01 March 2011

Kikwete alia na CHADEMA

*Ahofia maandamano yao na mikutano inayoendelea mikoani
*Asema yanachochea ghasia kuiondoa serikali madarakani


Na Edmund Mihale

RAIS Jakaya Kikwete jana kwa mara ya kwanza amezungumzia maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanayoendelea
katika mikoa mbalimbali nchini kupinga gharama za maisha akiyaelezea kuwa yenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko na uvunjifu wa amani nchini.

Akilihutubia Taifa katika hotuba yake kila mwezi, Ikulu jana, Rais Kikwete alisema kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia. Lakini, kuigeuza fursa hiyo kuwa ni jukwaa la kuchochea ghasia na kwa nia ya kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa mabavu ni matumizi mabaya ya fursa hiyo.

"Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila miaka mitano tunafanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wetu. Uchaguzi wa mwisho tumefanya Oktoba 31, 2010. Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. Kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na haya wanayoyazungumza sasa.

"Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama Cha Mapinduzi (CCM). Iweje leo, miezi mitatu baadaye kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni.

"Siyo sawa hata kidogo, kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa serikali madarakani ni kinyume cha katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima.

"Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi," alisema Rais Kikwete.

Alisema katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, wanapomaliza uchaguzi mmoja, wanajiandaa kwa mwingine. Wanajenga upya chama chao, wanaongeza wanachama, wanaboresha sera na hoja zao pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali wao na kuwakataa wenzao.

Alisema uwanja muhimu wa kufanya hivyo ni sehemu ya bunge na halmashauri za wilaya kupitia wabunge na madiwani

Alisema kitendo kinachofanywa na Chadema cha kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ili waingie  ni kinyume na misingi ya demokrasia.

"Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima. Hebu fikirieni, kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani?

"Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida. Hatuitendei haki nchi yetu na hatuwatendei haki wananchi tunaodai tunawapenda na kuwatetea.

"Ndugu zetu wa CHADEMA wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo. Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka. Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri. Wanataka kutumia mabavu. Naomba tuyakatae mambo yao. Tusiwafuate. Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. Sisi katika serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao," alisema Rais Kikwete.

Akizungmuzia hali ya maisha ya Mtanzania, Rais Kikwete amekiri kuwa kwa sasa hali ni ngumu ya kimaisha, hivyo amewataka kukabiliana nayo.

Alisema kuwa serikali kwa upande wake imeelekeza nguvu na rasilimali zote na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali. hivyo kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, bali kikwazo kikubwa ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi nchini na hivyo uwezo siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo Watanzania wengi wanapenda iwe.

"Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa. Mzee Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. Wa wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri.

"Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa naye kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo.

"Hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa. Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.

"Lakini, pia ni muhimu watu kutambua ukweli kwamba uchumi kama wetu ambao haujajenga uwezo wake wa ndani wa kujitosheleza kwa mahitaji yake, huathirika sana na yale yanayotokea katika uchumi wa dunia. Unapoyumba na sisi tunayumba," alisema Rais Kikwete.

Alisema kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia zinasababisha gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda hivyo mfumuko wa bei ukipanda China, nguo na bidhaa zinazonunuliwa kutoka China hupanda navyo hupanda bei.

Hivi sasa mataifa yote makubwa mfumuko wa bei umepanda na kuathiri uchumi wa nchi, kukosekana kwa mvua nako kunasababisha uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula. Hivyo hivyo lawama kwa serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi? aliahoji.

Alisema hata hivyo serikali imekuwa ikitafuta ufumbuzi wa  matatizo yote kwa lengo la kutafuta unafuu kwa kiwango tunachowezekana ikiwemo kutoa unafuu wa kodi kama ilivyofanya kwa sukari na saruji pale. inapobidi.

Jana gazeti la serikali la Daily News lilimkariri Msajili wa Vyama vya Siasa, Bw. John Tendwa akisema kauli  zinazotolewa kwenye maandamano hayo za kumpa muda wa siku tisa Rais Kikwete kutekeleza mahitaji yao ni za kichochezi na zinaweza kuingizwa katika makosa ya uhaini kwa kuwa kinawachichea wananchi waichukie serikali yao.

Hali ya umeme

Akizungumuzia hali ya umeme nchini alisema hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni mbaya kutokana na kupungua kwa maji katika bwawa la Mtera ambayo juzi kina cha bwawa hilo kilishuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7 na kubaki mita 1.25 juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.

Alisema  Februari 15 , 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. hivyo baraza hilo liliitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi.

Alisema baraza hilo pia lilisisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. Pia, wahakikishe kuwa mkataba watakaoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa na watoa huduma wawe ni kampuni zinazofahamika na zenye sifa stahiki na kuaminika.

"Natambua kuwa Bodi na Mejemienti ya Shirika la Umeme, wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011," alisema Rais Kikwete.

Alisema kuwa mwaka 2006/7 serikali iliamua kupunguza kutegemea umeme wa nguvu ya maji kwa kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati.

Alisema mpango umetengenezwa na utekelezaji wake unaendelea na tayari umeme wa MW 145 wa kutokana na gesi asilia umeongezwa kwa kugharamiwa na serikali. na mwisho wa mwaka huu MW 160 zitaongezeka MW 100 Dar es Salaam na MW 60 Mwanza kwa gharama za serikali.

"Bahati mbaya kutokana na matatizo ya fedha ya kimataifa, wawekezaji wa sekta binafsi wa kuzalisha MW 300 za umeme wa gesi asilia pale Mtwara walijiondoa. Umeme huo ungekuwa tayari umeshaingizwa katika gridi ya taifa hivi sasa na kuondoa tatizo la sasa. Wawekezaji wengine wamepatikana na mazungumzo yanaendelea vizuri," alisema Rais Kikwete.

Alisema Mradi wa Kiwira umecheleweshwa na mchakato wa kubadili milki na kupata mkopo wa dola za Marekani milioni 400 za kuwezesha ujenzi wa kituo cha kuzalisha MW 200. Lakini suala la kubadili milki limefikia ukingoni na mchakato wa kupata mkopo unaendelea kwa matumaini.

Hali ya chakula nchini


Rais Kikwete tayari Halmashauri 36 za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara na Iringa imeripotiwa kuwa na upungufu mkubwa.

Alisema serikali imeidhinisha kutolewa kwa tani 13,760 za chakula kutoka Akiba ya Taifa ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kuhudumia watu 423,530 walioathiriwa na upungufu wa chakula katika maeneo hayo.

