11 January 2011

Mabomu yarindima kutawanya wanafunzi UDOM

Na Waandishi Wetu, Dodoma

POLISI mjini Dodoma jana walilazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya wanafunzi na wahadhiri wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) walipojaribu kuandamana kwenda Ofisi ya waziri Mkuu kufikisha malalamiko yao.Jeshi
hilo lililazimika kufyatua mabomu ya machozi ambayo yaliwatawanya wanafunzi hao waliokuwa katika eneo la chuo hicho na kuwafanya kukimbia kila mmoja na njia yake kuelekea mjini kati na kukusanyika katika uwanja wa Nyerere Squire  na baadaye kufikia muafaka na  polisi kuwa wakiwa katika uwanja huo, wawe watulivu na wafikishe madai yao kwa Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini  bila kufanya vurugu.

Miongoni mwa malalamiko ya wanafunzi hao ni mikopo ambapo  baadhi ya wanafunzi ambao walikuwa wapatiwe Desema 6 mwaka jana  lakini hadi sasa hawajapatiwa na wanapofuatilia wanaelezwa kuwa mchakato bado unaendelea.

Madai mengine ni pamoja na  uhaba wa maji na hali ya uchafu wa mazingira chuoni hapo lakini pia wakishinikiza kuwa hawamtaki naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Shaaban  Mlacha.

Hata hivyo wanafunzi hao waliendelea kuimba katika eneo hilo huku wakiwafukuza waandishi wa habari kwa madai kuwa kituo kimojawapo cha televisheni kiliwahi kuchakachua habari zao hali ambayo ilisababisha  baadhi ya waandishi kupigwa.

Mmoja wa waandishi wa habari aliyepigwa na wanafunzi hao akiwa kazini eneo la  UDOM ni Bw. Haberi Chidawaliwa gazeti la  Mwananchi ambaye mbali ya kujieleza kuwa yeye si mwandishi wa kituo hicho cha televisheni na kuonesha kitambulisho alishambuliwa huku wakitaka kumnyang’anya kamera yake.

Mbali ya mtafaruku huo wa wanafunzi, wahadhiri nao wamekuwa  wakilalamika kutaka  hali bora.

Katika tamko la wahadhiri hao lililotolewa na Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wafanyakazi Wanataaluma chuoni hapo (UDOMASA), Bw. Paul Loisulie lilieleza kuwa uongozi umefanya jitihada kubwa kufuatilia utatuzi wa matatizo  yao bila mafanikio na  uongozi wa UDOM hauyajali madai yao hali ambayo imewalazimu kumtaka Rais aingile kati suala hilo.

Taarifa ya mwenyekiti huyo inasema kuwa kwa kuwa Menejimenti ya UDOM hadi wanataaluma hao wanakwenda kwenye mkutano,  haikuwa tayari kushughulikia matatizo hayo na mkutano mkuu wa nne wa UDOMASA wa Januari 8 mwaka huu ulilazimu kumwomba Rais  Kikwete kuingilia suala hilo.

Wahadhiri hao nao wameamua kuendelea kufanya mikutano  mpaka hapo matatizo yao  yatakapopatiwa ufumbuzi.Moja ya matatizo yanayolalamikiwa na wafanyakazi hao ni  malipo ambapo wanasema hawajapata mishahara mipya tangu ilipotangazwa Julai mwaka jana ya ongezeko la asilimia 20-30.

Pia  yapo madai kuwa Hazina imekuwa ikilipa mishahara ya juu ngazi  husika  lakini Menejimenti ya UDOM inapunguza kwa visingizio mbalimbali hali inayoaathiri uchagiaji wa wanataaluma hao katika  mifuko ya  jamii ikiwemo NSSF, LAPF,PPFna PSPF.

6 comments:

  1. Mwisho wa kuchagua rais kabila dogo na maendeleo hawajui ni kitu gani. Wao maendeleo ni kurogana basi. Mnaanzisha chuo kwa mbwembwe kumbe hamna uwezo wa kukitunza, hata maji, vyoo?????? Nakubaliana na Mkono mmeshindwa shule yake tena secondary!!!! Ndio matunda ya ufisadi CCM. Siasa mpaka vyuoni ili kuiba tu. Mkwere hata ili unahitaji mwekezaji? Na polisi badala kwenda kigoma kuwinda majambazi yanayoteka mabasi yanakalia kutimua wasomi. Ndo maana mnalala kwenye mbavu za mbwa.

    ReplyDelete
  2. pETRO eUSEBIUS mSELEWAJanuary 11, 2011 at 8:56 AM

    Mambo haya yote ya utumiaji wa FFU kama ndio hotuba ya kujibu malalamiko ya wananchi yana mwisho wake.Muda si mrefu.Subira yavuta heri!

    ReplyDelete
  3. Na hapa nap[o mlipata habari za Kiintelijensia. Mabomu ya nini sasa.

    ReplyDelete
  4. mh.....at least UDSM hali shwari

    ReplyDelete
  5. Kabila dogo ndilo limenusuru Tanzania - Nyerere,Mkapa,Mwinyi...Twakumbuka enzi ya kikoloni na ya Mangi Mkuu huko Moshi aliyetawazwa na mkoloni huyo huyo. Mangi Mkuu huyo Thomas Mareale angeshika usukani leo Tanzania ingelikuwa Afghanistan. Na mpaka leo hao mababe wanaona kwamba wao ndiyo wenye haki ya kuitawala Tanzania; bado wana fikra hizo hizo duni! Mbadilishe fikra hiyo na kuishi na wenzenu vizuri, kama walio wengi maradufu kuliko nyingi huko Mwanza. Watanzania kila wakati watawachagua viongozi wanyenyekevu, wenye uzalendo, ambao hawana dosari za kikabila. Baada ya Kikwete twaenda kusini au magharibi au kati au maeneo ya ziwa Victoria. Mtasubiri hata ufike wakati wa Bwana kurejea.

    ReplyDelete
  6. nyiewenyewe mnaosemasema yanamwisho wake mnamwisho wenu mtauona sisi wenye nchi tunawaangalieni tu mtakapo tuchosha tutawaomba kwa amani mtupe nchi yetu ushauri wangu ni wabure tunawaomba kwa heshima na taadhima tunaanza kuwachoka sasa kelelezenu hatutaweza zivumilia tena mmechoka na nchi yenu ingawa kisheria nyi mnaishi tu lkn wenye nchi hiyo wapo kimya wanawaangalia mchafuane mwisho wa siku hata chooni mtapaona mbali wahurumieni mama zenu na watoto maana nyie mliopewa midomo ya kuchonga hamyaoni hayo

    ReplyDelete