06 December 2010

ROBO FAINALI CHALENJI

*Kili Stars, Rwanda uso kwa uso
*Zanzibar Heroes mdomoni mwa Uganda


Na Zahoro Mlanzi
WENYEJI wa michuano ya Chalenji, Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars sasa itakumbana na Rwanda 'Amavubi' katika mechi ya robo fainali itakayopigwa keshokutwa kwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Robo fainali nyingine itakayopigwa
keshokutwa, itazikutanisha timu za Zanzibar 'Zanzibar Heroes' na mabingwa watetezi Uganda 'The Cranes' ambayo jana iliichapa Kenya 'Harambee Stars' mabao 2-0  na kufikisha pointi saba.

'Zanzibar Heroes' nayo imetinga hatua hiyo kutokana na kuwa na matokeo mazuri 'best looser' iliyokuwa nayo katika kundi B.Wakati timu hizo zikisubiri kwa hamu siku hiyo, michezo mingine ya robo fainali itaanza kesho kwa mchezo wa kwanza kuzikutanisha Zambia na Ethiopia na Ivory Coast ambayo itaumana na Malawi. Leo ni mapumziko.Kili Stars imetinga hatua hiyo baada ya kumaliza Kundi A, ikiwa ya pili

nyuma ya Zambia kwa kuwa na pointi sita huku, Rwanda wao wakishika nafasi ya pili kwa pointi tano nyuma ya vinara Ivory Coast, ambayo ina pointi sita.Zambia itaumana na Ethiopia, baada ya kuongoza kundi A kwa pointi saba huku Ethiopia, ikitinga hatua hiyo kutokana na kuwa ya pili hivyo kuwa na matokeo mazuri 'Best looser' kwa kufunga mabao manne na kufungwa manne huku ikiwa na pointi nne.

Ivory Coast imetinga hatua hiyo, baada ya kuongoza Kundi B kwa pointi sita ambapo sasa itaumana na Malawi, inayoshika nafasi ya pili katika Kundi C kwa pointi tano.Katika michezo iliyopigwa jana, Uganda ilipata mabao yake kupitia kwa na Emmanuel Okwi dakika ya 83 na Andrew Mwesiga katika
dakika mbili za ziada kwa mkwaju wa penalti.

Mchezo wa kwanza uliopigwa saa nane mchana ulizikutanisha timu za Ivory Coast na Sudan ambapo Ivory Coast, ilijihakikishia kucheza robo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

No comments:

Post a Comment