29 December 2010

Yanga, African Lyon hakuna mbabe

Na Addolph Bruno

TIMU za vijana za soka za klabu zinazoshiriki Ligi Kuu za Yanga na African Lyon wenye umri chini ya miaka 17, jana zilitoka suluhu katika mfululizo wa mechi za mashindano ya Kombe la Uhai, iliyofanyika asubuhi katika Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa ni wa kundi B wa mashindano hayo, yaliyoanza kufanyika juzi katika uwanja huo.

Katika mchezo huo, timu hizo zilishambuliana kwa zamu, ambapo katika dakika ya tatu, Yanga nusura ipate bao la kuongoza lakini Atupele Green, alishindwa kuuweka mpira kimiani.

Kipindi cha pili, kila timu iliingia uwanjani kwa nia ya kutaka kupata mabao, lakini hata hivyo milango kwa pande zote ilikuwa migumu.

Yanga kwa kuona ililazimika kumtoa Deo Magige na kumwingiza Emanuel Anganile ambaye hata hivyo hakuweza kuisaidia timu yake kupta bao.

Mara baada ya mchezo kumalizika kocha wa Yanga, Keneth Mkapa alisema safu yake ya ushambuliaji ilikosa umakini wa kufunga mabao, jambo ambalo atalifanyia kazi ili waweze kufanya vizuri michezo inayofuata.

Naye kocha wa African Lyon, Ramadhan Aluko alisema ameona matatizo ya kikosi chake katika safu mbalimbali, hasa ya ushambuliaji na kuahidi kuyafanyia marekebisho.

No comments:

Post a Comment