11 February 2011

Mbowe: Tutashirikiana na kamati za bunge

Na Tumaini Makene

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa msimamo wake rasmi juu ya mwelekeo wa kambi ya upinzani bungeni, baada ya
kubadilishwa kwa kanuni na uchaguzi wa uongozi wa kamati za kudumu za bunge, kikisema kuwa kitatoa ushirikiano wa dhati kwa wenyeviti wa kamati hizo, ilmradi wafanye kazi kwa uadilifu.

Pia kimeweka wazi msimamo juu ya hatma ya wapinzani wote kushirikishwa katika baraza kivuli la mawaziri ambalo atalitangaza wakati wowote, kikisema kuwa suala hilo kwa sasa haliwezekani, bali litategemea kutibiwa kwa majeraha na kurudisha kuaminiana miongoni mwa vyama vya upinzani vilivyoko bungeni, hapo baadaye.

Akizungumza na Majira jana, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho, alisema kuwa CHADEMA kinawatakiwa kila la heri wabunge wenzao wa upinzani waliochaguliwa kuongoza kamati mbili za bunge, kikiwahakikishia ushirikiano kadri utakavyohitajika.

"Kama unavyojua kuwa kuna wabunge wa upinzani ambao pia ni wenyeviti wenzangu wa taifa wa vyama vya siasa, ambao wamechaguliwa kuwa wenyeviti wa kamati za kudumu za bunge...tunawatakia kila la heri katika utendaji wao. Wasiwe na hofu, sisi tutawapatia ushirikiano wa dhati, kwani kazi waliyopewa ni kazi ya taifa na ni wabunge wenzetu, ilimuradi tu wafanye kazi kwa uadilifu.

Kuhusu kuwashirikisha wabunge wengine wa upinzani kwenye baraza kivuli la mawaziri la kambi ya upinzani bungeni, Bw. Mbowe alisema kwa sasa, suala hilo haliwezekani kwani bado kuna majeraha makubwa na hali ya kutoaminiana kwa kiasi kikubwa miongoni mwao, tangu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, uchaguzi wa mameya, uchaguzi wa spika na naibu spika na hata matukio ya juzi katika kubadili kanuni na uchaguzi wa wenyeviti wa kamati.

"Lakini kama unavyojua siasa ni mchezo wa ajabu sana, hakuna rafiki wala adui wa kudumu katika siasa. Hatuna chuki na yeyote, lakini hatuwezi kuunda umoja usiokuwa na maridhiano. Ushirikiano wenye mashaka unaolazimishwa au kupigiwa chapuo na CCM lazima uwe na walakini. Ushirikiano huu hauwezi kuzaa tija kwa taifa.

"Ni hali ya kusikitisha sana kuwa wapinzani tumeruhusu CCM kiwe ndiyo blocker (dalali) wa mahusiano yetu, CCM ndiyo kinatuchagulia viongozi watakaokwenda kusimamia mapato na matumizi ya serikali yake, yaani tunaotakiwa kuwasimamia wanatuchagulia watu wa kuwasimamia. Lakini ni matendo yao ndani na nje ya bunge yanaweza kurudisha imani.

"Kwa hiyo baraza kivuli la mawaziri ambalo nitalitangaza wakati wowote baada ya vikwazo vilivyokuwa vikichelewesha kuwa vimeondoka, halitakuwa la kudumu...linaweza kubadilika wakati wowote na kuwaingiza wapinzani wenzetu kama tutafikia maelewano ya msingi, tukaaminiana, tukajenga mahusiano mazuri ya kisiasa na kimtazamano.

"Kwa sasa hapana. Baadaye inawezekana, hasa kwa vyama ambavyo havina ushirikiano rasmi na CCM. UDP hawana ushirikiano rasmi na CCM, NCCR pia, na TLP, lakini hata CUF ambao wana ndoa rasmi na CCM huko Visiwani, nao huwezi kujua maridhiano yatachukua muda gani, mwaka jana walikuwa wapinzani asilimia 100 leo ni hamsini kwa hamsini, huwezi kujua kesho itakuwaje, milango itakuwa wazi," alisema Bw. Mbowe.

3 comments:

  1. HEy sio blocker ni broker (dalali. Tafadhali badili makosa

    ReplyDelete
  2. Jamani huyu Mbowe hanaanalolijua katika siasa yeye anajua habari za madisco tu,Cuf sikama kwa wanandoa na CCM au si wapinzani,Upinzani si kipinga tu hata mambo ya maana sasa yeye alitegemea Zanzibar watakaa hivyohivyo mapaka lini wakati mambo waliyoyataka yamefanyika asilimi 90 ?lazima uangalie maslai ya taifa si ubishi tu wa simba na yanga.Mmechaguliwa na wananchi kuwakilisha si kikimbia hoja bungeni mnapokimbia mnamaana gani? inaonyesha kabisa hamjakomaa kisiasa na wewe Kabwe nilikuwanakuona unauelewa wa siasa kumbe walewale waliokunywa uji wa mgojwa na wao wagonjwa.Huyu Mbowe si mwanasiasa ni mwizi tu hanalolote analolijua uongozi wakupewa na babamkwe ndiyo matokeo yake hayo,Wananchi kuweni macho msidangwanywe.

