02 March 2011

Rooney anusurika kibano FA

LONDON, England

KITUO cha televisheni cha Sky News cha Uingereza, kimesema kwamba mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney hatakumbwa na adhabu ya
utovu wa nidhamu kutokana na shutuma za kumpiga kwa kiwiko cha mkono kiungo wa Wigan, James McCarthy, kituo cha televisheni cha Sky News cha Uingereza kiliripoti juzi.

Katika mchezo huo Rooney alionekana kumpiga kwa kiwiko cha mkono kisogoni, McCarthy wakati wa kipindi cha kwanza cha mchezo ambao Manchester United iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, dhidi ya  Wigan uliofanyika Jumamosi.

Kosa hilo ndilo lililomlazimu mwamuzi, Mark Clattenburg kuamuru upigwe mpira wa adhabu na baadaye akakieleza Chama cha Mpira wa Miguu (FA) kwamba alifanya maamuzi sahihi jambo ambalo limekifanya chama hicho kushindwa kuchukua hatua za kinidhamu.

Hata hivyo kocha wa Wigan, Roberto Martinez anamshutumu vikali mwamuzi huyo kwa kushindwa kumuadhibu Rooney siku hiyo ya Jumamosi.

"Nadhani Rooney ana bahati sana. Ilikuwa apewe kadi nyekundu," alisema Martinez. "Nililiona wazi tukio hilo na mwamuzi alifanya hivyo kwa sababu alitoa mpira wa adhabu.

"Mwamuzi anapoamuru upigwe mpira wa adhabu inadhihirisha wazi ilistahili kutolewa kadi nyekundu, huku akisisitiza kwamba ukiangali mkanda wa video unaonesha wazi Rooney alimpiga kwa kiwiko James McCarthy," alisema.

Hata hivyo kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson anadhani mwamuzi Clattenburg alikuwa sahihi kutomuadhibu Rooney na akasema ana wasiwasi atakuwa akiwindwa na vyombo vya habari vya Uingereza.

No comments:

Post a Comment