa kumfananisha kiongoz shupavu kama mbowe na mizuzu ya ccm.kikwete hana lolote zaid ya kuuza sura marekan. huez kumlingansha m2 shupavu kama mbowe na kituko kama kilaza wako kikwete

    ReplyDelete
  18. mbona hukuona mambo makubwa anayowafanyia watanzania badala ya makengeza yake? jifunze kuangalia ya maana na maslah kulko ya kipuuz

    ReplyDelete
  19. kumbe huu ndui upunguwani wa wanaCCM. nyerere alipowaambia kikwete hafai mwaka ule kuwa bado hajakuwa mlidhani alikuwa na maana kuwa alikuwa hajapata balehe mtu wa miaka 47? akasisitiza tena kuwa kama mnamwona mzuri si mumchukuwe mkanywe naye chai?? bado hamkuelewa....sasa habari ndiyo hiyo, ni kiongozi weak kuliko wote historia ya nchi hii imewahi kushuhudia. na tutaandamana hadi kieleweke!

    ReplyDelete
  20. yote sawa kwani hakuna binadamu anayeweza kumpa binadamu mwenzake maisha mema asilimia 100, wote wanataka kula tu wapeni hao chadema nao wale washibe kelele zipungue, afrika hakuna kiongozi anayejidai kuwa atawapa wananchi maisha nafuu, uongo mtupu, andamaneni muwape ulaji Slaa,mbowe na wenzake waridhike kwani hata akina mbowe fedha walizoziiba serikalini bado hazijawatosha,andamaneni tu muingie Ikulu, Kikwete amewapa uhuru, mnajitamba eti mtaleta maisha bora kwa kushinikiza,eti kura zilichakachukuliwa, mfa maji aachi kutapa tapa, haya andamaneni kama Misri na Libya muingie madaraka Mundu wa wazungu nyie mnaopenda waafrika wauawe eti wataleta maisha bora,hizo fedha mnazozunguka nazo mtazilipa kwa rasilimali za watanzania wala hakuna lolote,mbona hata Obama alifagiliwa na bado ameshindwa, sembuse Mbowe na marafiki zake mwafrika Mweusi . Naililia Afrika! Afrika!Afrika vichwa vya wendawazimu, wasomi wa kiafrika wanatumiwa na Wazungu kama boya hawako Stable yaani bendera fuata upepo,hawana akili ya utambuzi. wazalendo wa Afrika mnawatukana, mnawaua mmemaliza nguvu ya Afrika na kufuata ushenzi wa nchi za Magharibi, hakika laana imeikumba Afrika. Afrika! Afrika!.

    ReplyDelete
  21. Alichosema Rais Kikwete ni uvunjifu wa amani ambao unaweza kusababishwa na maandamano ya uchochezi ya CHADEMA. Jaribuni kushirikisha ubongo mnaposhabikia mambo nyie mbumbumbu! Mnashabikia vita!? mnashabikia vifo?!! Do you know kwamba ikitokea vita hawa viongozi wa CHADEMA watakuwa less affected nyinyi mapunguani?
    Mbowe anampa rais siku tisa amalize matatizo ya wananchi yeye amekuwa nani?Akipewa yeye ndio atayamaliza?Au huyu muhuni wao aliyelaaniwa Slaa ndio mnadhani anaweza kumaliza matatizo yenu? For your information huyu Mbowe mnayemshabikia tunamjua in and out. You dont the true face of Mbowe and Slaa you folk!!
    Au kwa kuwa wanapambwa na magazeti yao(Mwananchi,Mwanahalisi,Tanzania daima) ya waliyoanzisha ya kuchochea vurugu? Do you know mmiliki wa magazeti hayo ni nani? Take time to think you folk. Ikitokea vita wa kuathirika ni mimi na wewe,na sio Kikwete,Slaa au Mbowe.
    CHADEMA wanaendesha siasa pendwa zinazoshabikiwa kwa kiasi kikubwa na watu wenye udini,wasomi walionunuliwa kama akina Dr.Lwaitama,Prof.Baregu,wanafunzi wa vyuo vikuu wanaoshawishiwa wagome kwa maslahi ya viongozi wa CHADEMA..STUPID!!
    Actually i couldnt imagine hata wasomi wenu wananunulika kirahisi namna hii kama nyanya tena zilizooza sokoni!! Na hii inanipa chalenge kuwa mfumo wetu wa elimu ahujaandaliwa kumjenga msomi wa Tanzania kuwa na "critical thinking",something must be done.. watu wanaburuzwa kama magari mabovu na wao wanakwenda tu!!
    Na hiyo vita mnayoitafuta,mtaipata then myaonje machungu yake..(Kumbukeni hakuna vita inayoanza kwa kupigana moja kwa moja,huanza kwa kutupiana maneno kama sasa).If that is what you need,it will not take long to take us there..
    Mwenyezimungu tuepushe na vita katika nchi yetu,kwani haijawahi kuwa vita ni yenye kujenga bali hubomoa,na hasa vita isiyopiganwa katika misingi ya haki kama wanayotaka kuanziasha CHADEMA,tuepushe na wenye kulaaniwa hawa wanaotaka kuhatarisha uhai wetu bila sababu,washishie maradhi mabaya watu hawa uwakoseshe nguvu ya kutembea na kueneza sumu hii katika nchi yetu.

    ReplyDelete
  22. Mambo gani makubwa aliyoyafanya Mbowe kwa Watanzania? Ni yapi hayo? Labda kwa nyie msiemjua mgeni nae sie tunayemjua Freeman na ndugu yake Charles walipokuwa vijana wanawatukana kina Nyerere na kusimama nje kwao kuwakejeli watanzania eti masikini wafuasi wa Nyerere kwa kuwa tu nchi ilikuwa kwenye ujamaa na baba yake na marafiki zake kina Mzee Ndesa na Mzee Mtei walikuwa mabepari wakubwa nchi hii. Sasa leo wale masikini wa Nyerere ndio kawageuza mtaji na kuanza kuutumia umasikini wao ndio mambo makubwa hayo?

    Pili mambo gani makubwa hayo ya kuchukua mabilioni ya NSSF enzi ya Mkapa ambayo mpaka leo hataki kuyalipa? Huyu ni msafi? Ana usafi gani FISADI mkubwa.

    Na huyo mkwewe Mtei ana majumba na kumiliki mali kibao nje ya nchi kapata wapi huo utajir kama sio UFISADI alioufanya alipokuwa waziri wa fedha enzi za Nyerere? Hebu tupisheni huko mtatumika kama tambara la deki wenzenu wakipata wataendelea kutanua kama mwanzo.

    Swali kwangu kama wao wanakubalika kwa wananchi kinachowafanya wasisubiri wakachaguliwa kwa kura wakati wa uchaguzi ni nini?

    Swali lingine kama wanapesa za kuchezea kufanya maandamano yasiyo na kichwa wala miguu kwanini Mbowe halipi mabilioni anayodaiwa huko NSSF walalahoi wakapewa chao? Yeye si ana huruma na wananchi masikini kwanini basi hataki kulipa pesa za michango za walalahoi alizokwenda kuchukua enzi ya Mkapa? Huruma gani hiyo?

    Ngoja niishie hapa kabla siaanza kumchambua huyo babu mwingine na kumwaga ufisadi wake hapa!

    Tena nia rahisi ya wao kuchaguliwa hizo pesa wangetumia kupeleka miradi ya maendeleo majimboni mwao hata ingebidi kuweka solar au kuwa na midi hydros ambazo hazihitaji mitaji mikubwa na mwishoe watu wangewachagua kwa kuwaona kuwa wako serious, ila hawa lengo lao ni lingine lazima wamtumikie aliyewatuma! Kazi wanayo waambieni siku hizi kila kitu kiko wazi sio zile enzi za Nyerere walizokuwa wanatuita masikini wa Nyerere! The Matarese Cyle lol!

