31 December 2010

Kortini kwa kuua wazazi wao

Na Bazil Makungu, Ludewa

WAKAZI wa Madunda Wilaya ya Ludewa, mkoani Iringa, Bw. Tito Willa (29) na mkewe Bi. Theopista Mtitu (29) juzi wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya kwa makosa mawili ya kuwaua
wazazi wao, Bw. Laurent Willa (60) na Bi. Alfonsia Msanga (56) kwa kuwakata vichwa.

Wakisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Bi. Mariam Rhobi Omari, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Bw. Robert Mwaluswa alisema katika kosa la kwanza washtakiwa wote kwa pamoja Desemba 25 mwaka huu saa 12:00 jioni walimuua Laurent Willa kwa panga na kutenganisha kichwa chake na kiwiliwili nyumbani mwake.

Katika kosa la pili, Bw. Robert aliiambia mahakama hiyo kuwa katika muda na mahali palepale washtakiwa kwa makusudi walimuua kwa mapanga Bi. Alfonsia Msanga na kutenganisha kichwa na kiwiliwili chake. Pia watoto hao baada ya kufanya mauaji hao wanadaiwa walifanya sherehe.

Awali akizungumza na Majira mtoto wa marehemu, Bw. Damasco Willa alisema amepata karatasi aliyoandika na marehemu kama wosia iliyodai amechoshwa na vitisho kutoka kwa mwanawe, kwamba angemuua wakati wowote.

"Muda mrefu sasa kaka yangu amekuwa akimpa vitisho baba na mama yangu bila sababu yoyote ya msingi huku akiwasingizia mambo ya ushirikina, jambo ambalo siyo la kweli," alisema.Washtakiwa wote hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

3 comments:

  1. hivi kuua wazazi wako ndiyo suluhisho ktk matatizo ya maisha? malipo ni hapahapa duniani.

    ReplyDelete
  2. naomba sheria ichukue mkondo wake wazazi wake wamemweka tumboni miezi 9 na kumkuza leo kakua anawaua wazazi sidhani kama mtakuwa na maisha mema baada ya hapo FRANCIS PAUL DSM

    ReplyDelete
  3. hao wauwe kwa kukatwa kidogokidogo mpaka wafe tena kwa muda wasiku saba bila chakula na tena wafungwe kamba kichwa chini miguu juu by carlos

    ReplyDelete