LONDON, Uingereza
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Didier Drogba amekanusha madai kuwa anataka kuondoka Stamford Bridge, baada ya kutokuwa na msimu mzuri kwa
ufungaji magoli.
Drogba amekuwa na msimu mbaya ambapo Novemba mwaka jana alipatwa na malaria, msimu huu ameweza kufunga mabao 10 tu.
Huku kochaa Chelsea, Carlo Ancelotti akiamua kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji kwa kumsaini Fernando Torres, kutoka Liverpool kwa ada ya pauni milioni 50, Januari.
Kulikuwa na uvumi kuwa anaweza kuondoka huku klabu za Marseille na Real Madrid, zikitajwa kumtaka.
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, aliyejiunga na Chelsea akitokea Marseille kwa ada ya pauni milioni 24 mwaka 2004, alisema kuwa anataka kuendelea kuchezea timu hiyo na anafuraha.
"Ni kila kitu ambacho ningeweza kutaka nacho nikiwa Chelsea," Drogba alikimbia kituo cha televisheni cha Orange Sport cha Ufaransa.
"Katika klabu kubwa, kwa kuwa una wachezaji wakubwa wa kusisimua, nikiwa na mazingira mazuri ya maisha kwa ajili ya familia yangu."
"Miaka iliyopita ningeweza kusema: "Nilikuwa nikitamani kuchezea AC Milan, Real, au Manchester United."
"Lakini kwa sasa, sijisikii hivyo zaidi. Niko katika moja ya timu nzuri zaidi duniani. Matamanio yote yameshaondoka."
No comments:
Post a Comment