31 December 2010

Wanasheria wajipanga kupinga Dowans

Na John Daniel

SAKATA ya malipo ya mabilioni ya walipa kodi kwa Kampuni ya Dowans limeingia katika hatua mpya baada ya jopo la wanasheria kuungana na kuanza kupitia vifungu vya sheria kwa lengo la kupinga hukumu hiyo iwapo itasajiliwa katika
Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hoja ya wanasheria hao ni ya nne katika kupinga kile kinachotwa kuwa ni hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara ICC tangu kuibuka kwa madai hayo.

Hoja nyingine zilizowahi kutolewa ni uhalali wa kampuni husika ambayo inaelezwa kuwa ni hewa na wamiliki wake hawajulikani, uhalali wa kiasi kilichotajwa kuwa ni sh. bilioni 185 huku taarifa nyingine zikionesha kuwa ni dola milioni 64.2 karibu sawa na sh. bilioni 90 za Tanzania.

Hoja nyingine ni uhalali wa madai hayo kutangazwa kabla ya hukumu ya usuluhishi kusajiliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kama inavyotakiwa kisheria, hali iliyosababsiha wananchi kuhusisha madai hayo na mbinu chafu za kifisadi.

Wakizungumza na Majira jana kwa sharti ya kutotajwa wala ofisi zao kwa madai kuwa itavuruga maandalizi yao, wanasehria hao walisema serikali ina nafasi kubwa kisheria kukwepa kulipa madai hayo kupitia Mahakama Kuu."Tayari kazi ya kupitia vifungu kadhaa vya sheria kuokoa nchi yetu na malipo haramu ya Dowans imeanza, tunasubiri tu wasajili tu maamuzi ya usuluhishi ili tuanze kazi.

Hadi sasa hatuna anayegharamia lakini tutajitolea kuonesha uzalendo wetu," alisema mtoa habari wetu.Wanasheria hao walisema hadi sasa kuna mambo makubwa manne yanayowapa uhakika kuwa suala hilo bado ni nyepesi kusitishwa kupitia Mahakama Kuu ya Tanzania.

Walitaja mambo hayo kuwa ni pamoja na uhalali wa Kampuni iliyouzwa kwa Dowans ya Richmond ambayo Kamati ya Bunge ilithibitisha pasipo shaka kuwa ni feki na haipo, hivyo kulazimu kuvunjwa kwa mkataba huo.

Sababu ya pili kwa mujibu wa wanasheria hao ni kifungu cha sheria kinachooruhusu madai dhidi ya mdai, (Counter Claim) inayohusisha Dowans na madai mbalimbali ya kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).Walisema kwa mujibu wa sheria hiyo, bado serikali inaweza kuomba tuzo hiyo kusikilizwa upya kwa kuwa kilichofanyika ni usuluhishi na si maamuzi ya Mahakama ya Rufaa.

Sababu nyingine ni kifungu cha 15 ya sheria za usuluhishi wa migogoro ya kibiashara za Tanzania kutoa haki kwa Mahakama Kuu kusitisha tuzo hiyo iwapo upande wowote utakuwa umekosea taratibu zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine wanasheria hao wamezidi kumkalia kohoni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, na kuhoji jinsi alivyoweza kupitia na kutoa maamuzi ya haraka kuhusu malipo ya Dowans.Walisema yapo majalada mengi yanayosubiri maoni au maamuzi ya Jaji Werema lakini bado hajafanyiwa kazi.

"Lakini pia tuna shaka ni kwa nini Mwanasheria Mkuu wa Serikali apitie jalada hilo haraka na kutoa jibu kwa muda mfupi hata kabla ya tuzo kusajiliwa Mahakama Kuu."Yeye mwanasheria Mkuu ana majalada mengi yanayosubiri ushauri au maamuzi yake lakini hayajafanyiwa kazi, inakuwaje hii akaishughulikia haraka na kutoa jibu jepesi kiasi hicho?" alihoji mwansheria mwingine.Kwa mujibu wa sheria namba 15 ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara nchini ambayo Majira inayo nakala yake Mahakama Kuu ina mamlaka ya kusitisha malipo ya tuzo hiyo na kutoa nafasi kwa mdaiwa kuendelea na utaratibu mwingine wa kisheria.

