27 January 2011

Adebayor kukipiga kwa mkopo Real Madrid

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Manchester City,  Emmanuel Adebayor anajiandaa kujiunga Real Madrid kwa mkopo, baada ya klabu hiyo ya Hispania kutangaza
makubaliano yamefikiwa wakati ukitafutwa uwezekano wa kusajiliwa kwa mkataba wa kudumu katika ya majira ya joto.

Suala ya la vipimo kuhusu mchezaji huyo, lilitarajiwa kufanyika jana mjini Madrid kabla ya mkataba huo kusainiwa na endapo vinara hao wa ligi ya Primera Liga, wataamua kumnunua mwishoni mwa msimu huu ada yake itakuwa ni pauni milioni 18.

Ripoti zinaeleza kwamba kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho anajivunia kumsainisha mshambuliaji huyo kutokana na mshambuliaji wake, Gonzalo Higuain kuwa majeruhi huku Karim Benzema akiwa ameshindwa kuonesha kiwango chake.

Taarifa iliyotumwa katika tovuti ya klabu hiyo ilisomeka kwamba: "Real Madrid na Manchester City wamefikia makubaliano ambayo itashuhudiwa Emmanuel Adebayor, akicheza kwa mkopo kwenye klabu yake ya zamani.

"Mchezaji atabaki Real Madrid hadi mwishoni mwa msimu huu, wakati klabu ikiangalia uwezekano wa kumnunua," iliongeza taarifa hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu ya Hamburg, kuiwekea ngumu klabu hiyo ya Bernabeu kumrejesha mchezaji wake wa zamani. Ruud van Nistelrooy mapema mwezi huu na Real ndipo ikaamua kuelekeza nguvu zake kwa mchezaji asiyefanya vizuri Manchester City, Adebayor ambaye anatimiza miaka 27 mwishoni mwa mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment