10 February 2011

Viongozi wa dini watoa maazimio kulinda amani

Na Peter Mwenda

MKUTANO wa viongozi wa dini za kikristo na kiislamu wa Mkoa wa Dar es Salaam wameitaka serikali katika ngazi zote iwashirikishe katika kuleta
imani nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Alhad Musa Salum alisema mkutano huo umeazimia mambo kumi ambayo yakitekelezwa kwa vitendo itasaidia kukemea uovu.

"Viongozi wa dini waepuke kununuliwa na viongozi wa vyama vya siasa kwa maslahi ya imani zao, vyombo vya habari vitunze maadili ya kazi yao kwa maslahi ya nchi," alisema Shekhe Salum.

Alisema umoja huo utakuwa endelevu na kuazimia kuandaa mkutano mwingine katika kipindi cha miezi sita ijayo kuzungumia hali ya amani nchini.

Mkutano huo ambao mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi, Askofu wa Kanisa la African Inland Church (AIC), Bw. Charles Salala alisema ni wajibu wa viongozi wa dini kuhubiri na kuombea amani na kuacha malumbano baina yao.

Shekhe Khamisi Mataka aliyetoa mada kwa upande wa waislamu alisema wanadamu wameumbwa na akili bila matamanio, lakini wamekuwa hawana tofauti na wanyama ambao waliumbwa na matamio bila akili.

"Viongozi wa dini wanapaswa kuwa madaraja ya mshikamano baina yao...tukubali kuwa amani ndiyo msingi wa kila kitu," alisema Shekhe Mataka.

Akifungua mkutano huo Bw. Mengi alisema viongozi wa dini kwa kutambua nafasi na majukumu yao kwa kutumia taratibu na mingi ya dini husika wameifundisha jamii na kuvileleza vizazi namna ya kuishi kwa kumcha Mungu katika upendo na amani.

Alisema amani katika bara la Afrika ambako hakuna amani watu wananufaika kuuza silaha na kutaka vita iendelee ili waendelee kuisha maisha mazuri.

Bw. Mengi alisema taifa lolote lile rasilimali yake ni amani kuanzia moyoni na kuingia kwenye mahusiano na kuongeza kuwa mahali popote ambako hakuna amani pana hofu.

1 comment:

  1. Hapo ndipo unafiki wa viongozi wetu wa dini unapokuja. Ninyi kweli mtakataa kununuliwa! Hivi huyo Wakala wa Kanisa Mengi siye aliye kununua wewe Alhadi pale Diamond Jubilee wakati wa hafla ya walemavu na kukwambia uufikishe ujumbe kwa wasiofika pale. NINI BWANA, MAMBO YOTE MSHIKO NA UNAFIKI. Hii bado, tutawaona tena katika sura nyingine ya unafiki!

    ReplyDelete