02 December 2010

Wakamatwa na nusu tani ya bangi

Na Benjamin Masese, Musoma

JESHI la Polisi mkoani Mara limewakamata watu watatu akiwemo mpiga picha wa kujitegemea wa kituo cha Televisheni cha ITV mjini Musoma kwa kukutwa na zaidi ya kilo mia tano za bangi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishina Msaidizi wa
Polisi, Bw. Robert Boaz aisema kuwa watu hao walikamatwa na kiasi hicho cha bangi Novemba 24 wakitoka katika Kijiji cha Ngoreme Wilaya ya Serengeti, wakati wakiisafirisha kwenda kuuza Kenya.

Watuhumiwa hao ni Bw. Athuman Mohamed (25), mkazi wa eneo la Mwigobero mjini Musoma, Bw. Chacha Mnanka (32) na William Werema (62) wote wakazi wa Ngoreme wilayani Serengeti.

Kamanda huyo wa Polisi alisema kuwa watuhumiwa hao
walikamatwa katika Kijiji cha Rung’abhure wilayani Serengeti wakiwa njiani kuelekea nchi hiyo jirani.
Taarifa zilifikishwa na raia wema wakiwemo waandishi wa
habari, baada ya kuelezwa kuwa kuna watu wanajihusisha na ununuzi wa bangi kisha kuuza nje ya nchi na wakati mwingine wamekuwa wakitumia gari lao kama la waandishi wa habari, wakiwa na kamera ili kudanganya, ndipo tulipoweka mtego uliozaa matunda haya,” alisema Kamanda Boaz.

Hata hivyo, alisema pamoja na kuwakamata watu hao bado jeshi hilo linawahoji watu mbalimbali akiwemo mwakilishi wa ITV Mkoa wa Mara, ili kujua endapo wanahusika na biashara hiyo haramu.

Alisema uchunguzi wa awali umekamilika ambapo
watuhumiwa hao watatu watafikishwa mahakamani mjini Mugumu kujibu tuhuma zao hizo.

No comments:

Post a Comment