24 December 2010

Sijapewa sumu-Zitto

Na Mwajabu Kigaza, Kigoma

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe amesema kuwa hajapewa sumu kama ilivyokuwa imedaiwa huku akisisitiza kuwa hakuna binadamu anayeweza kufanya hivyo.Pia mbunge huyo
wa Kigoma Kaskazini, amesema hana nia wala mpango wa kukihama chama hicho.

Bw. Kabwe aliyasema hayo juzi wakati akiwahutubia mamia ya wananchi Mkoa wa Kigoma katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kawawa ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji.

Alisema kuwa migogoro inayoendelea ndani ya chama chake isiwafanye wananchi wa Kigoma kuwa na hofu yeyote na hata yale yanayoandikwa na vyombo vya habari pia yasiwanyime rah,a waendelee kukisimamia chama chao.

"Wananchi wenzangu msiwe na wasiwasi, mimi ni mzima kabisa, yameandikwa mengi katika vyombo vya habari, mara nimepewa sumu, nataka niwahakikishie hizo habari si za kweli, mimi sijapewa sumu na hakuna binadamu anayeweza kunipa sumu, tuendelee kufanya kazi na kukijenga cha chetu," alisema Kabwe.

Siku za karubuni kumekuwapo na mgogoro ndani ya CHADEMA kutokana na mbunge huyo kutofautiana na wabunge wenzake kuhusu msimamowa kususia hotuba ya Rais jakaya Kikwete bungeni, hali iliyosababisha chama hicho kuundama kamati ya kuzungumza naye kumpa ushauri.

hatua hiyo ilichukuliwa siku chache baada ya wabunge wenzake kupiga kura ya kutokuwa na imani naye, kama Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni.

Wakati wabunge hao wanachukua uamuzi huo, Bw. Kabwe aliugua ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Aga Khan akisumbuliwa na tumbo, na baadhi ya vyombo vya habari vililiripoti kuwa amelishwa sumu, ingawa madaktari walisema ni tumbo lake lilikuwa tu limechafuka.

Katika hatua nyingine Zitto aliitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI) kuitisha uchaguzi wa meya wa Kigoma/Ujiji haraka ndani ya wiki mmoja uliokuwa umesimamishwa wiki iliyopita kutokana na mgogoro wa mgawanyo wa madiwani wa viti maalumu.

"Halmashauri zingine tayari zimeshafanya uchaguzi na wamepata meya, na kazi za kuleta maendeleo wameshaanza, sasa wao wanapozidi kutucheleshea sisi kufanya uchaguzi, wajue na kazi ya kuleta maendeleo katika manispaa yetu inazidi kuchelewa," alisema Bw. Kabwe.

Mbunge huyo amewataka viongozi wa vyama mbalimbali nchini kutumia fursa walizozipata katika kuleta maendeleo ya jamii na sio kuendekeza uadui na serikali kuu.

9 comments:

  1. Hongera sana Mh.Zito,Kwakuwa una urafiki wa karibu na Mh.Rais Kikwete ninaomba umkumbushe wakati mwingine atakapo samehe wafungwa awakumbuke wafungwa wa maisha waliokaa gerezani zaidi miaka15 awasamehe.Na isitoshe wafungwa wanaotumia vifungo vya maisha na wao ni binadamu kama sisi ispokuwa sio watoto wa vigogo.

    ReplyDelete
  2. Sasa tuone ushirikiano wako unaoufanya na wenzio sio kupayuka payuka tu. Fanya kazi ionekane kitenda cha KIGOMA kwenda NCCR sikuamini wewe ni kigeugeu hujengi chama unabomoa tu. Chadema mchungeni sana huyo anajikosha atakuja na stail nyingine. Hasa wabunge muwe macho nae akipata watu wa kumuunga mkono huyo anabomoa chama.

    ReplyDelete
  3. Wewe Zitto una kimbelembele sana huna sifa ya kuwa kiongozi kwasababu unapenda sana kuwa kwenye spot light. Chadema sio mama yako utaondoka tu siku yako ikifika. Hata Marehemu Mwl Nyerere alisema CCM sio mama yake. Augustine Mrema alisema hivyovyo hawezi kuondoka NCCR sasa hivi yuko wapi? siku zako zahesabika yakhe watch.....

    ReplyDelete
  4. Tunaomba Chadema msifanye makosa ya kumweka Zito kugombea urais 2015. Sisi wananchi na wanachadema TUMESHAMKATAA TANGIA SASA.

