30 December 2010

Abramovic kuwakodi The Black Eyed Peas

LONDON, England

BILIONEA na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amepanga kukodi wanamuziki wa bendi ya The Black Eyed Peas kwa ajili ya kuburudisha wakati wa mwaka mpya.Tajiri huyo wa Chelsea mwenye miaka 44, rafiki yake wa kike, Dasha Zhukova mwenye
miaka 29 na wageni wengine ndiyo wataburudishwa na bendi hiyo ya hip-hop ya Marekani, kwenye eneo lake la eka 70 la kisiwa cha St Barts alilolinunua kwa pauni milioni 58.

Alisema kutakuwa na mapochopocho kibao kwa ajili ya wageni, pamoja na vinywaji katika eneo hilo ambalo liko kwenye mwinuko lililozungukwa na maji.Binti wa Abramovich, Anna mwenye miaka 18, anasemakana ni rafiki wa nyota wa kundi hilo la Black Eyed, WILL.I.AM na ndiye aliyechagua.

Tajiri huyo Desemba 9, mwaka huu alinunua boti mpya ya kifahari ambayo ni ndefu zaidi kuliko zote duniani.

No comments:

Post a Comment