Na Grace Michael
WAZIRI wa Uchukuzi, Bw. Omar Nundu ameweka mambo wazi kuwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) haijawahi kutengeneza faida kwa kipindi chote
ilichofanya kazi na badala yake serikali ndio ilibeba mzigo mkubwa hata wa kulipa mishahara ya wafanyakazi.
Bw. Nundu aliyasema hayo jana katika Kamati ya Miundombinu ambapo alikuwa akieleza hali halisi ya Shirika la Reli Tanzania.
Unajua napata kigugumizi kuwaita RITES kama walikuwa ni wawekezaji au ni watu gani, kwani wao walikuwa na hisa asilimia 51 na serikali asilimia 49 lakini mzigo wote ilibeba serikali kwa kuwa hawakuwahi kuzalisha faida katika kipindi chote, alisema.
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa baada ya kuvunja mkataba na kampuni hiyo kinachosubiriwa kwa sasa wahusika wa kampuni hiyo kuja kwa ajili ya kusaini makubaliano ya kuvunja mkataba ili serikali iweze kuachana nao.
Alisema TRL iko kwenye hali mbaya kwa kuwa mpaka sasa inategemea treni mbili za reli ya kati lakini serikali ina mkakati wa kuhakikisha ifikapo Juni kuwe na treni tatu.
Itatengenezaji faida wakati huu ni mradi batili wa ufisadi mtupu? Huu ni mfano mmoja kati ya mingineyo mingi inayoonyesha dhahiri jinsi ufisadi ulivyoteka nchi yetu katika kipindi hiki cha miaka mitano tangu awamu ya nne iingie madarakani. Ona walivyochote mahela huko hazina kwenye uchaguzi wa mwaka jana na sasa nchi karibu imefilisika.
ReplyDeleteMh. Waziri Nundu, tafadhali tuambie je kuna yeyote atakaye wajibishwa baada ya kuvunjwa mkataba? Je hao walio saini mkataba huo ulilifilisi kabisa TRL,je watawajibishwa. Au ndio kuwalipa mabilion hao RITES halafu kuuingia mkataba mwingine wakiutapeli na matapeli wengine?
ReplyDeleteyale yale ya fidia yanakuja na huku
ReplyDeleteNdugu zangu watanzania hivi hawa viongozi wetu na hizo degree wanazojipa mbona nashindwa kuelewa kila leo madudu. Muheshimiwa rais jk chagua viongozi wenye uzalelendo,na maadili ya kazi maana sioni faida ya usomi wao sasa sijui kama elimu waliyopata ni kujifunza jinsi gani uibe vizuri.Kama serikali itaamua kujikita kwa nguvu zote fukueni hili shirika la reli ni kitega uchumi cha uhakika jaribuni hiyo reli ifike KIGALI,NA UGANDA muone Lakini viongozi wenyewe ufiasadi umeshika hatamu hizo mlizokwisha chukuwa hazijawatosha?hebu mkae mfikirie na nchi yetu au mpaka muone kama yaliyotokea RWANDA?
ReplyDeleteKWAKWELI MIMI NAFIKIRI WATANZANIA KUNA UMUHIMU WA KUAMKA SASA MAKE TUMELALA JAMANI HAWA VIONGOZI WETU WANAZANI WANAONGOZA NCHI ILIYOJAA WAJINGA MATOKEO YAKE HII ITAKUA KWA FAIDA YA WATU WALE WALE NA KWA MANUFAA YA WALE WALE MASKINI WANAZIDI KUA MASKINI NA MATAJIRI WANAZIDI KUA MATAJIRI,EMBU TUJIULIZE JAMANI MIMI TOKA NAZALIWA NALISIKIA SHIRIKA LA RELI MPAKA SASA HATUONI MAFANIKIO YA SHIRIKA HILI JAMANI HII NI HAKI KWELI?WAHINDI WALIIBA VYUMA WAKAONDOKA SERIKALI INAFUMBIA MACHO VITU HIVYI WAKATI NDIO VINAFAA KUA UTI WA MGONGO WA UCHUMI WA TAIFA LETU,JAMANI TUTAFIKA KWELI NAMNA HII.......!!!!!!!!!!!!
ReplyDelete