06 December 2010

'Serikali za umoja wa kitaifa ni uroho'

Na Grace Michael

KUWEPO kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa nchini Zanzibar imedaiwa ni mpango wa baadhi ya viongozi wa kutaka kuendelea kuwemo madarakani milele.Akizungumza na Majira jana kwa njia ya simu Bi. Catherine Malila ambaye alijitambulisha kuwa ni mwananchi wa
kawaida na mjasiriamali, alisema kuwa kupwaya kwa vyama vya upinzani au kuwepo kwa wapinzani wenye uroho wa madaraka umewafanya kukimbilia hatua hiyo.

"Mpango wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni mpango wa serikali zilizopo barani Afrika kutaka kutawala milele...wapo wanaotaka wawemo tu madarakani hata kama hawana ridhaa ya wananchi, hivyo hii hali ni mbaya kwani wananchi hawajashindwa kuchagua watu wa kuwaongoza kulingana na vyama vyao," alisema Bi. Malila.

Alisema kutokana na hali hiyo ni vyema serikali za namna hiyo zikaepukwa na suala hili kuachwa kwa wananchi, ambao ndio waamuzi wa mwisho katika suala la kuchagua viongozi wanaowataka wa kuwaongoza.

"Tatizo jingine wapinzania nao wana kasoro na hii inasababishwa na kuwepo kwa baadhi ya watu ambao nia yao kubwa ni madaraka na ndio maana hata CUF huko Zanzibar waliokuwa wanataka madaraka wameyapata na wamenyamaza kimya bila ya kujali ni makaburi mangapi yanayowatazama ambayo katika harakati hizo walisababisha umwagaji wa damu," alisema.

Akizungumzia msuguano ulipo sasa wa vyama vya upinzani ambao umewafanya wabaki wakirushiana lawama za hapa na pale na kushindwa kuwa kitu au msimamo mmoja ndani ya bunge, alisema kuwa wanachotakiwa kila mmoja kuangalia wananchi waliomchagua hivyo wajikite katika kuwatumikia wananchi na sio kuendeleza malumbano.

"Kila mmoja alichaguliwa na wananchi kwa sera alizozinadi, hivyo waachane na malumbano yao na wajikite katika kuangalia mahitaji ya wananchi waliowachagua na kwa upande wa vyombo vya habari navyo vifanye kazi yake ya kuwasemea wananchi ambao hawana sauti," alisema.

Mbali na hayo aliviomba vyombo vya habari kuandika habari zenye maslahi kwa Watanzania hasa kwa kuangalia tatizo kubwa la umaskini ambalo limesababisha tabaka kubwa la wenye nacho na wasio nacho.

Bi. Malila alisema kuwa kitendo cha kikundi cha watu wachache kujilimbikizia mali nyingi kwa njia za kuwanyonya wananchi wa kawaida ndicho kinachowakera wananchi na kuwafanya wawaadhibu katika chaguzi kwa kuwanyima kura.

20 comments:

  1. Wewe Grace umesomea wapi uandishi. Article yako umeichapisha kwa mawazo ya mtu mmoja - "Bi Malila" bila ya kufanya utafiti wa kutosha na kutupa takwimu za kisayansi tukafaidika!

    Kama lengo ni kuwasema hao Wazenj,binafsi sidhani kama ni kosa, kwani kulingana na hali waliyokuwa nayo na mazingira yaliyopo, serikali ya umoja wa kitaifa-GNU ndi chaguo lililobaki.

    Wewe ulitaka zifanyike chaguzi ngapi Zenj ili kuleta amani na utulivu. Nadhani hapa kwetu iwapo Chadema itaendelea kunyakua viti kadhaa na ikatokea CCM wakakataa kutoa madaraka,suluhisho litalobaki ni GNU.