Alisema kazi ya usambazaji inaendelea. Hadi sasa jumla ya tani 4,822 za chakula cha msaada zimetolewa katika mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro na Lindi.

Fidia ya Gongolamboto


Alisema serikali imebeba jukumu la kujenga upya nyumba za wakazi wa eneo hilo kwa mujibu wa kiwango cha uharibifu.

"Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia Shirika lake la Uchumi. Nimeamua hivyo ili kuhakikisha kuwa maisha ya ndugu zetu waliokumbwa na maafa haya yanarejea kuwa ya kawaida mapema iwezekanavyo," alisema Rais Kikwete.

Alisema ameagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Taifa cha Maafa kuhakikisha kuwa utekelezaji unaanza mapema iwezekanavyo.

49 comments:

  1. watanzania tunachekesha!
    Ukiona leo hii wanaounga mkono chadema ndio hao walioipigia ccm. Ndiyo hao waliovaa fulana za njano na kanga. "Mmeyataka wenyewe mtanitambua"
    Ujinga huleta umasikini. Hata kama mnasema mmechakachua kura nyingi amepata kikwete kutoka kwa watu wajinga.
    Kwa kikwete:Wewe ndiye rais halali uliyechaguliwa na wananchi hakuna mwingine! Ila utambue kuwa the end does not justify the means,tatua matatizo ya umeme na rushwa upate utulivu kwani hakuna amani tanzania kama kuna umasikini.Kwa chadema: Mzunguko wenu usiwe na lengo la kuleta vita ila uwaelimishe watu wafahamu jinsi haki yao inavyoliwa na wachache,pili msione umati wa watu mijini mkazani mnajulikana. watu wanaochagua CCm ni wale wa vijijini zaidi wengi hata baiskeli hawaijui, ambao hawana umeme, bibi yangu hajui dowasa ila sukari, sabuni,kibiriti na mafuta ya taa. Piteni kuwaelimisha watu vijijini, fungueni matawi kila kukicha vijijini, ongezeni wanachama, fungueni kituo cha tv chadema na radio chadema kwa wanavijiji, waonesheni watu kuwa ninyi siyo waukanda, udini wala ukabila hapo ndipo mtakaposhinda, otherwise hata mkirudia uchaguzi as of now ambapo wanavijiji hawawafahamu dowasa, kikwete atashinda tena kwa asilimia zaidi ya 2010. So,Jitangazeni mfahamike nanyi mfaidi ikulu, sisi tupo tu kitaani hata mkiingia hatuwagusi bse african leaders! you are all pumbafuu, the difference is the same from north to south.

    ReplyDelete
  2. HAKIKA RAISI JK TUNAKUSHUKURU KWA BIDII ZAKO!! LAKINI KUHUSU HILI LA UMEME BADO TUNAONA KUNA KIZUNGUMKUTI AU WASHAURI WAKO NI MBUMBUMBU, MAANA KTK SAKATA LA DOWANS TULIKATAA KUNUNUWA MITAMBO YAO KWA BEI YA BILLION 106 ETI NI GHALI NA PIA SERIKALI HAIRUHUSU KUNUNUWA KITU KILICHOTUMIKA!!(procurement act)HIYO NI MWAKA 2008,SASA ZIKO WAPI HIZO MASHINE ZA BEI RAHISI? PILI TANESCO KUPITIA WAZIRI WA NISHATI ANADAI MITAMBO INACHUKUWA MWAKA MMOJA MPK KUFIKA HAPA SAWA JE, TOKEA WAKATI HUO ILIKUWA KUNA MIKAKATI GANI ILIYOFANYIKA? NA LEO TUNAKODI KWA DHARURA HIYO MITAMBO AMBAPO GHARAMA ZAIDI YA BILL 400 ZITALIPWA,JE, HATUPATI MITAMBO MIPYA MBONA KICHEFUCHEFU? HEBU WABANE HAO WASHAURI WAKO KWA KAULI ZAO NA PIA KUWA KWAKO KIMYA NA BARIDI NDIO TATIZO LA KILA MTU KUJIBU VYAKE ATAKAVYO NA PIA KUTUWEKA NJIA PANDA NA NDIO MAANA HATA WAPINZANI WANAPATA WAPI KWA KUKUBANIA NA KUKUDHALILISHA HIVI ILIKUWAJE RICHMOND WAKAWEZA
    KULETA MITAMBO NDANI YA MIEZI 2 SERIKALI ICHUKUWE MWAKA MMOJA? NA KUNA UBAYA GANI KUNUNUWA MITAMBO ILIYOTUMIKA WAKATI NI MIZIMA AMBAYO INAWEZA KUTUMIKA ZAIDI YA MIAKA 20 MBELE?VIPI HIZO NDEGE YA RAISI NA ZA ATC TULINUNUWA MPYA AU MITUMBA?SHERIA ILIRUHUSUJE?
    TUACHE SIASA NA KUTAFUTA TEN PARCENT

    ReplyDelete
  3. Hivi Kuimarisha Vyama vya siasa ( vya upinzania) kunafanywa kwa njia zipi?
    Je? hofu aliyonayo raisi kwa sasa inatokana na nini haswa? Mikutano kama hii inayoendelea sasa imekuwepo siku nyingi sana sasa wasi wasi unatoka wapi hadi kufikiri anatolewa madarakani kwa nguvu?

    ReplyDelete
  4. ni bahati mbaya kuwa watanzania weng hasa vjjn bado n mbumbumbu ndio maana rais zuzu kama kikwete anaendelea kutawala. chadema sambazen moto wa mapinduz popote il tumwondoe huyu laana na balaa anayeliangamiza taifa. sasa anatapatapa ili yasitokee ya misri lakin yote kwa chadema na nguvu za uma tunaweza

    ReplyDelete
  5. ni aibu kwa watanzania kumskiliza huyu pmb. maswala ya umeme na kupanda kwa gharama za maisha yote yanasababishwa na uzembe wa kilaza huyu pamoja na woga wake wa kukabiliana na mafsad ambao kihalsia ndio wanatawala kwa sasa.hamna demokrasia iliyomwingza kikwete madarakan ila n tume fsadi ya uchaguz ambayo ni vbaraka wa ccm na ofs ya msajl wa vyama vya siasa ni kimada wa ccm. tunataka demokrasia si domokrasia ya kikwete.tena aharakshe katba la sivyo uchaguz ujao ccm itakiona cha mtema kuni

