03 December 2010

Ipswich kuivaa Arsenal nusu fainali

LONDON, England

KLABU ya Ipswich itapambana na Arsenal katika mechi ya nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Ligi ya Uingereza, baada ya kuifunga Wes Brom bao 1-0 katika mechi ya robo fainali juzi.Ipswich iliweka pembeni jinamizi la kufanya vibaya katika mashindano ya
Ligi ya Soka Daraja la kwanza na kuibuka na ushindi katika uwanja wa Portman Road.

Katika mechi nyingine ya robo fainali, Birmingham ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa, huku bao lake la ushindi likipatikana katika dakika za mwisho kwa kuwekwa kimiani na Nicola Zigic.

Birmingham sasa itachuana na West Ham katika nusu fainali.Grant Leadbitter, ndiye alifunga bao pekee kwa Ipswich kwa njia ya penalti baada ya Graham Dorrans, kumwangusha Carlos Edwards katika eneo la hatari.Brian Murphy aliokoa mpira uliopigwa na Pablo Ibanez, ambao ungeweza kufanya timu hiyo ya nyumbani kusawazisha.

Ipswich maarufu kama Tractor Boys, sasa watapambana na Arsenal katika mechi ya nusu fainali huku, Birmingham itapambana na West Ham ambayo iliifunga Manchester United mabao 4-0.Ipswich ni timu pekee ambayo haipo katika Ligi Kuu, iliyotinga nusu fainali ya michuano hiyo.Timu hiyo itacheza mechi ya kwanza ikiwa nyumbani dhidi ya Gunners, ambayo itafanyika katika kuanzia Januari 10, mwakani.

Ipswich ilicheza mbele ya mashabiki 11,363 katika Uwanja wa Portman Road  na kufanya kocha Roy Keane, kuwa katika presha baada ya timu yake kupoteza mechi nne kwenye Ligi Kuu.

Birmingham ilipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Villa, katika Uwanja wa St Andrew ambapo Larsson alifunga penalti dakika ya 12 na Zigic, dakika 84 huku bao la Aston Villa liliwekwa kimiani na Agbonlahor dakika ya 30.

Bao la Nikola Zigic dakika sita kabla ya mpira kuisha, liliwakatisha tamaa mashabiki wa Aston Villa ambao baadhi yao kwa hasira walivamia uwanjani baada ya mechi kuisha.Zigic alitumia vyema krosi ya Cameron Jerome.

Villa inayonolewa na kocha Gerard Houllier, ndiyo ilionekana kutawala mpira kwa muda mrefu lakini ilishindwa kuibuka na ushindi, wapinzani wao waliwapa presha na kipa Ben Foster, alishindwa kudaka mpira wa Zigic.

No comments:

Post a Comment