    Lengo la mimi na wewe ni maendeleo, iwapo hatutoyapata katika multi party politics,njia ya salama ya kuwaunganisha wananchi ni GNU. Hii ni kulingana na mazingira yakwetu

    ReplyDelete
  2. Mwandishi umeandika comment za grace kwa mantinki ipi? basi chukua hata comments zangu pia uchapishe gazetini! La sivyo haileti maaana kabisa! kila mtu anamtizamo wake! huwezi kuchukua comment za Grace mmoja tu na mhariri kuzipa headiline "GNU ni UROHO" how come? mlifanya reasearch kweli? AU HESHIMA YENU IMESHUKA? au ndio Znz si nchi maneno ya Pinda?

    ReplyDelete
  3. Bi Malila hatakama ni uroho wamadaraka wewe Zanzibar inakuhusu nini? waliokufa ni wanzazibari si watanganyika na hiyo GNU ni sisi wazanzibari ndio tuliopiga kura ya kukubali sasa nini kinachowauma ?

    ReplyDelete
  4. Jamani nawaomba hebu waachieni hawa wajinga Bi Malila,Grace n.k walie mpaka watokwe na machozi ya damu, sisi waZanzibari kilio hicho hakitushughulishi wala hakituumishi vichwa vyetu, waZanzibari tuko imara na tunakijuwa nini tunachokifanya ambacho kitatuongoza kuingarisha na kuleta nuru ya maendeleo, neema na maisha mema. BIIDHNI LLAH.

    ReplyDelete
  5. sasa bi Grace unasema hivyo lakini je unafhamu kuwa hiyo serikali iliopo imewekwa na wanachi? walipiga kura ya maoni na wakaikubali,au kwa kuwa Tanganyika hakuna kitu kama hicho ndio unataka kusema kuwa Zanzibar haiwezi kuwa nacho ? wacha zako hizo....Zanzibar wanafanya kilicho na maslahi nacho na hakuna bunge wala raisi wa jamhuri au nani atakesema hii haifai...huu sio wakati wa Nyerere aliposema kuwa Jumbe atolewe kwenye uraisi au Seif Sharif afukuzwe kwenye chama na amri yake ikatiiwa,wakati umebadilika..sasa ni kuheshimiana na sio kuogopana.Mwandishi unaandika mawazo ya mtu 1,je huna kazi ya kufanya ?

    ReplyDelete
  6. Hamna lolote, ni uroho wa madaraka kweli. si mseme tu. na yetu majicho. na wewe unadai eti ya zanzibar yanawahusu nini inamaana umewatenga watanganyika. Haki ya walahi hiyo dhambi iwatafune. Nawaombea kwa Mungu hiyo serikali idumu kama haina uroho wa madaraka lakini kama kuna mkono wa uroho........ kazi kweli kweli. watanganyika someni alama za nyakati oooh!

    ReplyDelete
  7. Hapa inaonyesha ni jinsi gani watanganyika wasivyo elewa. mtoa mchango hapo juu namuunga mkono kidogo. Maoni hayo mengine hapo juu yanaonyesha jinsi gani Wazanzibar ambavyo hawa wadhamini watanganyika. Unaposema damu iliyomwagika ni ya wazanzibar na siyo watanganyika huo ni ubaguzi. Mnajiona wazanzibar sasa hivi, tutawaona huko mbeleni. Watanganyika na kweli someni alama za nyakati. Hakuna maana ya muungano wakati wenzetu wamejitenga kwa mengi. Bora ibaki Tanganyika kama Tanganyika.

    ReplyDelete
  8. Wanzanzibar tuko imara na wala si wakati tena wakututisha kisiasa kwamba tunajiona wanzabari sasa hivi,si sasa hivi tu ni wanzanzibar tokea tulipopata uhuru wetu na kuhusu suala la kusema kama bora mubaki kama watanganyika sisi hilo hatuliogopi na ndilo tunalolipigia kilele kama unafuatilia vizuri.