    ReplyDelete
  6. kikwete ungekuwa na akl usingeendelea kuongea pumba ila ungechukua hatua za haraka kukabiliana na tatzo la umeme na gharama za maisha ambayo yote n uzembe wako la sivyo yatakupata ya ghadafi na mubaraki tena tutakunyonga kwan ni her ghadaf kulko wewe unatia aibu sasa

    ReplyDelete
  7. AMMA KWELI MAJINGA NA MAZUZU WAKO WENGI SANA HIVI KUTOA MAWAZO YAKO KWA BUSARA HUWEZI SI UKAE KIMYA? ADMIN NI BORA KUWAKANYA WATU KAMA HAWA HUWEZI KUMUITA RAISI WA NCHI KUWA NI ZUZU AU PMB HAWA NI WAJINGA TENA WAO NDIO PMB, KWANI ILIMRADI UTOE UTUMBO WAKO NDIO UONEKANE WEWE NI MCHANGIAJI AU NDIO SERA?ACHENI UJINGA HUO WEWE HUMTAKI HUMKUBALI LAKINI UJUWE KUNA TULIOMKUBALI NA KUMCHAGUWA ACHENI ULIMBUKENI

    ReplyDelete
  8. daima ndege wafananao huruka pamoja kwa hyo wewe unayemuunga mkono rais pimbi n zaid ya pmb. uhuru wa maoni hauna mipaka na matusi ni njia muafaka ya kufikisha ujumbe tena kwa ufanisi. pole sana kwa kuwa nitaendelea kumwita pmb rais wako na daima kumbuka panga litaendelea kuwa panga na kamwe halitaitwa kisu kwa kulazmisha kwako

    ReplyDelete
  9. alaaniwe milele rais huyu wa ajabu anayetawala nchi kama yuko kwenye mdundiko wa kizaramo. nadhan rais huyu anawaza midundko, miduara,kichen pati,sendoff,na safari za kujiuza marekani kulko hal ngumu ya maisha ya watanzania. sasa amezinduka baada ya kuona kinachoendelea misri na libya. ila pamoja nakuznduka hataeza kufanya lolote kwan kichwan hana jipya zaid ya midundko

    ReplyDelete
  10. Nashangaa, kwani Rais kweli anapewa taarifa feki, kwani katika hotuba yake hasa kuhusu hali ya chakula hakugusia hata wilaya moja katika Mkoa wa Kagera, hivi hajui kuwa kuna ugonjwa wa migomba wa mnyauko bakteria ulioshambulia zaidi ya theluthi mbili za migomba hasa wilaya za Misenyi, Bukoba Vijijini, Bukoba Mjini na Muleba? Hajui kuwa ndizi ndio chakula tegemezi kwa watu wa mkoa huu? Pia hajui kuwa mvua za vuli zilinyesha chini sana ya kiwango, kiasi kwamba maharage ambalo ni zao linalotegemewa na wengi lilipatikana kwa asilimia kama 10 au 20 tu. Nilitegemea sana pia wilaya tajwa zitajwe kama zinazohitaji sana msaada wa chakula kwenye hotuba yake. Kwa mengine hasa ya kuongopa CHADEMA najua ni hofu yake isiyo na msingi. Mbona hakugusia DOWANS na mfadhili wake mkuu anayemugopa Rostamu Hazizi?

    ReplyDelete
  11. KIKWETE acha KUWADANGANYA wananchi kwamba ati CHADEMA ni tatizo.... WOTE TUJAJUA : Tatizo siyo CDM bali ni CCM, MAFISADI, mgawo wa Umeme, kupanda kwa garama za maisha na hasa mfumko wa bei, Kuwadanganya wananchi kwamba watapata MAISHA BORA badala yake wakaambulia KASI MPYA ya maisha DUNI kwa kila Mtanzania,Elimu secondari na vyuo kushuka, Vijana hawana ajira, mikataba mibovu na rasilimali za Watanzania kuendelea kuibiwa na kutajirisha wachache. Ombwe la uongozi, safari za nje ya nchi za garama kubwa wakati wanachi wako kwenye umaskini wa-kutisha !!

    ONYO: Mambo yasipo badilika haraka, yale yaliyotokea TUNISIA, MISRI na sasa LIBYA lazima yatafika Tz.


    JUA KWAMBA : WATANZANIA na hasa Vijana HATUDANGANYIKI Tena NG'OOOOOOOO !!!! Tunazo akili tunajua mkombozi wetu ni CHADEMA ili rasilimali zetu zirudishwe mikononi mwa watanzania. .............Bai bai CCM !!!


    Laiti nengekuwa mwanamuziki ningemtungia KIKWETE wimbo huu :

    Presha hizo zinapanda, zinashuka, Kikwete, CCM, Mafisadi, Presha Juu !!

    KIKWETE + CCM + MAFISADI wakiisikia CHADEMA
    presha zinapanda ohhh Presha zinashuka eeeeeeeeehhhhheeeeeeee X2

    PRESHA, PRESHA, PRESHA x2 zinapanda ohhh eeeeeeeeeehhhhheeeeeeee X2

    Chadema chapa Kazi tupo wote !!!!!!!!!!!
    ccm Bai bai !!




    by Ali Abdallah

    ReplyDelete
  12. shehe yahya yuko wap sasa? labda majn yake yanaeza yakatatua matatzo ya umeme na gharama za maisha kwan yalijitahd sana kuwatsha watu wakati wa kampen na kwa kiasi kikubwa yalisaidia ushnd wa rais kikwete. sasa nadhan n wakati mwafaka wa kikwete kutumia majn ya shehe yahya kwan nch ina hal mbaya kulko wakat wa kampen. kaz kwako shehe mtukufu yahya. nadhan kwa msaada wa majn yako unaeza kuwa mshauri mzuri wa matatzo makubwa yanaloikumba taifa la umeme na gharama kubwa za maisha

    ReplyDelete
  13. hivi rais alitaka ninikwenye hotuba yake. binafsi sikumwelewa. ni kweli watu tulidhike hata kama maisha hayaeleweki. vitu vinapanda bei umeme hakuna anataka tutulie bila hata kuonyesha hatukubaliabiani n hali. Waziri wake ailiyejinadi kwa mbwembwe kwenye vyombo vya habari kwamba umeme tabu kwa heri hajaonekana hadi leo akitupa updates halafu watu wakae kimya tu. hii nchi si ya marobot. ni ya watu wenye uwelewa na mambo yanao wahusu. ninachomshauri raisi wetu ajikite kutimiza yale ambayo watu wanavalalamikia na si kujibu hoja ya za cdm. Lakini angalizo CDM andamaneni kwa kadili muwezavyo lakini msijaribu kutupeleka misri maana kwa sisi WATZ tunataka kupeleka mambo yetu kisomi na si kwa kuua ndugu zetu. BE PRACTICAL JK WE NEED ACTIONS AND NOT POLITICS NOW.

