29 December 2010

Momba amnyuka Mashali kwa pointi

Na Amina Athumani

BONDIA Said Momba, juzi alimtwanga kwa pointi Charles Mashali katika pambano lisilo la ubingwa lililofanyika katika Ukumbi wa Manzese Texas, Dar es Salaam.Pambano hilo ambalo lilikuwa ni la raundi 6, liliandaliwa na Rama Jah na
kusimamiwa na Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST).

Momba aliibuka bingwa katika pambano hilo, baada ya kumsukumia makonde mazito Mashali ambaye alidondoka mara mbili katika raundi ya pili na ya tano.

Hata hivyo mwamuzi wa pambano hilo, Charles Mlundwa alilazimika kusimamisha pambano katika raundi ya tano, baada ya mashabiki kuanza kuleta fujo na kuamua kutoa ushindi kwa Momba.

katika mapambano mengine ya utangulizi bondia, Audiface Augustino alimchapa Abdallah Kitete kwa pointi 39-37 uzani wa light flyweight, huku Miraji Ally wakitoka sare na Issa Selemani kwa pointi 39-39.

katika pambano lingine Hussein Daud alimchapa Abdul Makawashi, katika raundi ya kwanza ya pambano la raundi nne uzito wa bantamu, huku fabian Lyimo akimshinda Fadhil Awadh kwa pointi 38-37.

No comments:

Post a Comment