    ReplyDelete
  9. GRACE umewapa ukweli na wajitambue ya kuwa tulikuwa tunawaangali. Hawa watu ni wagomvi hawakusaidii chochote zaidi ya kujikomba kwako na kujishaua. Kama ni uandishi dada yetu kaandika ukitaka kutambua amefanya nini tafuta kitabu cha VERONICA QUEEN au film yake utajua mwanamke huyu alifanya nini kwenye nchi yake mpaka ikapata amani na unyanyasaji ukaisha katika serikali yao. Serikali inajikomba kwao kuhusu utaifa sasa wayaone. Ndio maana wanalialia udini udini. Hawa watu wanaagenda ya siri sema tu hawajatoa makucha yao. Wanakula taratibu taratibu kama mchwa.

    ReplyDelete
  10. ZANZIBAR NI NCHI, itafanya itakavyo bila usimamizi wa Tanganyika! GET IT IN YOUR MIND you idiots

    ReplyDelete
  11. Walitaka wabara wazanzibari waendelee kuuwana ili wapate kutumia rasili mali zao. Wazanzibari wamepiga kura ya maoni na wamekubali wenyewe serikali ya pamoja. matokeo ya uchaguzi ccm 50.1% na cuf 49.1% kigezo gani unataka kuonyesha kuwa znz lazima serikali ya pamoja?
    Wacheni ubinafsi, waachieni wazanzibari wafanye mambo yao jinsi wanavotaka.

    ReplyDelete
  12. Waatanganyika wengi wenu ni kuweka viti nje mukanywa pombe, ndio munaona maisha mumeyapatia kwa ujinga wenu siasa hamuijui suburini tuwafundishe siasa, mutashtuka labda baada ya miaka ishirini, Grace ndio mdudu gani? Wazanzibar wamepiga kura kuamua aina ya serikali waitakayo sasa tabu iko wapi? au furaha yenu haikutimia yakuona tunauliwa na jeshi la Kikatoliki? subirini kidogo Wakatoliki ndio arubaini zenu zinakaribia, maana historia ya dunia nzima kila palipokuwa na vita muanzilishi ni kanisa katoliki, tukianzia Rwanda,Burundi,Congo, sudan,Siera Lion na nchi nyingi za Afrika na Ulaya, East na West,kwa hiyo Watanganyika tunawapa heads-up kazi kwenu, sisi haooooo.

    ReplyDelete
  13. Tumsubirie OSAMA BIN LADEN arudi atawamaliza. Kwanza aanze kule asia ambako mauaji hayaishi. Tumechoka kuangalia luninga kila siku za huko zinafundisha vijana wetu maadili mabaya ya ukatili. Sadamu atakwenda kumaliza na mahakama yao ya kadhi, huko Somali, Nigera, Sudani nk. Nendeni shule mtajua elimu ni nini.

    ReplyDelete
  14. Mchonga Meno, mkatoliki, kaondoka kama walivyoondoka wenzake wasio wakatoliki. Dunia inabadilika vibaya sana. Watanganyika wengi bado wana kasumba za mchonga meno kwa hio si ajabu wakashikilia mambo ya karne zake. Alokufa keshakufa, nyie bado muko hai wacheni taka za mashikio hizo jamani. Dunia inaendelea mbele, jifunzeni nini maana ya development, sio mukae na kasumba zenu hizo. GNU ni katika maendeleo.

    ReplyDelete
  15. Hivi hii mizigo Rais aliyokwenda kuchukua huko Zanzibar nani atamsaidia? Hatumo yakikushinda uyatatue mwenyewe. Mzigo yenywe ndio iko bandarini haijapakuliwa lakini makelele hayooo. Utadhani ndio kila mmoja ameambiwa achukue upamga aingie mitaani.

    ReplyDelete
  16. Dada katoa mawazo yake mbona hamjengi hoja ni kulaumu watanganyika tu,jengeni hoja leteni mezani tujadiri,Huyo Seif alitaka madaraka hilo halina siri,ndiyo maana hata wabunge wa chadema walivyotoka bungeni wakati Rais kikwete anaanza kutoa hotuba,Seif alisema ule ni uhaini ila kasahau wabunge wa cuf walitoka bungeni na kutomtambua rais wa znz kwa miaka kumi?!!,ama kweli wanasiasa kiboko,Fatma Maghimbi na mwenzie kelele nyingiiiii mwisho wa yote kunyimwa nafasi ya kugombea ubunge huyoooooo ccm,ama nitumie nafasi hii kupongeza Rais mstaafu wa znz KOMANDOO Dr Salimin Amour Juma,huyo ndiye rais niliyemuheshimu sana huko znz,maana alifuata SHERIA, kama unataka kujua KOMANDOO ni nani muulize Duni Haji
    kamandoooo uko wapi gombea tena urais zenji

    ReplyDelete
  17. Komandooooooooooooooo uko wapi??,watu walishaanza kelele rudi

    ReplyDelete
  18. Ndugu zetu wa bara bado mnaishi katika complacency ya Chama kimoja, nyinyi kwenu mnachojua kuwa ni CCM kushinda kwa hali yoyote! Je huo si uroho wa madaraka?

    Hebu angalieni, Zimbabwe, Kenya na Sasa Guinea na kwa Mama yenu UK kote kuna mfumo huohuo. Kinachopelekea wapinzani kuingia katika GNU ni pale serikali zilio madarakani zinapogeuka ni mfao wa Ufalme wa milele na kuhodhi nguvu za dola kwa kisingizio cha sera za chama na kuingiza siasa katika majeshi yake kisha kutumia nguvu hizo kukandamiza raia hasa wakati wa uchaguzi!

    Tumeona jana tu nini kimetoke Ivory Coast na mpaka leo hakuna serikali za Africa hata moja iliokemea incumbent kukataa matokeo kama kashindwa na badala yake Jeshi limeunga mkono!

    Egypt nayo hali kadhalika! Leo under the AU Sudan inataka kupasuliwa pande mbili katika misingi ya Kidini na Nchi kama Kenya, Uganda na Tanzania ziko mstari wa mbele kushangiria hilo! Wakati ulimwengu mzima unajuwa kuwa nguvu za nje ya Africa ndio ziko nyuma sababu ni Mafuta na Gesi asilia. Tusubiri tusikie Tanganyika inagawiwa miko ya kusini iwe ni tanganyika ya Kusini na Ya Kaskazini kusikokuwa na mafuta iwe ni Tanganyika ya Kilimanjaro na Serengeti!

    Ndugu zetu kama hamsomi hayo mtabaki hivyo na kulaumu failure yenu kisiasa kusingizia wa Zenj! Sisi tumejifunza zamani hizo janja za Magharibi including Kanisa tokea zama za Livingstone na Speke ndio maana hatuwaamini nyinyi kwani mumeanza kushiriki tokea hapoa awali na lengo ni kuimeza Zanzibar.! Tukiwahesabia mliyiyafanya ni mengi lakini tunawapa la hivi karibuni tu. Yaani siku tano kabla ya uchaguzi Zanzibar mumeleta jeshi lenu la mauwaji na kuzikalia sehemu zote nyeti za Serikali ya SMZ kisingizio cha kuleta usalama wakati jeshi liliahidi ahlitoingila uchaguzi, kumbe liko standby kutimiza matakwa yenu ili wapinzani wakatae matokeo muanze kuuwa kama kawaida yenu lakini hamkujua siri ya maridhiano basi ndio hii siri kubwa ni kuwa juhudi zenu za kutugawa na kutuua tumeiweka chonjo!

    ReplyDelete
  19. kama nyinyi rudi nyerere na angekuwa rais mpaka leo mngekuwa hakuna hata tv hata moja huko kwenu shenzi type

    ReplyDelete
  20. ivinikitugani kina sababisha wa tanzania kua na uroho wa madaraka ikiwa baadhi yetu atuna la kusema nibora tunyamaze, lakini kwa hili atutoweza kulifumbia macho nilazima tuonyeshe mabadiliko ya kisiasa,nina wapongeza sana wale walio jitolea kutufikisha hapa tulipo, ila tusiishie hapa ni lazima tukumbuke ya kwamba tuna safari ndefu, kwenye msafara wa tembo fisi hawakosekani.

    ReplyDelete