    ReplyDelete
  14. Ama kweli Kikwete sasa hata mimi nakushangaa, hivi hiyo hotuba uliandika mwenyewe ama uliandikiwa? pole sana, kama uliandikiwa na wewe ukaisoma tu bila kufikiri basi safari ya chama chako iko ukingoni, unadhani leo ni wakati sahihi wa kuendelea kuwadanganya watanzania? ama kweli tulichagua kiongozi! maana sioni kama wewe unaweza/unafaa kuiongoza Tanzania, hufai, wewe upo kwa ajili ya Matajiri, Mafisadi, ndio nduguzo, ndio maswahiba wako. Umeme, UMEME, toka 2002 mpaka leo bado tuna mgawo wa umeme! unazungumzia mitambo ya kukodi huzungumzii KUNUNUA ili iwe mali ya TAIFA. Hii janja yenu ili muingize makampuni yenu muendelee kuliibia taifa hili. OLE WENU, siku zaja ambazo mtalipa yote mnayoliibia taifa hili. UKOMBOZI WA TAIFA LETU UKO MBIONI KUFIKA, WALA HAUKO MBALI.

    ReplyDelete
  15. Penye ukweli tukubali watanzania wenzangu, CCM ina kasoro sawa na hata wao wamekiri kuwa chama chao hakijatekeleza mambo fulani ambayo watanzania wanahitaji na wanaendelea kufanya marekebisho na wananchi waliwapa ridhaa kuendelea kushikilia dola katika uchaguzi uliopita, matatizo hayaishi kwa mara moja hata katika familia yapo matatizo ambayo uzee unamkuta mtu hayajamaliza na kama CCM wameshindwa tuwang'oe kwa uchaguzi halali wa demokrasia.sasa chadema mbona hawataki kukubali makosa yao kuwa wanawachochea wananchi kuichukia serikali? hivi wanapotoa muda wenye masharti kwa rais kutekeleza madai ambayo hata wao hawawezi ina maana gani kama sio uchochezi?demokrasia yao iko wapi kama wao hawana uvumilivu.pamoja na kwamba nchi ina ufisadi hivi wao ni wasafi kama hawatumiwi na baadhi ya nchi au watu fulani kutaka kuingia madarakani? wawaeleze watanzania fedha wanazotumia katika mizunguko yao zinatoka kwa nani,watueleze vyanzo vya mapato yao, hii ni siasa bwana, tunawaomba mtujali walalahoi,mtuelimishe mpaka vijijini, hivi nchi hii na umaskini huu ukiingia mgogoro wa vita ya ndani walalahoi tutakwenda wapi,nimepata nafasi ya kuhudhuria moja ya mikutano ya chadema kanda ya ziwa ni kweli baadhi ya maneno yao yana uchochezi,ndugu zangu wachadema wananchi wanaendelea kuelimika vuteni suburi watawapa kura.hata hivyo tunajua kuwa mtandao huo ni wa Freemason kwa sababu hata kule Misri na Libya wanatumia alama ya vidole viwili ni mtandao ambao ni hatari kwa usalama duniani, watu hawa huwa wanajivika vazi la kondoo lakini ni mbwa Mwitu wanaopenda kulamba damu ya binadamu wenzao huku wakijificha eti wao ni wanademokrasia.

    ReplyDelete
  16. Hii nimeipenda :

    Presha hizo zinapanda, zinashuka, Kikwete, CCM, Mafisadi, Presha Juu !!

    KIKWETE + CCM + MAFISADI wakiisikia CHADEMA
    presha zinapanda ohhh Presha zinashuka eeeeeeeeehhhhheeeeeeee X2

    ReplyDelete
  17. wewe mbwa unayesema matatzo hayaishi unaimanisha nn haswa. kwamba tatzo la umeme haliez kuisha? au tatzo la mafsad ,haliez kuisha? ttzo la mikataba mibovu ya madn haliez kuisha? mbona kikwete na mafsad wenzake wanaendelea kuitafuna nchi na kuish maisha ya hal ya juu na magar ya kupindukia kwa ufahar huku wananch wa kawaida wakiteketea kwa umaskn. kama n matatzo waache anasa il tujue tuko kapu moja na si matatzo yatu afu wao wanadunda. hii sio haki kabisa

    ReplyDelete
  18. kikwete sasa ni wakati wa kumwita mume wako obama kwan siku zacko madarakani zinahesabika. kama alikusaidia vyandarua basi sidhan kama atashindwa kukulinda kijeshi. kama marekan itashndwa labda brown atakukumbuka kwan hata huyo n mpenz wako

    ReplyDelete
  19. KWA MWENDO HUU WA UHURU WA KUTOA MAONI TUNAJIPOTOSHA KWA KUTOA MATUSI KAMA HAYA NI AFADHALI SAFU HII YA MAONI NDUGU MHARIRI UKAIFUTA AU MPK UIPITIE MAANA NI HATARI PIA NI KUKOSA MAADILI MEMA NA HAKUNA NIDHAMU

    ReplyDelete
  20. Mheshimiwa kikwete acha woga. unachotakkiwa kufanya ni kuchukua hatua haraka kwani watanzania wamechoka na propaganda zako kila kukicha. Hata wana CCM wenzako sasa wanaelewa kwamba hata chama umegeuza mali ya famiria yako nafikiri ndivyo unavyotaka kuwafanya watanzania pia. Tumeamka na tunataka mabadililko sasa.Unaonekana huna hulka ya kusikiliza vilio vya wananchi wako. Mabomu mbagala fidia elfu 30000. Naona hazimo timamu.