Majira ilipofika Mahakama Kuu kujua iwapo Dowans imesajili hukumu hiyo ya ICC ili kutoa nafasi kwa hatua nyingine, Msajili wa Mahakama Kuu, Bw. Ignas Kitusi alisema hawajapokea tuzo hiyo.Alipoulizwa iwapo taratibu za Mahakama Kuu zinaruhusu mwanya kwa hukumu hiyo kusikilizwa upya alisema hawezi kuzungumzia suala la kisheria ambalo halipo na kuweka wazi kuwa wanashangaa wanaojadili kitu ambacho hakipo.

"Sisi kisheria bado hatuna hata habari na hiyo tuzo ya Dowans maana hautujaipata, hatuwezi kuzungumza kitu ambacho hakipo, sheria haibahatishi," alisema.

16 comments:

  1. Afadhali jamani saidieni maana tutakoma japo mimi sikupigia wala kuhudhuria kampeni za CCM.

    ReplyDelete
  2. Great wananchi. Waliodhani Tanzania itaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu wakome! Watanzania wasomi watafanya kazi. Je, inawezekana hao mafisadi waliwapa mshiko mawakili wa Tanesco kusudi wasiwasilishe hoja zenye nguvu ili tushindwe? Naamini inawezekana na tunapaswa tujue hoja walizotoa ambazo wasuluhishi waliona hazina nguvu! Hizi siyo fedha kidogo, na mwenye kulipwa tumjue. Mwanasheria Mkuu kaanza ulaji naye? Mbona anamtetea mhindi eti yeye ni "mwakilishi tu wa kisheria"? Ana agenda gani?

    ReplyDelete
  3. Tusiingize siasa hapa,hili ni suala la sheria,wasiwasi wangu isijekuwa na hao mawakili nao ni dili ili nao wamwagiwe ulaji. NCHI HII MPAKA HAPO TUTAPOACHA KUNYOOSHEANA VIDOLE KWA KUWAHADAA WANANCHI NDIPO TUTAKAPO KOMBOKA. SIMUAMINI YEYOTE MAANA TABIA ZA MAWAKILI WA NCHI YETU INATISHA SANA NI WALAFI,MAKATILI NA WASIO NA HURUMA KAMA HAO WALIOCHEZA DILI HIYO YA DOWANS. NAULIZA TENA HAWA MAWAKILI WANA NIA YA DHATI AMA NI DILI HII?

    ReplyDelete
  4. Dowans ni mali ya wahuni wachache mafisadi wa nchi hii ambao wanajiandaa kuchukua nchi 2015. Kaeni chocjo wananchi mtakamuliwa mpaka mtoke damu. Tatizo la baadhi ya watu hawajui madhila ya CCM kila uchao hawaachi kuwasifu CCM na kuwapigia kura kwa vitu vodogo tu kama khanga, nguo, chakula na posho kidogo. Jamani wananchi tubadilike na tuipige chini CCM haifai hata kwa kulumangia

    ReplyDelete
  5. Nachukua nafasi kuwapongeza hao mawakiri wenye nia ya kujitolea kwa jambo walilo lisomea huu ni uzalendo ambao umetoweka Tanzania ya leo. Tujue historia ita tuhukumu wasomi tunao wahujumu watanzania masikini, wanyonge na wengi wasio na elimu (kama mtu anaweza kupiga kula baada ya kupewa kofia,tisheti na soda nakusahau gharama ya unga na sukari huyu mtu anataka msaada) Ikiwezekana ifunguliwe akaunti ya harambee kuwa saidia mawakiri hao waweze kusimamisha nia chafu ya mafisadi. Haiwezekani pesa ya kujenga barabara ya rami tangu Manyoni hadi Tabora ichukuliwe na wahuni. Huyu Wereme kusoma hukumu yenye kutia taifa hasara haraka na kutoa majibu haraka ana nia gani. Kama hii ndilo lilikuwa ndilo jarada la mwisho ofisini huu mwaka kila mmoja anaweza kukubali kitu ambacho si kweli. Yawezekana kuna msukomo furani aidha ujasiri wa kufunga mjadara anautoa wapi? Wizara yake ndiyo kinara kwa kuthibitisha mikataba yenye utata ikiwemo ya madini na waewekezaji ambao kwa ujanja wanabadirisha majina ya makampuni inapofikia kuanza kulipa kodi. Haya yote yanaweza kupigwa stop na wanasheria wakereketwa wazalendo. Wasomi wote kila mmoja kwa fani yake akionyesha uzalendo nchi inaweza kuimalika baada ya kupata katiba mpya.

