ROME, Italia
WACHEZAJI wa Ligi Kuu ya soka ya Italia maarufu kama Serie A, wameleta mgogoro baada Chama cha Wachezaji Italia (AIC) kuitisha mgomo utaofanyikaa Desemba 11 na 12, mwaka huu.Mgomo huyo umekuja baada ya kuwepo mazungumzo kati ya
AIC na waendeshaji wa ligi, wakitaka kurekebishwa baadhi ya mambo na kushindwa kukubaliana Jumanne.
Awali mgomo huo ulipangwa kufanyika Septemba, lakini uliahirishwa na mazungumzo kuelezwa kuwa yanaendelea, lakini uamuzi wa mwisho utaathiri baadhi ya mechi za Serie A, ambazo zitaangukia wikiendi hiyo.
"Kwa upande wetu kulikuwa na nia ya uwezekano, tulifikiri kungekuwepo makubaliano lakini, hakuna makubaliano yaliyofikiwa. Mgomo umepitishwa kufanyika Desemba 11-12," alisema Makamu Rais wa AIC, Leonardo Grosso.
Mechi kati ya Juventus na Lazio, zitaweza kuathirika kutokana na uamuzi huo, wakati Inter Milan, AC Milan na Roma nazo zina mechi katika wiki hiyo ya mgomo.
Rais wa Serie A, Maurizio Berretta alilaumu uamuzi wa chama hicho akiuelezea kuwa si uwanjibikaji na ni wa hatari.
"Mkutano wa leo (jana), haukuwa wa kawaida, haukuwahi kuwepo katika historia," Berretta alisema.
"Chama kiligoma kusikiliza maoni ya Rais wa shirikisho, ikiwemo suala la wachezaji walio nje ya vikosi.
"Tumeingia katika hatari na mauaji mageni. Mgomo wa wanasoka ni uamuzi wa kutowajibika na hauna msingi."
Mgomo huo umekuja wiki moja baada ya kufanyika mgomo wa waamuzi wa Ligi ya Scotland, wakipinga baadhi ya mambo wanayofanyiwa waamuzi na klabu.
No comments:
Post a Comment