14 February 2011

NSSF yaisadia BFT sh. milioni 1.6

Na Zahoro Mlanzi

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), umetoa udhamini wa sh. milioni 1.6 ili kufanikisha mashindano ya Taifa ya ngumi za
ridhaa kutafuta Mabingwa wa Taifa, yaliyopangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, Februari 26 hadi Machi 5, mwaka huu.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Msemaji wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Eckland Mwaffisi, alisema udhamini huo umedhihirisha dhamira ya mfuko huo kuendeleza na kuibua vipaji vya mabondia wa ridhaa nchini.

Alisema hadi sasa, mashindano hayo yamepata udhamini wa NSSF pekee, mbali ya umuhimu wake kwa taifa, pia itasaidia kupata mabondia ambao wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa.

Mwaffisi alisema, si mara ya kwanza kwa NSSF kuona umuhimu wa kudhamini mashindano makubwa ya ngumi za ridhaa ambayo yanaandaliwa na BFT.

òMwaka 2010, mfuko huu ulitoa udhamini wa sh. milioni moja ili kufanikisha mashindano ya kimataifa ya ngumi za ridhaa ya Afrika Masharik ya Bingwa wa Mabingwa.

òNatoa mwito kwa mifuko mingine ya jamii, taasisi, kampuni na wadau wengine wa michezo, kuiga mfano wa NSSF ili mashindano haya yaweze kufanikiwa kama yalivyopangwa ambapo mikoa 21, tayari imethibitidha kushiriki,¦ alisema Mwaffisi.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya ngumi za ridhaa, Hurtado Pimenter kutoka nchini Cuba, atachagua mabondia ambao wataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ikiwemo michezo ya Afrika, ambayo imepangwa kufanyikia mjini Maputo nchini Msumbiji, Septemba mwaka huu.

Alisema gharama za mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 25, ambapo hadi sasa, BFT imepata sh. milioni 1.6 kutoka NSSF .

Alisema mashindano hayo yana umuhimu mkubwa kwa Taifa kwani mchezo wa ngumi za ridhaa na riadha, ndiyo pekee iliyoweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na wachezaji wake, kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

òLeo, mchezo wa soka ndiyo unaopewa kipaumbele na wadhamini kuliko michezo mingine, ambayo kama itapata udhamini wa kutosha, Tanzania itafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na kuondoa dhana iliyojengeka kwa wachezaji wetu kuitwa watalii,¦ alisema.

No comments:

Post a Comment