    ReplyDelete
  21. Mtani wangu Mkwere alidhani urais ni ngomba ya mdundiko. Hawezi akalinganisha na mapambano aliyokuwa nayo mwasisi wa nchi kama Mtumishi wa Mungu Mwl. Nyerere. Yeye walikuwa wanatafuta wajenge Tanzania ya aina gani. Ndio maana licha ya Matatizo Kiwete na wenzake mlisoma bure.
    Tatizo la kiwete anadhani urais ni kama mtu na familia yake, anachofanya ama kusema kiwe kimetafitiwa na siyo kuandika kwa mawazo yake. Hii ndio sababu hotuba zake nyepesi mno, ni za majungu majungu tu.
    Hivi jaribu kujiuliza Hivi CHD ndio chanzo cha maisha magumu, mipango mibaya ya uchumi.
    Waswahili walisema ivumayo haidumu! Rais wetu mpendwa aliingia kama masiha na kila mtu kama mimi alishangilia sana.
    Oh kumbe tulikuwa hatumjui! Rais wangu tafuta washauri wazuri. Yupo Lipumba, Yupo Slaa, wapo maprofesa wazuri tu. Acha kung'ania jinsia ama dini ndio kigezo uchaguzi. Wacha Makatibu wakuu wakae hata miaka mitano. Wakusaidie kutekeleza sera.
    Natatakiwa USHINDI DHIDI YA MAFISADI

    ReplyDelete
  22. Mtanzania mwwenye akili timum hana sababu ya woga juu ya maandamano ya CHADEMA. Hivyo ndivyo ilivyo kwa kiongozi mwadilifu. kiongozi mzursi ni yule anayetumia upinzani kufuta makosa aliyoyafanya na hii ni kutatua kero za wananchi. Kikwete huna haja ya kulalamika kwani uko madarakani na wakati na nafasi nzuri ya kutumia rasiilimari tulizonazo kwa uangalifu mkubwa ili kutatua kero za wananchi wako. ukifanya hivyo hawa CHADEMA watapata wapi kero za kunadi kwa wananchi? Ukweli Kiwete(kikwete) huna dhamira ya dhati ya kuwasaidia wananchi ila kuwasaidia hao wezi wenzio akina Rost Hamu. tunazidi kuchoka ipo siku tutawapiga mawe uraiani. Nafikiri ndipo mtatuelewa kuwa tumewachoka.

    ReplyDelete
  23. kikwete anakiogopa kivuli chake mwenyewe! ndio gharama za kung'ang'ania uongozi ilihali hukuchaguliwa... la kwako hilo ! chadema kaza buti tupo pamoja!

    ReplyDelete
  24. USHAURI WA HAPO JUU KABISA NI BOMBA ILE MBAYA. NAMKUBALI ALIENDIKA NA NAMUNGA MKONO.
    MUNGI IBARIKI TANZANIA!!

    ReplyDelete
  25. kikwete na serikali yake hawana jipya la kuwaambia watanzania jamaa anakua na uoga juu ja chadema na maandamano wanayofanya mikoani na pia japo watanzania wote na waliopo vijijini kama wangeliweza kujua dowans ni nini make haitasaidia kumbuka ccm wanashinda zaidi vijijini jamani kama ikiwezekana tuwaelimishe vijijini na watu pia wahusishwe na siasa kumbukeni tunawachagua hawa watu watutetee ili tuwe na maisha bora kila mtanzania sio watu wachache tu...tuamke jamani.......ila kikwete acha kudanganya wananchi we kaupepete mdomo kwa majirani zako wa ivory cost wakati tanzania tuna tatizo kubwa we shauriyako kama kazi imekushinda sema wapewe wengine....mbuzi...!!!

    ReplyDelete
  26. Mheshimiwa rais
    angalia upepo huo waja kwa kasi ya kimbunga
    wahenga walisema TABASAMU HALIPONYI KIDONDA
    chadema wanatumia udhaifu wa serikali yako kupata umaaru wee huoni?
    sasa CHA KUOGOPA NI UOGA WENYEWE!
    haki ya nani mwaka huu shetani alaumiwe kwa stail hii ya uongozi kazi unayo mzee me sikutishii NYAU ila ukweli utabakia milele
    BADILISHA STAILI YA KUTAWALA

    ReplyDelete
  27. Ni kweli hali TZ si shwari, hasa ukizingatia kuwa Watanzania walio wengi hawana uhakika wa kuamka kesho! Hali inayosababishwa na mambo mengi; fikra za watawala, fikra za watawaliwa na matarajio yao, mwelekeo wa fikra na uchumi wa dunia nzima, kiwango cha ushiriki wa kila mmoja katika kukabili mambo yanayomkabili na hatimaye jamii na namna ya kupokeleka kwa jitihada hizo binafsi kunakofanywa na vyombo vya maamuzi, n.k Maamuzi mazito na magumu yanapaswa kuchukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuisababisha ndani ya CCM na Serikali ili kuinusuru hali hii na kurejesha matumaini ya wenye nchi (watanzania) yatakayoweza kujenga fikra za utaifa zaidi.

    Pengine twende basi pale Namtumbo kwa ndugu yangu "Vita" kurutubisha hata ile Uranium kwa lengo la kutokomeza kabisa tatizo la umeme, hata kwa dada yangu "Jane" kule Nakatuta kwenye maporomoko makubwa ya maji na ya kihistoria n.k hatimaye kuifanya nishati hii kuwa rahisi kwa kila mmoja hali itakayopelekea hata huduma na uzalishaji katika sekta mbalimbali kuwa rahisi.

    Maandamano hata kama ni haki yetu ya msingi, tunapaswa kuyaratibu vema ile yawe na dhima nzima ya kuelekeza namna ya kukabiliana na tatizo pale ambapo pamekuwa na mapungufu ya kifikra na kiutendaji ili yaweze kutuletea tija badala ya mtafaruku katika jamii yetu ambayo kwayo "amani na utulivu" ndizo nguzo kuu.

    Wana CCM, wakati wa utani, kejeli na mizaha, ushabiki kwa masuala nyeti na ya kitaifa si huu. Sasa ni wakati wa kujenga nchi kila mmoja kwa uwezo wake na katika nafasi aliyonayo. Ni wakati sasa wa wanachama kuondoa woga na kuwawajibisha watendaji na viongozi wa chama wazembe, waliokosa ubunifu, na wanaoshindwa hata kusimamia vema utekelezaji wa majukumu ya Serikali. Hizi si zama za "hewala bwana mkubwa...lolote utakalo na liwe" yatupasa kuwa suluhisho la tatizo na si sehemu ya tatizo.

    Wananchi yatupasa pia kuwa wachambuzi makini wa mwendendo wa siasa na viongozi wa vyama vya siasa nchini. Tupime nguvu ya hoja zao na msukumo wa hoja hizo ili tutambue utashi wao kisiasa. Isije ikawa "maji yakimwagika hayazoleki" kwa kukosa tu umakini wa uchambuzi wa mambo hayo endapo itatokea tumetumika kwa manufaa "yao". Itatugharimu hata uhai wa tulio wengi kuweka mambo sawa. Hayo wanayotuambia au hayo wanayotenda, kwa kiasi gani yanaleta tija kwa maisha yetu ya kila siku? Iwe ni upinzani au chama kilichopo madarakani, tusisite kushauri na kuonesha njia bora ya ukombozi wa maisha yetu.

