26 January 2011

Kompany amtabiria makubwa Dzeko

LONDON, Uingereza

MCHEZAJI Vincent Kompany, amesema anaamini kuwa mshambuliaji mpya wa Manchester City, aliyesainiwa kwa ada ya pauni milioni 27
Edin Dzeko, atapata mafanikio.

Huku Darren Bent akianza vizuri katika timu ya Aston Villa kwa kufunga goli dhidi ya City Jumamosi, tayari kumeanza kuwepo hali ya kumtazama
Dzek,o baada ya kushindwa kufunga katika mechi zake mbili za mwanzo.

Lakini Kompany, anaamini kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Wolfsburg, atakuwa miongoni mwa wafungaji karibuni. Beki huyo wa kati alisema: "Edin hataathirika kwa hilo.

"Hutokea washambuliaji kukosa kufunga magoli na walinzi kuruhusu magoli kuingia kwao.

"Edin amecheza kwa muda mrefu  Ujerumani na ana uchezaji wa Kijerumani, ina maana anatakiwa kufanya kazi kubwa kubadilika.

"Ligi ya Bundesliga ni tofauti kabisa. Hawezi kulinganishwa kutokana na kutumika nguvu na kasi katika Ligi Kuu. Ni ligi  tofauti katika Ulaya."

Kompany aliwahi kucheza miaka miwili  Ujerumani katika timu ya Hamburg, kabla ya kujiunga na Eastlands ili kuleta mapinduzi.

Alisema anatarajia kumuona
mchezaji huyo akibadilika katika uchezaji wake siku za baadaye.

Aliongeza kuwa tayari ameona dalili nzuri kwake kwa kuanza kuzoea uchezaji, lakini kitu rahisi sana kwa kuwa ameanza kumchezesha katikati ya msimu.

No comments:

Post a Comment