02 December 2010

Yanga yamsajili Kijiko wa JKT Ruvu

Na Elizabeth Mayemba

UONGOZI wa Yanga, umewaongeza wachezaji wawili katika dirisha dogo la usajili lililofungwa juzi, kwa ajili ya kuongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji.Wachezaji waliosajiliwa katika usajili huo ni Mzambia Davies Mwape na
Juma Seif 'Kijiko', aliyekuwa akiichezea JKT Ruvu, pia aliwahi kukipiga katika timu ya Kagera Sugar.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana ndani ya Yanga, zilieleza kuwa uongozi wa klabu hiyo ulimalizana na wachezaji hao juzi jioni, hivyo tayari majina hayo wameshayapeleka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

"Ni kweli juzi jioni tumekamilisha usajili wa wachezaji hao, na huyu Juma Seif anamudu kucheza nafasi ya kiungo na Mwape ni mshambuliaji," alisema mmoja wa viongozi wa Yanga.

Alisema Wakongo waliokuja nchini ambao walitokea Kenya, hawajasajiliwa hivyo wakati wowote kuanzia sasa watarejea kwao.

No comments:

Post a Comment