11 March 2011

Fabregas kukosa mechi ya FA

LONDON, Uingereza

NAHODHA wa Arsenal, Cesc Fabregas atakosa mechi ya Jumamosi ya michuano ya kuwania Kombe la FA, itakayochezwa Old Trafford mjini
Manchester.

Fabregas aliumia msuli wakati alipokuwa akicheza katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, dhidi ya Barcelona.

Alisema: "Dakika kumi na tano katika nusu ya kipindi cha pili, nilihisi kubanwa maumivu na nilijua kuwa mchezo kwangu umekwisha."

Kiungo huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 23, sasa atafanyiwa kipimo cha skana kuonesha kiwango cha tatizo.

Mchezaji huyo alikosa kucheza katika fainali ya Carling na mechi ya nyumbani iliyoishia kwa sare dhidi ya Sunderland, baada ya kutoka kwa maumivu katika mechi dhidi ya Stoke.

Habari mbaya zaidi kwa kocha, Arsene Wenger ni kwamba Thomas Vermaelen, anaweza kuwa nje ya uwanja kwa msimu wote uliosalia.

Beki huyo wa kati wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 25, alifanyiwa upasuaji wa enka Januari na alikuwa anatarajiwa kurudi uwanjani mwezi huu.

Lakini Vermaelen alisema: "Sijui ni wakati gani nitaweza kucheza tena. Haiwezekani kuwa Machi. Sijarejea hata katika mazoezi. Huu ni wakati mgumu kwangu."

No comments:

Post a Comment