02 February 2011

Tyson apata mtoto wa tisa

NEW YORK, Marekani

BINGWA wa zamani wa masumbwi katika uzani wa juu, Michael Tyson na mkewe Lakiha Spicer Tyson, wamepokea mtoto mwingine baada ya
mwanamke huyo kujifungua mtoto wa kiume.

Vyanzo vya habari vilivyopo karibu na wanandoa hao, vilieleza kwamba familia hiyo ilipokea mtoto huyo wiki iliyopita na kwa sasa, Tyson na Lakiha wana furaha kubwa na kila mmoja anajivuna.

Wanandoa hao ambao tayari wana mtoto mmoja, ambaye wamemzaa pamoja aitwaye  Milan alikuwa bado hajapewa jina.

Taarifa hizo za furaha zilikuja ikiwa ni miezi 18, tangu afariki mtoto wa Tyson aliyekuwa na umri wa miaka minne Exodus, aliyefariki mwaka 2009.

Tyson tayari alishaoa mara mbili kabla, wakiwemo waigizaji Robin Givens na Monica Turner na amezaa watoto watano Rayna, Amir, Mikey, Miguel na  D'Mato, kutoka katika ndoa zake na marafiki zake wa kike.

Bondia huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 44, ambaye ndiye bondia wa kwanza kutwaa taji la uzani huo akiwa na umri mdogo, baada ya kushinda taji hilo mwaka 1986 anafikiriwa kuingiza dola milioni 300 katika kipindi cha kazi yake, lakini Mei mwaka jana akadaiwa kifilisika ila akasema kuwa anajisikia mwenye furaha katika  nafasi aliyopo.

No comments:

Post a Comment