    ReplyDelete
  5. Hapa ndipo haja ya kuwa na katiba mpya inapoonekana kuwa kubwa. Wanasiasa aina ya Zitto ambao hawawezi kwenda na misimamo ya vyama vyao wanaweza kuwa wagombea wazuri na wawakilishi wazuri kwa kugombea kama WAGOMBEA BINAFSI. Wanataka wawe maarufu kuliko vyama vyao. Wanalazimika kujiunga na vyama ili kupata ubunge, kumbe ingewawia rahisi kuwakilisha kama wagombea binafsi kama katiba ingekuwa inaruhusu. Zitto hawezi ku-fit katika chama cho chote bila kuzusha tafrani, na kwa hakika CHADEMA wajiandae kubeba mzigo huo hadi 2015. Poleni sana wana-CHADEMA

    ReplyDelete
  6. Well, said that Zito has no stand and undefined at times.
    I personally think he is bought and he is not a true oppositionist but rather disguised as Chadema while he is infact CCM just Like Mrema of FLP.
    It is high time you show your true colors Mr.Zito!
    Hon.Zito contray to what the names suggest in Swahili, but your really hold no weight than that of a feather in Chadema, and it is too bad we are realising this little too late!. But for heavens sake Step down and let this genuine party lead our Nation to victory for the benefit of our country Tanzania at Large.
    Not being one with your comrades and fellow leaders in the decision that was ment to send a strong message for constitution change and unjustified election results well etc was so unpatriotic on your side.
    Had i been you resigning would have been the wiser option; so as to be responsible for you action!.
    Now that you haven't resigned, Please tell us how are your going to make up for the lost trust?!.

    ReplyDelete
  7. Iko siku watakupa hiyo sumu,jihadhari. iko siku nilikuwa kwenye majadiliano kwenye facebook,mchangiaji hoja mmoja ana family name la kichaga sitaki kumtaja jina,nilimuuliza hao wanaoingiza masuala ya dini kwenye uchaguzi kwa sababu ya padri slaa itapofika 2015 ccm ikisimamisha mkristo mwenzenu apambane na slaa je hamtabaguana huyu mprorestant,hatufai? akanijibu nimekosea sana maana chadema watamsimamisha kijana mahiri zitto mwislam mwenzenu,nilicheka sana nikamwambia kama mtafika naye huko sijui akanipinga sana na sasa yanajitokeza,hata siku mija hawezi kuwa mtu ambaye si kibaraka wa watu wa mikoa ya kaskazini ashike madaraka makubwa chadema,chadema ina wenyewe, hamkusikia juzi slaa akiwaambia chadema mbeya njia nyaupe ondokeni. na wewe zitto kaa sawa hapo

    ReplyDelete
  8. Hao wachaga ni mafia watakuua tu.hamna chochote watanzania watapata chadema ikishika madaraka,huko ikulu kuna nini mpaka chuki na ugomvi mkubwa kiasi hicho hata baada ya uchaguzi kwisha. wewe padri slaa umezungukwa na wafanyabiashara papa wa kichaga kama ilivyozungukwa ccm,watz tuachane na vyama hivi viwili ili tupate maendeleo ya kweli,hawa ugomvi wao mkubwa ni jinsi ya kuitafuna hazina yetu zaidi ya kuwaletea maendeleleo,ikulu si pahala pa biashara,chaguaeni watu kutokana na staili yao ya maisha wanayoishi,hivi wewe Mbowe kweli una sifa ya kushika uongozi wa juu katika serikali yetu? hazina itapona? umebeba pesa NSSF kama walivyobeba kina sumaye kisha ikawa tabu kurudisha leo ati tukupe hazina ya nchi yetu.hakutakuwa na tofauti. hata majira ukichakachua maoni haya ujumbe utakuwa umefika

    ReplyDelete
  9. Mheshimiwa Zito ulitakiwa upime kwanza kama utaendelea kuwa Naibu kiongozi wa upinzani au la?
    Hivyo unavyofanya unabomoa Chadema si kujenga!
    Tunaomba umtii mwenyekiti wa CHADEMA na si mwenyekiti wa CCM,Kama unataka kuwa karibu na Kikwete siuhamie CCM.
    uKIGOMBEA URAIS siku hiyo ndiyo upinzani utakufa rasmi.

    ReplyDelete