01 March 2011

Ajali yaua watano Dodoma

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

WATU watano akiwemo mtoto wa miaka mitatu wamekufa papo hapo baada ya basi walilokuwa wakisafiri kugongana na jingine dogo aina ya Coaster eneo la
Kizota mjini wa Dodoma.

Ajali hiyo ambayo ilitokea saa 6:20 ilihusisha basi la Allys lenye namba za usajili T 312 AUU lililokuwa likiendeshwa na Saidi Omar  likitokea Kahama kwenda Dar es Saalam liligongana na Coaster yenye
namba za usajili T896 BGH iliyokuwa ikiendeshwa na Ramadhani Shaabani likitokea Dodoma kwenda Mantoni-Itigi mkoani Singida.

Dereva wa Coaster, Bw. Shaabani ambaye alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo, alitaka kulipita lori lililokuwa mbele yake bila kujua kuwa basi hilo linakuja mbele yake.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Godfyrey Mtei alisema kuwa wamepokea maiti za watu watano ambao miongoni mwao yupo mtoto wa miaka mitatu na mwanamke mmoja.

Alisema kuwa pia walipokea majeruhi 34, kati yao wanawake 16 na wanaume 18; majeruhi 15 walikuwa wametibiwa na kuruhusiwahuku 19 wakiendelea na matibabu.

Miili ya marehemu ilikuwa haijatambuliwa hayajatambulika hivyo kutoa rai kwa wananchi ambao wanafahamu kuwa ndugu zao walikuwa wakisafiri na magari hayo kujitokeza na kuitambua.

Waliokuwa wamelazwa hadi jana ni pamoja na Geneviva Kaombwe (22) mkazi wa Maili Mbili, Nyamilembe Kabugumira (27) mkazi wa Bahi, Paskalina Emmanuel (22) mkazi wa Itigi, Happynes Roman (17) mkazi wa Miyuji, Naomi Mgondo (19) mkazi wa mkazi wa Area D na Veronica Festo (15) mkazi wa  Dar es Saalam.

Wengine ni Aziza Rajabu (20) mkazi wa Chang'ombe, Sara Lucas (18) mkazi wa Kikuyu, Lucy Augustino (38) mkazi wa Chinangali, Zaidina  Bakari (22) mkazi wa Nkhuhungu, Regina Makala (27) mkazi wa Shelui pamoja na Pastory Mnzunguru 934) mkazi wa Kigoma.

Alibainisha kuwa wengine ni pamoja na Rashidi Yasini (26) mkazi wa Chang'ombe, Birindwa Shaban (28) mkazi wa Kongwa, Estomy John (25) mkazi wa Kahama, Enock Martin (29) mkazi wa Dar es Saalam, Peter Michael (36) mkazi wa Mailimbili na Flora Michael (18) mkazi wa Kahama.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. James Msekelea ambaye alifika hospitalini hapo na kujionea majeruhi alisema kuwa wakati umefika kwa madereva kuwa waangalifu na kuzingatia sheria na kanuni za usalama barabarani.

No comments:

Post a Comment