    ReplyDelete
  3. MH!!!!!!!!!!! KWELI SIASA NI NGUMU BORO NLIYEJIAMULIA KAWA MKULIMA, JAMANI UNAPOMJAJI KIONGOZI HATA KAMA HATOKI CHAMA CHAKO AKIFANYA JAMBO JEMA MSIFIE TU UUMPE MOYO, HIVI WW ULIYECOMENT HAPO JUU UMEIILEWA HABARI KWELI!!!!!????????????ULIMTAKA MBOWE AWAJUMUISHE WOTE KWA SASA ILIHALI HAWAPATANI? KESHASEMA NILA MUDA WATAKAPOBADILISHA TOFAUTI ZAO WATAWAWEKA WENZAO HIVYO BAS HATA MIGOGORO IKIISHA WIKI IJAYO SI ATAWAWEKA! KWELI KWAAKILIZAKO NANATUPIANA VIJEMBE KILA SIKU WATAWEZA KEFANYA MAMBO YENYETIJA KWELI KWA SASA? CHAMUHIMU NIKUBADILISHA TOFAUTI ZAO WOTE WAWE KAMA WAPINZANI KWELI HATA NA HAO CUF KAMA MUUNGANO ULIKUWA KWAMASLAH YA WANANCHI TOKA MOYONI BASI NAO WASIMAME KAMA WAPINZANI KWELI KWEL TENA WAKIJITAHIDI 2015 ZENJ NIYAO KABSA HATA MATOKEO WAMEZIDIWA KIDOGO SANA, BASI WAACHE KUWA UPANDE WA CCM HAPO HATA CHADEMA WAKIWASEMA TUTAWAJIA JUU ILA KWA SASA NIKWELI WAKO UPANDE WA CCM KUMBUKA HATA KIPINDI CHA CHAGUZ NDOGO ZA BUNGE LA NOVEMBA HAWAKU WASURPOT CHADEMA KABSA, LAMSINGI HAPA WASIMAME KAMA WAPINZANI NA WAPENDANE WOTE KWAPAMOJA WAWE KITU KIMOJA MBOWE AWAWEKE NA WAO ILIKAMBI IWE NA NGUVU ZAIDI WAWABANE HAWA MAFISADI CCM NIWAJANJA WANAWAKOROFISHA MNABAKI KUGOMBANA BUNGENI WANANCHI TUNA WAONA MNAVURUGU 2015 TUNACHAGUA CCM TENA KUMBUKENI SIKILA MTU ANAUELEWA WA JUU KIIVYO WAKUWAELEWA MNACHOKIFANYA NISAHIHI. SO YOU HAVE TO BE VERY CAREFUL YOU ALL WAPINZANI PENDANENI FASTA MUUNDE MAJESHI, TAMBUWENI WANANCHI TUMEAMUA KUWACHAGUA WAPINZANI KIPINDI HILKI COZ TUMEWACHOKA HAO MAFISADI WANAO TUNYONYA KWANJIA YAKUPULIZA WANAJICHEKESHA WANAJIDAI WAPOLE ILITUWAONE WEMA. NASEMA HIVI COZ KWAMAENEO NLIYOPO SASA TOKA TAR NANE MLUMBANE NAWASIKIA WATU WENGINE CHADEMA WANAJAZBA WENGINE CUF WAMENUNULIWA SIONI WAKILAUMU THOSE FISADIS MKICHEZA WENZENU WATATAKE ADVANTAGE YA TOFAUTI ZENU KUREKEBISHA MAPUNGUFU YAO. OOOH!!!!!!!! HV HAMUWAJUI CCM EEH! KAMAMNAKUMBUKA KUNA SIKU MAKAMBA ALISEMA MAJIMBO WALIYO CHUKUA WAPINZANI DAR WAMEWAKOPESHA WATAYARUDISHA TENA KASEMA KUNANJIA NYINGI ZA KUYARUDISHA EBU FIKIRIA KWA HALI YA KAWAIDA MFANO UBUNGO WANANCHI WANAVYOMPENDA MNYIKA BADO ASEME HIVYO HATA NA MDEE PIA OOH! KUWEN MACHO ONE MISTAKE ONE GOAL NANYIE CUF MSIFIKIRI CCM WANAWAPENDA ILA WAMEAMUA KUWAPIGA TAFU COZ ZENJ WASHAKATA TAMAA WANAJUA MTASHINDA NA WANA JUA KWABARA HAMUWEZ NA NDOKUNAWATU WENGI KWA KITI CHA URAIS HIVYO WANAWAGOMBANISHA ILI CHADEMA WAPITEZE MVUTO BAR 2015 WAENDELEE KUSHIKA DOLA. WITO WANGU KWENU CUF AND CHADEMA KWANINI MSIWAAIBISHE CCM 2015 KWAKUWA KITU KIMOJA ILI 2015 CUF MCHUKUE ZENJ AFU CHADEMA BARA? NALINAWEZEKANA KABISA THOSE FISADIS WAMELIGUNDUA HILO NDOMANA WAMEONA HAKUNANJIA NYINGINE YAKUJIKOMBO ZAIDI YA KUFANYA FITNA.

    ReplyDelete