    Mungu ibariki Tanzania!
    mpiganaji@gmail.com
    0767588600

    ReplyDelete
  28. Malumbano ya maneno hayatatufikisha mbali Watanzania ila kama alivyosema Mama wa Taifa Maria Nyerere kwa Wanachadema waliomtembelea nyumbani kwake ya kwamba Vyama vya Siasa vishirikiane kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya nchi yetu kwa pamoja. Kumsakama mtu mmoja na kutukana kwa matusi kutokana na baadhi ya wachangiaji na watoamaoni sidhani kama kutasaidia kubadilisha hali ya nchi yetu. Ni kweli ya kwamba hotuba ya Rais Kikwete haina jambo jipya: Je yale waliyoyasema Viongozi wa Chadema mbele ya Mama wa Taifa ni yapi mapya? Si yale yale yaliyowahi kusemwa na Hayati Baba wa Taifa? Mtanzania kuwaita Watanzania wenzake waishio vijijini eti ni mbumbumbu kwa kuwa wamemchagua Kikwete inanisikitisha na inatia fedhea. Napenda kusema kama alivyosema Nyerere Jr ya kwamba 2015 ikiwezekana wain`goe CCM kwa amani, hapo ndipo muda wa Kikwete kama rais utafikia mwisho. Kwa sasa tudumishe amani yetu.
    Sidhani binadamu anaweza kuwa mbuzi!!!!

    ReplyDelete
  29. Maji shingoni Mheshimiwa sana Rais Dk. Mwenyekiti Kikwete. Umekuwa mdhaifu kiasi cha kulalama hivyo. Sera zimekuishia na Chadema ndiyo wanaiongoza nchi sasa kwa taarifa yako.

    ReplyDelete
  30. Tayari Mubaraki na familia yake wamezuiliwa kusafiri nje ya nchi yao!!!!Ina maana lazima wajibu kwa yale waliotenda hakuna pa kukimbilia.Huku nako zikipita siku tisa mtu ataumbuka na wako wengi wa kujibu!!
    CCM wanafikiri hizi zama za kale kuwa ukiingi madarakani hata kwa kuiba yanaisha hadi miaka mitano.Sasa wanatapa tapa baada ya kuona tunisia wametupa mbinu mbadala ya kutosubiri miaka mitano.CHADEMA msihofu jipangeni kuleta mabadiliko ya kweli.kuna mtu kasema chadema haiko vijijini!!NOO hiyo ni propaganda kwani mbozi kusini,kigoma kaskazini ni mjini,watu wameamka kote

    ReplyDelete
  31. Hili ni funzo kwa watanzania kuwa wakati tunapofanya uchaguzi tusiangalie chama tu bali na mtu aliyepo katika chama hicho. Hebu ona Rais kiazi kama huyu JK mawazo yake yote yako kwenye ngoma na unyago kwa wakwere

    ReplyDelete
  32. Mimi sio mwanachama wa chama chochote lakini la kusikitika tu ni RUSHWA na Uchakachuaji wa Kura katika nchi yetu. Kwa hilo kwa kweli Tanzania hakuna ustaharabu. Napenda comments lakini mnapotoa comments ya matusi in maana ulikosa maadili mema katika maisha yako. Sidhani kama mtu aleyekuzwa vema anaweza kutoa matusi katika jamii. Jua Raisi naye ni mwanadamu na tatizo la tanzania ni tatizo la afrika nzima. Kwa ujumla Africa kuna shida kunahitaji mageuzi ya hali ya juu na hii itatokana na dhamira ya kweli kwa viongozi lakini cha ajabu mwafrika akishapata uongozi anasahau ya nyuma. Mhariri bana comments zenye matusi.

    ReplyDelete
  33. BINGWA WA KUTABASAM KUMBUKA TUMECHOKA AHADI YA PIPI KESHO KESHO ZE DAYS ARE NUMBERED BETER FOR 2STEP DOWN AS WELL REST IN PEACE CCM !!!!!!!!!!!!!!!!!!H

    ReplyDelete
  34. FAHAMU LUGHA YA MATUSI INATOKANA NA SHIDA ,DHIAKA YA MUDAMREFU WA RAISI MAGWIJI WA KUOA ,LIALI WATU WANA KUFA NJAA ASANTEH MHARIRI MAKE ZE AFRICA HOPE ALIVE USICHOSHWE NA VIBARAKA SISI HADI LEO VYUONI FEDHA ZA MIKOPO AZIJAFIKA SABABU FEZA ZA KULIPA DOWANS ZIPO NA KUENDEA NJE ZIPO TUMECHOKAAAAAA CHADEMA GO AHEAD NEVER TREMBLE FOR NONSENSE WANAVYUO TUPOPAMOJA NANYI WAONDOENI MANDULI WALIO SALIA

    ReplyDelete
  35. Wanachuo ni kweli mna haki ya kugombea haki zenu za msingi nk. Lakini kumbukeni ya kuwa wale wale wazazi wenu ndio wale wale wahangaikao na kuwafikisha hapo mlipo. Kabla ya Uhuru na hata baada ya uhuru wetu sisi tuliotangulia tulisoma kwa shida pengine kuliko hata za kwenu. Wazazi wetu ambao pengine ni bibi na babu zenu walihangaika. Japo kulikuwa na shida na matatizo mengi lakini matusi ya namna hii ya leo mimi sikuyasikia.. Jambo la kuoa linakujaje kwenye mchakato wa siasa. Kumbe unatazamia mkopo! wakati wetu hatukuwa na mikopo; jua ya kwamba mkopaji huomba mkopo na wala halazimishi kukopeshwa. Mkopeshaji anapokuwa na hali nzuri ya kukopesha basi atafanya hivyo! Vuta heri.

    ReplyDelete
  36. chonde chonde wtz wezangu mungu atatunusuru na balaa hili.....

    ReplyDelete
  37. WATANZANIA HII NDIYO SIASA, ALL CHADEMA IS DOING IS TO GAIN GROUND, NDO KAZI YA OPPOSITION PARTY. TATIZO HAWA VIONGOZI WAMEZOEA VYAMA MFU AMBAVYO VIKISHAPATA VITI VYAO VIWILI BUNGENI VINANYAMAZA NA KULA POSHO YA VIKAO,. HIVI NDIVYO SIASA ZENYE UPINZANI ZINAVYO TAKIWA, HATA OBAMA HAPA MAREKANI YALIMKUTA NOVEMBER MWAKA JANA. WATU WAELEWE THATS POLITICS,...