    ReplyDelete
  23. Mimi kwa umri wangu nimeshavuka ujana, ninalekea uzee, nimeona na kutumikia awamu zote za uongozi katika nchi hii, Ninafahamu mazuri na mapungufu ya awamu zote nne, sina chama chochote cha siasa, ni muislamu kwa kuzaliwa lakini nadhani siamini sana katika dini, nimesoma vizuri masomo ya sayansi katika vyuo vikuu mbali mbali ndani na nje ya nchi. ningependa kusema kwamba kwa kweli nchi inahitaji mabadiliko, na nadhani kwa hali ninavyoiona mabadiliko kwa sasa hayazuiliki, yanakuja kwa kasi sana, ninawaomba viongozi wasome ramani ya wakati, na wananchi wote tujiandae kwa mabadiliko ambayo nadhani hayazuiliki. Wito wangu kwa watanzania ni kwamba tuyakaribishe mabadiliko haya kwa amani. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  24. Nini maana ya nguvu ya soko ambayo tumeikumbatia. Na pale nchi ikiendeshwa kifisadi utaona hata biashara zinaendeshwa hivyo hivyo. Suala la sukari kupanda bei si kwa bahati mbaya. Wanajua, sukari ni ishu kwa watanzania, then what they do, is to create a scacity scare, reduce supply and then politisize it. Bang!!!!!, si unaona sasa serikali inaagiza sukari kwa dharura (Unajua inapokuwa ni dharura maana yake ni nini????), lakini at the same time sukari ya Malawi kule mpakani Mbeya ni shilling mia sita (600) un beleavable. Kwa hiyo ukiiruhusu mpango wa kifisadi hautafanikiwa inawekwa marufuku kwa sukari hiyo kuhudumia mikoa ya karibu na Malawi. Ukikamatwa na TRA au serikali huko mbeya, mali yako inataifishwa na mahakamani juu (No msalie Mtume) wafanya biashara wanajua, wakikamatwa huwa wanaachia mali yao kwa madereva wasiojua kwa sababu gari hunganganiwa! na ili kukomesha kabisa hata gari lilobeba linawajibika kulipa mafaini mengi ambayo huwa alimanusra nalo kuuzwa/kunadiwa. haijalishi ni kiasi gani cha sukari ali mradi ni ya Malawi. Waulizeni watu wa Mbeya. Hii ni Tanzania yetu, msishangae sana kwa sababu maandalizi ya kukusanya fedha za kampeni ya 2015 imeshaanza. Hawangojei hadi kuchwe.

    ReplyDelete
  25. Ndugu yangu uliye post (March 2, 2011 11:04 AM),i agree with you..You have addressed the good point. Wengine mnao post kwenye ukurasa huu kiushabiki wa kivyama,nawashauri mtulie muandike mambo yenye tija.Hata kusoma wanayo post wengine ni njia ya kuelimika.
    My point: Pamoja na yote haya,we still have have to think about one thing crucial,AMANI KATIKA NCHI YETU NI MUHIMU KULIKO VITU VYOTE. Approach ya CHADEMA katika ku-address mambo haya watatupeleka pabaya. Tujiulize kitu kimoja.Katika hali ya kawaida,CHADEMA ni chama cha upinzani,ambacho kilio chao na vyama vingine vya upinzani ni kuwa hawana fedha,leo maandamano nchi nzima,wamepata wapi hizi fedha?Do you think wakishika dola watalipa na nini hizi fedha kama si kodi zetu kama ambavyo CCm wanatulipisha madeni ya hela wanazotumia kwenye kampeni? Msisahau Mbowe ni mfanyabiashara kama anavyojulikana na wengi(mi sijui ni biashara gani zaidi ya kumiliki ukumbi wa disko(Billcanas),kumiliki kampuni ya kuchapisha magazeti ya free media inayochapa magazeti ya Tanzania daima,na gazeti lingine nimelisahau..

    ReplyDelete