24 December 2010

Mwandishi kortini kwa kupokea rushwa

Na Muhidin Amri, Songea

MWANDISHI wa habari wa kujitegemea mkoani Ruvuma, Bw Kwirunus Mapunda, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Ruvuma kujibu kosa la kushawishi na kupokea rushwa ya sh. 200,000,  Mwandesha Mashitaka wa
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoani hapa, Bi. Maria Mwakatobe alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Bi. Janeth Mtega kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Desemba 22, mwaka huu katika mji mdogo wa Peramiho.

Aliendelea kudai kuwa, mtuhumiwa alishawishi na kuomba rushwa ya sh. 500,000 na kupokea kiasi cha sh. 200,000
kutoka kwa Padri Fidelis Mligo wa Shirika la Wabenediktine, Peramiho Songea Vijijini, ikiwa ni malipo ya awali ili asiendelee kuandika habari za ushirikina zinazohiusu taasisi hiyo.

Bi. Mwakatobe aliendelea kuieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo huku akijua ni kosa la jinai, kushawishi, kuomba na kupokea rushwa chini ya sheria na. 15(1) ya mwaka 2007.

Mtuhumiwa huyo alikana mashtaka yote na yupo nje kwa dhamana, na kesi hiyo itatajwa tena tarehe Februari 1, 2011.

No comments:

Post a Comment