03 February 2011

Kikwete mgeni rasmi Tamasha la Nyerere

Na Nayla Abdulla

RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la The Mwalimu Nyerere Film Festival, lililoandaliwa na Shirikiasho la Filamu
Tanzania (TAFF) ambalo litakalofanyika Februari 14 hadi 19 mwaka huu.

Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza, litaenda sambamba na uzinduzi wa shirikisho hilo ambalo litafanyika katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

Akizungumza Dares Salaam jana, Rais wa shirikisho hilo, Simon Mwakifwambwa alisema lengo kuu la kuanzishwa kwa tamasha hilo ni kukuza soko la kazi za filamu nchini na kukuza mahusiano ya kisekta kati ya wasanii na taasisi ya kibiashara za ndani na nje ya nchi.

Alisema tamasha hilo litafanyika sambamba na kumuenzi Hayati Mwalimu Nyerere, kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya filamu hapa nchini enzi za uhai wake.

Mwakifwamba alisema tamasha hilo litahudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo nyota wa filamu wa Afrika Kusini na Hollywood wakiwemo Diamond Eliot wa Nigeria, Marwa na Mama Kayayi wa Kenya.

Alisema zaidi ya filamu ishirini zilizofanya vizuri za ndani na nje ya Tanzania, zitaoneshwa katika tamasha hilo ambalo litasindikizwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma za asili, vichekesho, muziki wa dansi, taarabu, bongo fleva, pamoja na michezo ya asili.

Mwakifambwa alisema tamasha hilo litatanguliwa na mafunzo ambapo mada mbalimbali zinazohusu shughuli za filamu na maigizo zitatolewa na wakufunzi waliobobea kwenye fani za utunzi, uongozaji, uhariri na ufundishaji.

2 comments:

  1. Tunamtaka rais kwenye kongamano la kujadili mustakabali wa taifa letu na katiba mpya, sio kwenye matamasha ya ngoma za asili, vichekesho, muziki wa dansi, taarabu, bongo fleva, pamoja na michezo ya asili tu.

    Rais wetu ni wa kusherehesha tu! Mbona hachukulii maswala kwa uzito wake? Mbona hajatmbua maswaibu ya watanzania? JK sasa niwakati wakuongoza mabadiliko ya Tanzania tunayoitaka au kaa pembeni...

    ReplyDelete
  2. Chonde chonde Mr anonymous, najua nyie chadema mmezidi. Inaelekea Slaa amewapandikiza sumu mbaya ya kumchukia Kikwete. Nyie chadema mnadanganya umma kana kwamba matatizo ya Tanzania yanatokana na Kikwete. Matatizo ya kiuchumi na kisiasa yanaanzia tangu tulipopata uhuru, hayajaanza na Kikwete. Ufisadi, mikataba mibovu, madeni, umaskini, etc yameanzia huko nyuma.

    ReplyDelete