06 December 2010

Shibuda awa kivutio mkunoni Sinyanga

Na Suleiman Abeid, Shinyanga
 
SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Shinyanga kimefanya mkutano mkubwa wa kihistoria uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa
mji wa Shinyanga.
 
Katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga juzi viongozi mbalimbali waandamizi wa CHADEMA akiwemo mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kwa tiketi ya chama hicho, Bw. John Shibuda walihutubia na kuvuta kwa kiasi kikubwa hisia za wasikilizaji.
 
Kivutio kikubwa katika mkutano huo kilikuwa ni wananchi kuamua kumpokea Bw. Shibuda kwa stahili ya aina yake alipowasili katika eneo la mkutano huku akibebwa juu juu na umati wa wananchi huku wakiimba, “Jembe jingine limeingia! Jembe limeingia, kiboko cha mafisadi.”

Akizungumza katika mkutano huo, Bw. Shibuda alimtaka Rais Jakaya Kikwete kufungua kesi katika mahakama ya kimataifa kudai fidia kutoka kwa wawekezaji wa madini na fedha zitakazolipwa zitumike kujenga vituo vya afya na shule katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
 
Alisema Rais Kikwete achukue uamuzi huo kutokana na wizi uliofanywa na wawekezaji katika sekta ya madini hapa nchini.  
Alisema pamoja na mikoa ya kanda ya ziwa kuwa na utajiri mkubwa wa madini, lakini wakazi wa mikoa hiyo bado wako nyuma kimaendeleo hasa katika upande wa sekta za elimu, afya na uchumi wa mtu mmoja mmoja. 
Alisema iwapo serikali itadai fidia hiyo fedha itakayopatikana itumike kwa mikoa hiyo kujengewa vituo vya afya, zahanati vijijini na mabweni katika shule za sekondari za kata na kuinua uchumi wa wananchi wake.  Sisi CHADEMA sasa tunamuomba Rais Kikwete kama kweli anachukizwa na vitendo vya ufisadi ashirikiane na waziri wake wa mambo ya nchi za nje wafungue kesi katika
mahakama ya kimataifa kudai fidia kutokana na wizi tuliofanyiwa na wawekezaji wa madini kupitia mikataba mibovu.
 Kama kweli viongozi hawakupokea  kutoka kwa wawekezaji, basi tunaomba kesi hiyo ifunguliwe, tumenyonywa sana kupitia mikataba mibovu iliyoingiwa kati ya wawekezaji na viongozi wetu, wananchi tulipwe fidia, Kikwete usipofanya hivyo ni wazi unalinda mafisadi, alisema Bw. Shibuda na kushangiliwa na wananchi.

Aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Bw. Philipo Shelembi aliwataka wakazi wa mji huo kuwa
watulivu na kusubiri matokeo ya kesi iliyofunguliwa katika mahakama kuu kupinga matokeo ya uchaguzi wa mbunge katika jimbo hilo.
 
Bw. Shelembi alisema kwa hivi sasa wanachama na wapenzi wa CHADEMA hawana budi kukaa na kusubiri uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya kupinga kutangazwa kwa mgombea wa CCM, Bw. Steven Masele.
 
Kauli hiyo Bw. Shelembi ilimaliza uvumi uliokuwa ukisambaa pole pole mjini hapa kuwa CHADEMA wameshindwa kufungua kesi hiyo ikidaiwa kuwa mgombea huyo amepewa fedha na kutakiwa kuachana na mambo ya kwenda mahakamani. Ndugu zangu napenda nikuthibitishieni leo hii kuwa mimi sijahongwa chochote na watu wa CCM na siwezi kufanya hivyo hata siku moja, ni bora nife maskini kuliko kupokea
fedha za kuhongwa na kuwasiliti watu wa Shinyanga,  Unaweza kupokea sijui sh. milioni 200 au 300 kama ilivyokuwa ikivumishwa hapa mjini na baadhi ya watu, ukafa hata kabla hujatumia senti moja, siwezi kuwaacha wananchi wangu kwa tamaa ya fedha, watu wakiniona nimekaa baa nakunywa wanadai nakunywa fedha za kuhongwa, ni uongo,” alieleza Bw. Shelembi.

4 comments:

  1. Mie sisemi mwe! nadhani msgs sent and delivered. CCM naona ufisadi unatumaliza, jamani tujirekebishe tuweze kurudisha majimbo.

    ReplyDelete
  2. KIKWETE ALIDANGANYWA KUWA SHIBUDA HAKUBALIKI SHINYANGA SASA MABO NDIYO HAYO VIONGOZI WA CCM SHINYANGA HASA MWENYEKITI MGEJA ACHA SIASA ZA MAKUNDI MNAKIHARIBU CHAMA,LAKINI NAJUA TATIZO LENU NI VIWANGO VYA UELEWA YAANI SHULE.

    ReplyDelete
  3. Japokuwa Elimu ya darasani siyo kigezo Muhimu sana kwa Mtu kuwa Kiongozi bora lakini huyu Mgeja ndiyo chanzo cha matatizo yote kwenye CCM.Nadhani wakati umefika kwa kibaraka huyu kukaa pembeni na kupisha wenye uwezo washike usukani.Atumie busara kukinusuru chama.

    ReplyDelete
  4. Nice,Tabora
    Shibuda kweli una nia ya dhati chadema au upo kwa ajili ya uongozi tuu.Shime shibuda onyesha kwa vitendona fanya kazi na viongozi wako wa chama chako cha chadema.Kila la kheri mwana kwetu kwa uongozi sio lazima CCM,bora umekihama chama cha CCM kwani ni chama cha Mafisadi.

    ReplyDelete