    ReplyDelete
  6. MTAKAOCHANGIA KWENYE AKAUNTI HIYO MMELIWA SEHEMU KUBWA YA WATANZANIA NI MAFISADI ILA WANATOFAUTIANA KWA UKUBWA NA UDOGO WA AINA YA UFISADI. WATANZANIA WENGI NI WEZI NA PENGINE HAO WATOAJI MAONI WENGI AMBAO KALAMU ZAO AU KEYBOARD YA KOMPUTA HAIACHI KUANDIKA MAFISADI WAKATI NDANI YA NAFSI ZAO NI MAFISADI. NCHI INASIKITISHA WATU WANAONA UTAJIRI NI MUHIMU KWAO KULIKO KITU KINGINE CHOCHOTE,WANAFIKIA KUUA HATA WAZAZI WAO WAENDE KWA MGANGA NA VIUNGO ILI WAPATE UTAJIRI NA TUSIJIDANGANYE HAYA YANAFANYWA NA WATU WASIO NA ELIMU,SIO KWELI HATA WASOMI NAO WAMO. TUWE MAKINI HIVI KWELI MTU ANAYETAKA KUTETEA NCHI YAKE ANAWEZA KUZUNGUMZIA KIZANI ATI KWA KISINGIZIO WANAWEZA WAKAVURUGWA,HIYO SI KWELI.HILO NI DILI WATAPEWA PESA HAO NA MAFISADI. WANGEANZA HAPAHAPA NYUMBANI KUWABANA WATUHUMIWA WA UFISADI. LEO KINA MARANDO WANAWATETEA MAFISADI WA EPA,BOB MAKANI NA WENZAKE WANAMTETEA ALIYEKUWA BALOZI WA ITALY AMBAYE ALIBEBA MABILIONI MBONA HATUWAONI HAO MAWAKILI NAO WAKAJIPANGA KUHAKIKISHA HAWA MAFISADI WANAREJESHA PESA NA KUHUKUMIWA? WOTE HAO BABA MOJA MAMA MOJA .MNAWACHEKA WANAOPEWA KANGA NA SUKARI KWENYE UCHAGUZI NA NYIE MNAODANGANYIKA KWA HILI MNA TOFAUTI GANI?

    ReplyDelete
  7. Bila kutaja mmilki au wamilki wa Dowans na uhalali wake tukubali kuwa serikali inataka kutuibia kwa kuwapa wakubwa zake pesa yetu. Muhimu ni kuiwajibisha serikali ambayo kazi yake kuu ni kulinda raia na mali zao.
    Serikali yetu imekuwa kichwa cha mwendawazimu.
    Walikuja IPTL, Richmond, na sasa Dowans wakachota. Hapa hujagusia EPA, CIS, Meremeta, SUKITA,Tangold, na mazimwi mengine ambayo yote yana mkono wa wakubwa. Kazi ya Kikwete hata mimi siioni.
    Umma wapaswa kuamka na kuondosha kadhia hii.