    ReplyDelete
  38. acha ujinga ww kaeni tu huko africa hamjui lolote tatizo wabongo mnajifanya mnajua hamna hata kimoja mnachojua unategemea hao chadema watawasaidia nn nyie sasa wanacho angaika ii?uchaguzi umeisha wasubiri 2015 wanaweza kuingia madarakai wakijitahidi kumbukeni kuwa sio hiyo chadema ya mboe na slaa hapana hiyo haina bao ujue kuwa katoliki watawapa kura zao walokole hawatawapa wajue hilo waislam ndiokabisa tena kampeni zitapigwa hata misikitini wajue hilo kutawaliwa na kafiri nimarufuku tena wakiroma ndio kabisa waliee tu watoa mada hapo juu nadhani mgetumia busara zaidi kuliko kumtukana raisi wako hata kama hukumchagua kwani mumewenu mboe na slaa wanamtambua itakuwa nyie vidampa?dugu gazeti la majira tunakuomba sana kuliko kuendeleza chuki miongoni mwa jamii yetu tunakumba sana habari yingine uwe unazichuja kumbuka kuwa matatizo yatakapo tokea hayata mkuta mtu mmoja hata we nafamilia yako mtaumia tu

    ReplyDelete
  39. Nakubalisana na msemaji mmoja kuwa tatizo sia Chadema, bali tatizo kubwa na hatari kwa Watanzania ni ccm.

    ReplyDelete
  40. we muhaya uliyeyoongelea zao la mgomba. huna hata haya. kagera ina mvua mwaka mzima, ardhi nzuri..mnategemea zao moja, unafikiri nini kitatokea? acheni uvivu..fanyeni kazi..limeni mazao mengi.

    ReplyDelete
  41. Mimi nadhani muheshimiwa alikosea sana kuilalamikia CHADEMA, yeye angeendelea kutatua matatizo ya wananchi wake,kwasababu kila jambo hupimwa kwa matendo, sasa hivi watanzania wengi wamechoka na hali ngumu ya maisha.Muheshimiwa mimi ningeomba ili uwashinde wapinzani tekeleza ahadi zako, wewe umetuahidi mengi 2005 ambayo hadi sasa hujayatekeleza na bado mwaka jana umeongeza ahadi, je utazitekeleza lini ili watanzania tukuamini? hata mtoto ukimdanganya kila siku kuwa kesho nitakuletea pipi usipomletea zaidi ya mara moja lazima akuchukie na kukuona kuwa wewe ni muongo.
    Mh! tunakuombea sana Baba,maana kazi iliyopo mbele yako ni kubwa,wananchi wako dhiki inaongezeka kila kukicha badala ya kupungua.

    ReplyDelete
  42. Usilie na CHADEMA lia na umasikini ulikithiri kwa wananchi wako unaowaongoza.

    ReplyDelete
  43. Aliyewaambia ccm kuwa wafanyabiashara wanaweza kuingia kwenye siasa nani? Wafanyabiashara mliowaingiza wamewachimbia kaburi. Hamtalikwepa. Wafanyabiashara ndio wafadhili wenu. Sasa mmeyaona. Ninachosema mimi hakuna kukodi mitambo ya kufua umeme. Tumechoka, tuko tayari kuchangishwa fedha zetu mifukoni tununue mitambo yetu wenyewe. Kodi zetu ndizo mnazokula na kuishi kama mko mbinguni. Kila mtz aoneshe uzalendo kwa kuchangia harammbee hii. Mh. JK itisha kikao tuje tupige harambee tununue mitambo yetu mipya. Mitambo ya kukodi ni ufisadi mkubwa zaidi. Tunawajua.

    Kama tumeacha mito tuliyo nayo kwa miaka yote hii, leo hii tunazungumzia mitambo ya kukodi ni kupungukiwa busara. Hivi ni kwa nini hatuna uchungu na nchi hii? Hivi mawaziri uliowachagua wakusaidie wanafanya nini? Mbona hawana msaada?

    Mh. JK nipo tayari kutoa mchango wa laki moja tununue majenereta yetu wenyewe na si nya kukodi. Mbona kuna watu wenye pesa ambao wakionwa wanaweza kuchangia fedha za kununua majenereta yanayoweza kuzalisha umeme wa kutosha?

    Ninawaomba watz tuitishe harambee ya kitaifa tutnunue majenereta yetu wenyewe maana haya ya kukodi yatatuweka pabaya. yataturudisha kwenye mijadala inayotupotezea muda kama hii inayoendelea. Kuonesha tuna uchungu tufanye hivyo.

    Aidha, kama JK hutafanya hivyo, CHADEMA chukua hiyo fursa; Ombeni wananchi tuchangie fedha za jenereta, zikishatosha mnunue majenereta na kuikabdhi serikali na hapo mtakuwa mekamilisha anguko lake.

    Hatutaki serikali goigoi, serikali isiyojua kuwa matatizo ya wananchi wake ndio hufanywa sera. Mbona ccm mna wataalamu mliobobea na sasa mnataka tuwafundishe siasa? JK nakutakia harambee njema.

    ReplyDelete
  44. ILLUMINATE KAZINI NDIO MAANA UNAONA MATUSI YAMETAWALA HATA MHARIRI WA HILI GAZETI NA MWENYE HILI GAZETI WOTE NI MEMBA WA HAO ILLUMINATE TAZAMA ALAMA ANAYOTUMIA JAY Z NA NDIO HIYO HIYO WANAYOITUMIA CHADEMA

    PILI PESA NDIO ZINAWAFIKISHA WATU KUABUDU SHETANI LAKINI YOTE YAMO NDANI YA MAANDIKO WANAOABUDU SDA NA KUISOMA BIBLIA YOTE WAKAULIZE KANISANI KWAO KAMA HAYA YANAYOTOKEA HAYAMO KWENYE BIBLIA NI LAZIMA YULE MWANAMKE ACHUKUE UTAWALA WA DUNIA NA KILA MAHALI ANA WATU WAKE WANAOMFANYIA KAZI NA KWA KUWA YEYE NI NUSU MPAGANI BASI NI LAZIMA KATIKA FUJO ZAKE DAMU IMWAGIKE.

