17 March 2011

Chelsea yaliwinda kinda la Sao Paulo

LONDON, England

TIMU ya Chelsea ipo mbioni kukamilisha usajili wa kinda wa timu ya Sao Paulo, Lucas Piazon ambaye amepachikwa jina la Kaka mpya.Mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 17 kwa sasa anakipiga katika timu ya taifa ya  Brazil ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ambayo ni mabigwa wa Amerika Kusini  na Blues ina matumaini ya kufikia naye makubaliano atakapotimiza umri wa miaka 18.

Miezi miwili iliyopita, Piazon alikuwa mbioni kujiunga na timu ya Juventus baada ya kutumia muda wa wiki moja akifanya mazoezi nayo, lakini hata hivyo Chelsea inaonekana kuwazidi kete baada ya mmiliki wake Roman Abramovich, kuendelea kumwaga fedha katika soko la usajili.

Hata hivyo bado haifahamiki wazi ni kiasi gani timu hiyo itatumia kumnasa Mbrazil huyo, lakini inasadikika kwamba huenda ikawa ni kati ya pauni milioni 5 na milioni 8.

No comments:

Post a Comment