    ReplyDelete
  8. Sasa nyinyi watanzania acheni kuchanganyikiwa. Kila mtu anajifanya kujua na kuwa kiongozi. Tatizo wasomi wetu wamekuwa parisan. Wengi wanatoa maoni kisiasa kiasi kwamba sisi watu wa kawaida hatupati taarifa zenye ukweli. Ili swala la Dawns na Richmond lilitatuliwa zaidi kisiasa ndiyo maana we are now paying the price. Akina Sitta, wabunge na wapambanaji na wanaharakati walishughulikia tatizo hili kwa kutaka kujijenga kisiasa na matokeo yake tumeyaona. Sasa wanamwambia mwanasheria ajiuzuru. Jamani tuachane na siasa za kukurupuka. Halafu hawa wakurupukaji hawataki kusikia mtu mwingine mwenye mawazo tofauti hii ni demokrasia gani tunayoijenga?

    ReplyDelete
  9. Hongereni wanasheria mlioamua kujitoa muhanga kuinusuru nchi yetu kutoka katika konga za wanasiasa walafi. Mimi niko tayari kuchangia gharama wakati muafaka ukifika ili mradi utolewe utaratibu wa jinsi ya kuchangia. Ni matumaini yangu watanzania wenzangu wenye uchungu na nchi yao wataungana nanyi!

    ReplyDelete
  10. CCM IKO HALI MBAYA KIFEDHA.
    Mhe jaji werema tunajua sasa unafanya kazi uliyoelekezwa, kama kweli una mafaili kibaooo yanayohitaji uyapitie kwa utulivu na kwa kina kisha utumie taaluma yako kutenda kazi. kwa uzoefu inaonyesha si kazi ya siku tatu hasa ukitaka kujiridhisha. naona na wewe unaelekea kwa mwenzio wa VIJISENTI,(RAIS WA AFRIKA). Jamani naungana na mtu mmoja aliyesema ka kuuliza swali kwa wanasheria wetu ambao wana uzalendo wa dhati(sijui kama kweli) JE MNA NIA YA DHATI NA SUALA HILI.? isije ikawa mnatafuta umaarufu ama vinginevyo, mkumbuke tofauti na hivyo MUNGU anajua kilicho mioyoni mweni na mimi binafsi nawaombea heri ili MUWEZA WA YOTE AWAJAZE NGUVU YA KUPAMBANA NA HAO WEZI WATATU WA KIMATAIFA.

    ReplyDelete
  11. Wanajeshi Mko wapi???????

    Enough is enough. Jeuri imekithiri kupita kiasi, hawaheshimu wanaichi tena. Kivuli cha demokrasia kunatuua. It is time yale ya Mauritania au Niger yafanyike. Nchi isimamishwe inakokwenda ambako siko na kurudi tunakotakiwa kwenda. Hakuna njia nyingine ila kujitoa mhanga.

    Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  12. Unayetaka kujitoa muhanga jitokeze tukufunge mabomu kifuani ujilipue kama una ujasiri huo,acheni blabla

    ReplyDelete
  13. Kweli tuliimba wenyewe wimbo "Mungu Ibariki Tanzania, WABARIKI VIONGOZI WAKE".... Sasa wambarikiwa.....Halafu baada ya HESHIMA, ww raia uheshimu, UMOJA - yaani Ukubali lilisemwa, na AMANI - uwe na amani"

    Yote tumeyapata, na tunaendelea kuyaomba hayo hayo. Tusilie......

    Tunahitaji Tanzania mpya.

    ReplyDelete
  14. Kuna utata kisheria katika kuilipa DOWANS.Kampuni hii kisheria haipo.Msajiri wa makampuni ktk database yake anesema bayana kuwa imesajiliwa,mmiliki wake hajulikani,is it possible? Kama haina mmilikiki malipo hayo akabidhiwe nani? Katika malipo hayo,mmiliki wake ni lazima ajulikane,whose signatory for the compassatio to be paid? Mmiliki alete vivuli vya nyaraka vinavyoonyesha jina la mmiliki ktk usajili wake,wananchi wamjue.Nje na hapo changa la macho na TUTAANDAMANA HADI TUMJUE MMILIKI WA DOWANS.Hawezi akawa MWAIFWANI,MWANJONDE,AU MWAFILAMBO SASA NI NANI?

    ReplyDelete
  15. Nimesikia Freeman Mbowe na baba yake wana hisa IPTL sasa sijui tuamini au iwe ni majungu?

    ReplyDelete