    Kama mtu haamini tazama tu jazba walizonazo wachangiaji wao pamoja na matusi wanayoyatoa kwa kila awapingae hawa wana nguvu za ziada, na wanahemkwa chuki kweli kweli kwani ni kazi ya huyo aliyewatoma wanakuwa kama wamekunywa ulevi fulani hivi. Hivi niwaulize tangu tumepata uhuru si ni asilimia 11 tu ndio wanaotumia umeme, sasa hiyo ndio iwe sababu ya maandamano?

    Na kama wao wanapesa za kufanya maandamano nchi nzima kwanini wasitumie hizo pesa hata kupeleka miradi ya umeme wa solar kwenye majimbo yao? Kujenga vituo vya afya, kupeleka walimu na kumaliza matatizo ya wananchi badala ya kuandamana? Lengo lao ni kuleta machafuko na kamwe kwenye machafuko hakuna maendeleo! Wanataka machafuko ili watoto wa Illuminata wapate kuzaliwa maana wakinamama watabakwa na wafuasi wao na kujaza kizazi chake hapa duniani.

    Najua mtanitukana lakini siwashangai kwani ndio mtazidi kuonyesha ushahidi kwa wasiojua kuwa nyie ni wafuasi wa illuminate na ushahidi mwingine ni mapesa mnayopewa na Sabodo anayapata wapi kila siku? Biashara gani hiyo ya kutoa mabilioni msaada kila siku mbona hazionekani kwa macho hizo biashara zake?

    Kwa mwenye akili ya kuelewa na kufahamu atajua kuwa hii ni kazi ya yule ambaye yu nusu pagan na nusu ajifanya muumini!

    ReplyDelete
  45. Sijawahi, kutukana mtu, lakini wewe uliyeandika ujumbe hapo juu natamani nikutukane.

    Ukiona mtu anaingiza maswala ya IMANI kwenye SIASA huyo ameishiwa.

    Tunacho kiona wote, ni kwamba maisha ya mtanzania kwa sasa ni magumu, Elimu imeshuka, Umeme ni Tatizo, ufisadi uko juu. Nchi haieleweki kabisa. Haya ndo yanaonekana wazi.
    Swala la Imani hapa linatoka wapi. Kikwete ameshindwa kuongoza Nchi thats all.

    Sasa swala kuabudu Mungu ama shetani linatoka wapi?

    Nakushauri hayo mafundisho yako yapeleke Kanisani ama msikitini siyo kwenye maendeleo ya nchi.

    ReplyDelete
  46. g.o.kichere@gmail.comMarch 2, 2011 at 10:54 AM

    Wewe acha porojo zako kwa hiyo wewe ndiyo MZALENDO pekee unayo ya ona haya matatizo yanayotokea nhini kiasi ufikie hatua ya kumtukana MH.Raisi wa Jamhuri wewe unatofauti na mtu anaye mtukana BABA YAKE,PILI wewe ni mtovu wa nidhamu, Huna adabu nenda kwa wazazi wako wakufundishe kwanza kabla ulimwengu hauja fanya hivyo.WEWE UNA AGENDA YA SIRI NDANI YAKO.NAKUONYA CHUNGA MANENO YAKO NA KAULI ZAKO WALIOKUTUMA TUNAWAJUA,HAKI UNAYOITAFUTA SIO KWA JINSI HIYO.NA JUA MMEPIKWA NA MASON KISHA KUTAWANYWA KWA MATAIFA YOTE AMBAYO Either HAYAKUBALINI MOJA KWA MOJA NAO AU WANACHELESHA KUTEKELEZA MAMBO YAO,Wamefanikiwa kuondoa dola kazaa IRAQ,MISRI,Na wanaendelea na nchi nyingine sasa Chini ya usimamizi wa MAREKANI, WATANZANIA MSISHABIKIE MAMBO MSIYO YA JUA MTAKUJA KULIA NA MSIPATE MSAADA.

    ReplyDelete
  47. wewe wa mason ni punguan kama kikwete nadhan hata hyo mason huijui na umeikarir kwa shehe wako kwan hao ndio kabisa elimu imewapga mgongo na wamebak kuongea chuki na jazba zisizo na maana huku waumn wao wakiendelea kuwa mbumbumbu na mafukara wakkupndukia.v wakat wenzetu wakristo wanafungua vyuo kila kanda na huduma nyingne mishehe inaendelea kupga pumba.mm ni mwislam ila nachukia sana kuwa mwislam

    ReplyDelete
  48. Ninakumbuka kituko kimoja alichonisimulia rafiki yangu. Kulikuwa na kijana fulani aliyekuwa na ugonjwa wa akili lakini ukimwona huwezi kutambua ya kwamba ana kasoro fulani; huyu alikuwa kila akikutana na mtu huanza kumtukana kwa maneno mazito. Siku moja alikutana na kijana mwingine na kama ilivyo kuwa desturi yake akaanza kummwagia matusi hayo mazito; yule kijana naye bila ya kutafakari alianza kubadilishana matusi naye. Rafiki yangu aliniuliza je, kati ya hawa wawili nani ni mgonjwa? Nilimjibu wote wawili hawana tofauti. Majibizano ya matusi na maneno yasojenga hayatasaidia kutatua matatizo ya Watanzania. Iwe kumtukana rais, chama, dini, mtu binafsi hii haitatusaidia. Swala la muhimu ni watu kujituma na kuacha uvivu wa kukaa vijiweni na kula madawa na wale waliomo kazini waache kutumia muda wao kwa mambo yao. Wabunge wawakilishe mambo wanayotumwa na wananchi Bungeni ili serikali iweze kutekeleza. Kwa ujumla siwezi kusema ya kwamba hakuna jema lililotendeka nchini mwetu tangu tulipopata uhuru yapo mema na hata mengine hayakumalizika. Tanzania ya leo ni tofauti kabisa ya ile ya kabla ya uhuru. Tena tukumbuke ya kwamba kila kukicha kuna jipya litokealo. Nani alijua kuwa kutakuja UKIMWI? Tuacheni malumbano yasio na maana bali tushikamane tuijenge nchi yetu.

    ReplyDelete
  49. Pole sana tumekuzoea,leo unanini jipya,matusi kwako ni pumzi,Hakuna siku waona jema,Kilisiku wajipanga kumtukana Mh.Rais na leo unanini jipya ropoka tena uridhishe moyo wako ila kumbuka uo muda wa kufikiria matusi na kuandika humu laiti ungewaza mambo yako ya msingi ungekuwa mult -billioner elimika Mtu mwenye akili timamu hawasilishi hoja kama wewe.Nakukumbusha nitukane tena leo ufurahi.

    ReplyDelete